SERIKALI: TUNASHUGHULIKIA MADAI YA WAFANYAKAZI WA SGR KUHUSU MALIPO YA NSSF
Your browser is not able to display this video.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David M. Kihenzile amesema Serikali inafahamu kuwa Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa SGR (Yapi Merkezi) anasuasua kwenye kufanya malipo katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa watumishi wake katika mradi huo licha ya kuwa Sheria inaeleza anatakiwa kuwasilisha malipo haraka iwezekanavyo.
Akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge Mashimba Mashauri Ndaki, Naibu Waziri amesema wameshaanza vikao na Ofisi ya Waziri Mkuu kushughulikia changamoto hiyo ili Mkandarasi awe analipwa mara tu anapolipwa fedha na kisha kuwalipa Wazabuni wengine wa ndani.
Akiongezea majibu kuhusu hoja hiyo, Prof. Joyce L. Ndalichako ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) amesema:
“Nakiri kweli kuna madai ambayo Mkandarasi anadaiwa na Mfuko unafuatilia, tayari kuna makubaliano kati ya NSSF na Mkandarasi ili madeni yalipwe ndani ya mwaka mmoja pia kuna utaratibu maalumu wa kuwalipa wale ambao wanastahili kulipwa.”