Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni

Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Muswada huo umesomwa Leo Septemba 23, 2022 Bungeni Dodoma ambao unalenga kuweka misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi za wananchi, Kuweka Kiwango cha Chini cha Matakwa ya Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi, na Kuanzisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Masuala mengine muhimu ni pamoja na Kuimarisha Ulinzi wa Taarifa Binafsi Zinazochakatwa na Vyombo vya Serikali na Vyombo Binafsi pamoja na Mambo mengine yanayohusiana na jambo hilo.

Jamii Forums kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za Kisheria walishiriki katika kushauri na kuandaa masuala kadhaa kuhusu Muswada huo ambayo yaliwasilishwa Serikalini kwa ajili ya kupitiwa na kujadiliwa.
 

Attachments

... naomba kujua faida na hasara za hii sheria.
 
Back
Top Bottom