HATIMA YA UCHUMI NCHINI TANZANI
andiko hili lina sehemu tatu,
sehemu ya kwanza inaelezea maana ya uchumi
sehemu ya pili, inaelezea mifano ya baadhi ya taasisi mamlaka zinazofanya vizuri kwenye maeneo yao ya utendaji
sehemu tatu, inaelezea pendekezo la nini kifanyike Ili kuwa na Uchumi imara nchini Tanzania.
MUSTAKABALI WA UCHUMI NCHINI TANZANIA
1; UCHUMI, Uchumi ni jumla ya shughuri zote za kibinadamu zinazo lenga kutosheleza mahitaji yao, kutawala na matumizi sahihi ya rasilimali zinazopatikana. Mfano, uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali zinazo lenga kutatua changamoto za kijamii ili kuweza kutawala rasilimali.
Uchumi huchochewa na shughuri mbalimbali za kimaendeleo kama vile, kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji wa madini, biashara, viwanda n.k. Pia unaweza kusema, Uchumi ni jumla ya maendeleo yote ndani ya nchi.
Maendeleo ya kiuchumi ndio hutumika kuweka mataifa katika matabaka mbalimbali ya kiamaendeleo, Mfano, nchi zilizo endelea, nchi zinazo endelea Au Nchi zenye uchumi wa juu, Nchi zenye uchumi wa kati na nchi zenye uchumi wa chini.
Kwa maana hiyo, ni vema nchi kuwekeza nguvu kubwa katika kuimarisha uchumi wa nchi kuliko nguvu zinazowekezwa kwenye sekta nyingine, kwasababu nchi zenye uchumi imara zinaweza kujisimamia na kuweza kuwa na uhuru katika kufanya maamuzi ya mambo yake yenyewe kama vile, uhuru wa kisiasa, ulinzi n.k. Kabla sijatoa pendekezo la suluhisho au mustakabali wa uchumi katika nchi yetu ya Tanzania, natoa mifano ya baadhi ya taasisi/wakala au mamalaka zinazofanya vizuri Katika maeneo yao ya utekelezaji hapa chini.
2; Kwa mfano Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ilianzishwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Baada ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitisha msaada wa sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 mnamo tarehe 16 April, 2007.
TAKUKURU Imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na cha kuridhisha, Hii inatokana na usimamizi madhubuti wa viongozi wa taasisi. Januari 28, 2021, Taasisi ya utafiti ya kimataifa ijulikanayo kama Transparency International (TI) ilitoa taarifa ya hali ya rushwa kwa mwaka 2020 duniani, ambapo Tanzania ilishika nafasi ya 94 kwa kupata alama 38 kati ya nchi 180 duniani zilizofanyiwa utafiti, alisema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Brigedia Jenerali Mbungo, kwenye kikao alicho fanya na wandishi wa habari.
Aidha alikumbusha kuwa mwaka 2015 wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani, takwimu za Transparency International za kupima hali ya rushwa nchini zilisema kuwa, Tanzania ilipata alama 30/100 na kushika nafasi ya 117 kati nchi 180 zilizo fanyiwa utafiti. Taarifa hiyo ya mwaka 2021 ulionesha kua, Tanzania ilipanda alama 8 na kuzipita nchi 23 ndani ya kipindi cha miaka mitano tu. Kulingana na taarifa hiyo Tanzania ilishika nafasi ya 2 katika jumuiya ya Afrika Mashariki. ( habari kamili kutoka diramakini). Haya ni matokeo ya usimamizi madhubuti ya uongozi wa TAKUKURU.
Tanzania Rural and Urban Road Agency (TARURA). TARURA ni wakala wa barabara za vijijini na mijini, iliyofunguliwa rasmi na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa tarehe 2 julai 2017. TARURA imeweza kufungua maeneo mengi hasa maeneo ya vijijini na kuyafanya yafikike kwa urahisi. Hapo awali kabla ya ujio wa TARURA watu wanaoishi vijijini kama wakulima walikua wakipata changamoto za usafirishaji wa mazao hasa kipindi cha masika. Wakulima walikua wakikodi magari yenye uzito mdogo kwa ajili ya kusomba mazao kutoka mashambani, kitu ambacho kilikua kikiongeza gharama za mazao, ambazo wakulima wengi walikuWa wanashindwa kuzimudu.
