Muuaji Shoga Aliyepukutisha Wenzake...!

Kisa kinasisimua sana, usimuliaji utafikiri Riwaya za Mtobwa lol....
Mkuu bongo kungekuwa na soko la kueleweka kwenye tasnia ya Vitabu ningekutafuta tuangalie ni namna gani kitu ya namna hii tuingize sokoni, last time ulitupa kile kisa cha Uingireza ambapo kuna yule jamaa anatuhumiwa kwa mauaji ya mkewe afu na yeye akajiua japo ulisema ile bado Scotland Yard wanakomaa!
Pamoja na kwamba ni unatafsiri toka huko kwenye sources zako, hyo haizuii mng'ao wa kipaji chako mkuu...
Nashukuru kwa kuishehenesha JF.
Kwa kurudi kwenye stori, hao FBI hawakuwa makini hata kidogo na hamna kazi waliofanya,
najaribu kuimagine hyo kazi ingefanywa na Special Agent Molles yule wa kwenye movie ya Colombiana hahahahahaha si unakumbuka alivyombaini Cantalinhia kwa kapicha kamoja kalikoingia kwenye system zake lol....
Mwaka 97 sidhani kama teknolojia ilikuwa chini kihivyo kwa America.
Au we unasemaje?
 

Kwanza Ahsante sana Bwana JouneGwalu kwa Compliment.
Kusema kweli nimekuwa muumini mkubwa wa hizi crime investigation na hiyo imenifanya niwe mtafutaji wa kesi za kushangaza mtandaoni na kujaribu kuzitafsiri kwa kwa kiswahili kwa namna ya simulizi yenye kuvutia na isiyochosha kusoma. Nashukuru kwa mwitikio nilioupata kutoka kwa wasomaji wote wawe ni member wa JF na wale wasio member wa JF.


Nikija kwenye maoni yako juu ya kitabu kwa kweli, hilo wazo lako ni zuri, lakini kama ulivyosema kuwa soko la vitabu hapa nchini sio la kuvutia sana, na linachosha kwa kweli. Sisi hatuna utamaduni wa kupenda kusoma vitabu na hilo limesababisha watunzi wengi wa riwaya kufa moyo na kutafuta shughuli nyingine za kufanya. Wenzetu raia wa nchi nje hususan wale wa Ulaya na Amerika wao wana utamaduni wa kupenda kusoma. hebu chunguza hata wale walioko hapa nchini utawakuta kila wanapoenda hawakosi vitabu vya kusoma kwenye mikoba yao. Akiwa wanaendesha gari halafu kukawa na foleni atatoa kitabu chake na kuanza kusoma, akiwa kwenye foleni ya huduma fulani anatoa kitabu chake na kuanza kusoma.............. yaani hakuna muda utapita tu hivihivi bila kuutumia kuingiza kitu kichwani..............huo ndio utamaduni wao.

Nakumbuka kuna siku niliingia Internet cafe moja pale mwenge nikiwa na kitabu ambacho ndio nimetoka kukinunua tena kwa shilingi 75,000.......... Niliondoka na kukisahau kile kitabu pale, nilikumbuka nikiwa nyumbani usiku. nikajua kitakuwa kimepotea.
Siku mbili baadae nilipita pale kama kubahatisha, na nilishangaa kukikuta kikiwa pale pale nilipokiacha. nilikichukua na kuondoka nacho na wala hakuna aliyejishughulisha kuniuliza.

Kuhusu Movie ya Colimbiana, nakubaliana na wewe kuwa mwaka 1997 teknolojia ilikuwa pana sana, lakini tukumbuke tu kuwa wakati mwingine kuna kuwa na uzembe au tuseme kuwa ajizi katika kufuatilia kesi fulani kwa sababu ya kutokuwa na uzito kwa jamii. Mara nyingi Polisi wetu na sio hapa nchini tu bali pia duniani kote wana kawaida ya kuzipa kesi uzito kulingana na jinsi jamii itakavyoichukulia kesi hiyo, kama aliyeuliwa hana uzito wowote katika jamii, basi itawekwa kapuni.....................na maisha yataendelea kama kawaida.
 
Asante nimeelewa sasa kwanini Gianni Versace was murdered. Nilihisi tu alikuwa shoga and though mafias killed him kwasababu za kibiashara.
 
Ni ndefu, lakini ni nzuri kama ukiisoma weekend ukiwa nyumbani umejipumzisha...............
Tamu sana hii. Na hakuna urefu wowote hapa labda kwa watu wenye matatizo ya macho! Kitu imeisha mi natamani ingeendelea!
 
Du nice nitaipitia baadae ngoja niperuzi au nii-Bookmark
 
@ Braza Mtambuzi, unajua mwanzoni nlidhani hii stori umeichomoa mahali fulani, lakini kama umeiandika mwenyewe bado lazima nikubali kwamba unacho kipaji cha story-telling..mkuu keep it up na uangalie jinsi ya kufaidika na kipaji na hobby yako.
 

Mi si mpenzi sana wa simulizi ndefu lakini leo nimepatikana huwezi kuishia kati stori hii ,hata kama ndefu.
 
Nilitaka nikusalimie mkuu,
binti yako cantalisia amenielekeza kuwa upo hapa sebuleni kwako,
asante kwa hii story,
mimi niliisoma kule kwenye blog yako ni nzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…