Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Salaam wana bodi,
Hatimaye ule Muswada Tata wa Marekebisho ya Katiba, umewasilishwa rasmi Bungeni leo kwa ajili ya kutangazwa kwa mara ya kwanza chini ya hati ya dharura.
Baada ya hapo ndipo itafuatia hatua ya muswada huo kujadiliwa kwenye ngazi ya kamati kwa muda wa siku nne. Majadiliano hayo, yatafanyika mjini Dodoma kwa siku mbili na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam kwa siku mbili nyingine.
Maoni ya wadau yatajumuishwa na kupelekwa bungeni kusomwa tena kwa mara ya pili na kujadiliwa na wabunge kwa muda wa siku mbili tarehe 18 na 19 mwezi April. Tarehe hiyo kipindi cha jioni, Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu, na around 1:30 usiku, utasomwa kwa mara ya tatu na utapitishwa kwa kauli moja (ya wabunge wa CCM, hata wapinzani wote wakigomea!), na kuwa sheria rasmi. Bunge litaahirishwa mpaka Jummane Juni 7 ambalo ni la kikao cha bunge la bajeti na mchezo kuigiza wa katiba mpya, utaishia hapo, itabaki utekelezaji tuu.
My Take:
Kuawsilishwa huku, ni uthibitisho mwingine wa jinsi serikali yetu ilivyo ni serikali ya kibabe, jeuri na yenye msimamo mkali, ikiamua kitu, imeamua, hata wananchi wake wapige kelele vipi, haitasaidia kitu,
Ni marekebisho ya katiba na sio katiba mpya!.
Naomba kuwasilisha.
Pasco.
==============
MASAHIHISHO:
Muswada uliowasilishwa ni wa namna ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya mabadiliko ya Katiba; public hearing itafanyika Dar na Dodoma - Invisible
Hata Zanzibar nao wameomba kupewa fursa ya Public hearing lakini Spika anadai kuwa Zanzibar wameshauriwa watumie kituo cha Dar es Salaam; Wabunge toka Zanzibar wanapinga hoja hii ya Spika - Invisible
Wabunge wanapendekeza muswada huu ubadilishwe uende katika lugha ya Kiswahili ili wananchi waelewe nini kimo; serikali inadai inafahamu umuhimu wa kutumia kiswahili lakini hawakufanya tafsiri ya kiswahili na wanatambua kuwa huo ni upungufu, wanaamini wananchi watapata watu wa kupata tafsiri na wao hawadhani kama ni kikwazo sana - Invisible
Zitto anasisitiza muswada wenyewe ndio kwanza wabunge wameupata na hawajaupeleka kwa wananchi kuujadili, anaona hakuna udharura kwani wabunge lazima kwanza washauriane na wananchi juu ya mabadiliko haya - Invisible
Spika anadai mmoja wa watu walotaka uwe na uharaka ni Zitto hivyo anamshangaa kuwa inakuwaje atoe hoja hiyo - Invisible