Kwa kipindi cha miaka mitano, TARURA imefanikiwa kuongeza urefu wa mtandao wa barabara za wilaya kutoka kilometa 108,946.59, kati ya hizo, 56,624.59 zilitangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali (toleo la juni 25,2021) mpaka urefu wa kilometa 144,429.77.
Haya ni mafanikiob makubwa yaliyo fikiwa ndani ya mda mfupi ambayo bila uwepo wa TARURA, ingechukua muda mrefu zaidi kufikia mafanikio hayo. Usimaizi madhubuti wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja, kuwepo kwa mamlaka (wakala) ambayo husimamia barabara pekee, kuwepo kwa wasimamizi wenye taaluma, wabobezi katika usimamizi wa rasilimali husika na upatikanaji wa wazabuni wenye uzoefu na weledi katika ujenzi wa barabara na madaraja, ni miongoni mwa vitu vilivyo chochea mafanikio hayo.
Baada ya mifano ya baadhi ya tasisi na sekta zinazofanya vizuri na zenye mafanikio makubwa na ya kuigwa. Yafuatayo ni mapendekezo kuhusu suluhisho la Ujenzi wa Uchumi imara nchini Tanzania.
3; Ili Tanzania iweze kujenga uchumi imara na kuweza kujitegemea, Ni lazima viongozi waweze kuchukua maamuzi yafuatayo, Moja, Kuanzisha wakala/mamlaka amabayo kazi yake ni kusimamia miradi yote inayolenga kuimaarisha uchumi kama vile, kilimo (mfano,kilimo mkakati cha Alizeti Dodoma), ufugaji (Mfano ufugaji Wa Ng’ombe Tanga na Iringa), uvuvi ( mfano, Uchumi wa Bluu Zanzibar). Lengo kuu ni kuhakikisha watekelezaji na wasimamizi wanajihusisha na kusimamia uchumi pekee, Hapa namaanisha kuweka mipaka ya kiutendaji kati ya wanasiaisa na wana uchumi.
Hapa tunaweza kuchukua mfano wa TARURA ambayo imepata mafanikio makubwa ndani ya mda mfupi tofauti na kabla ya uundwaji wake. Pili, baada ya uundwaji wa mamlaka hiyo, serikali chini ya wizara husika, ihakikishe Muundo wa uongozi na utekelezaji unajumuisha wataalamu wa uchumi pia kulingana na mradi husika, Kuanzia kwenye Uongozi wa juu wa mamlaka hiyo mpaka chini kabisa kwa maana ya watekelezaji wa mwisho wa miradi husika ya kimaendeleo.
Hapa tunaweza kutumia mfano wa TAKUKURU Ambayo kutoka Uogozi wa juu mpaka uongozi wa ngazi za chini za utekelezaji kwenye Idara mbalimbali kwa ujumla wake, wote wana taaluma husika . Hii inasidia mtu kufanya kitu kwa kujiamini na kwa ufanisi mkubwa kwasababu anafanya kitu amabcho ana uelewa nacho.
Kuna wataalamu wengi sana wa uchumi, kilimo, uvuvi, ufugaji,m miradi, n.k walioko mtaani, huku miradi ya kimaendeleo ikipewa wasimamizi ambao hawana utaalamu ya kutosha katika maeneo husika. Mfano, mojawapo ya majukumu ya mtendaji wa kijiji/mtaa ni kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao ya kiuongozi.
Ni kitu kizuri kwasababu viongozi wa serikali za mitaa, pia husomea maendeleo ya jamii na uchumi japo sio kwa undani sana, Pia kuna afsa maendeleo wa kata waliosomea maendeleo ya jamii lakini sio usimamizi wa miradi ya kimaendeleo na uchumi kwa ujmla.
Jambo hilo haliwezi Kuwa na ufanisi mkubwa kama ambavyo ingekuwa endapo miradi hii ingepewa wataalamu wa miradi hiyo au wataalamu wa uchumi.
Hivyo ni muhimu kua na mamlaka ya uchumi inayo jitegemea ili kuweza kufikia wananchi wote kiufanisi Zaidi.

Upvote
1