Muuaji wa kimya kimya wa Wanaume na Wanawake huyu hapa!

grafani11

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Posts
15,441
Reaction score
5,816
Pamoja na kuonekana kuwa ni fasheni (mtindo) inayowapendeza wanawake wengi na inayopata umaarufu zaidi kwa vijana wengi nchini wakiwemo wasanii, ukweli ni kuwa suruali za jeans na zinazobana maarufu kama "skinny jeans"… ni bomu linaloleta madhara taratibu.

Uchunguzi wa kitaalamu umebainisha kuwa suruali za kubana hasa za jeans zinasababisha maradhi mbalimbali ikiwemo kuharibika kwa mishipa ya fahamu, fangasi sehemu za siri na kupungua kwa nguvu za kiume (kwa wakina baba).Hii ni kwa sababu zinaibana mishipa inayosambaza damu mwilini hasa katika mapaja, kibofu cha mkojo na korodani hivyo kushindwa kusambaza damu katika baadhi ya maeneo.
Baadhi ya maeneo ambayo huathirika zaidi ni mapaja, kibofu cha mkojo kwa wanaume, nguvu za kiume na kufa ganzi kwa miguu kwa wanawake. Wataalamu wa afya wanasema kuwa unapovaa suruali ya kubana sana mishipa midogo midogo inayosafirisha damu nayo hubanwa.

Kwa kawaida damu husafiri kwa kasii kama maji hivyo misuli inapobanwa damu hushindwa kusafiri na kusababishaneva za fahamu kufa au kuharibika (Dk. Makgato Thabo wa Milpark Hospital, South Africa).
Kliniki ya Mayo inaeleza kuwa suruali za jeans zinazobana huiua mishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mapaja kufa ganzi kwa kitaalamu unaofahamika kama "Meralgia Paresthetica", ambao husababishwa na kubanwa kwa neva.

Dk. Jones anayefanya kazi katika kampuni ya TENA alieleza kuwa wanaume wanapata matatizo zaidi kwani huweza kuharibu mfumo wa mkojo na kupinda kwa korodani. Amewashauri wanawake wa wanaume kuacha nafasi kubwa katika maeneo nyeti. Ni vizuri kuhakikisha suruali na nguo ya ndani vinapata nafasi na wala usibanwe kwa namna yeyote.
Hakuna ubishi wanaume wanaovaa mavazi ya kubana wanaharibu afya zao. Kupinda kwa korodani kunatokea pale suruali inayobana inapozuia mirija ya mbegu za kiume kutembea kwa uhuru. Hivyo mbegu hushindwa kusafiri katika njia yake na kupita katika njia nyingine jambo ambalo husababisha kusimama kwa usambazaji wa damu.

Pia, suruali za kubana huongeza msukumo katika kibofu cha mkojo jambo ambalo husababisha bakteria kuzaliana na kuingia katika mwili hivyo kusababisha kuathirika kwa mirija ya mkojo.
Dk. Jones anashauri watu kuvaa suruali za jeans za kubana lakini zinazovutika ili kujiondoa katika hatari inayowakabili.

Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya mwili , Meshack Shimwela anasema ni jambo la kweli kuwa wanaume kuvaa nguo zinazobana huathiri kuzalishwa kwa shahawa kwa kuwa maeneo ya korodani yanahitaji nafasi, kule kubanwa kunasababisha mbegu za kiume zisizalishwe inavyotakiwa.
Pia anaeleza kuwa licha ya suruali za kubana wasichana wanaopenda kuvaa nguo za ndani zinazobana sana, wanajiweka katika hatari ya kupata maradhi ya fangasi kwa sababu ya joto jingi.

Dk. Sydney Yongolo (Bingwa wa masuala ya mfumo wa mkojo kwa wanaume na uzazi kwa wanawake) anasema korodani zinahitaji joto la kadri ili kufanya kazi vizuri na kuzalisha shahawa.
Inapotokea zikabanwa sana mishipa midogomidogo inayofanya kazi ya kusambaza damu na kuzalisha mbegu hushindwa kufanya kazi. Inafahamika kuwa wakati wa baridi korodani hupanda juu kutafuta joto n awakari wa joto hushuka ili kutafuta joto la kadri.

Hivyo basi, endapo mwanaume amevaa suruali za kubana korodani hushindwa kupanda au kushuka kama kawaida yake. Ni kama yai la kuku, wakati wa kuatamiwa linahitaji joto la kadri kwa siku 21 ili kifaranga kizaliwe, hivyo ndivyo ilivyo kwa mbegu za kiume.
Dk. Yongolo anaongeza kuwa si suruali pekee, bali hata nguo za ndani zinazobana husababisha madhara makubwa kw awanaume na wanawake n andicho chanzo cha ugumba. Maeneo hayo yanahitaji nafasi, kwa sababu joto likizidi au likipungua uzalishaji na mfumo wote hubadilika.

Dk. Karen Boyle wa Hospitali ya Greater Baltimore, Uingereza anasema kwa bahati mbaya tatizo hili huwa kubwa zaidi kwa wanawake wanaovaa suruali za jeans za kubana sambamba na viatu vyenye kisigino kirefu.
Anasema, wanawake wanaovaa viatu vyenye visigino virefu pamoja na suruali za kubana misuli yao hukaza, mishipa hushindwa kusafirisha damu na hivyo kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kufa ganzi kwa miguu na mapaja. Baada ya muda, wanapata misuli midogomidogo yenye rangi ya kijani, jambo linaloonyesha usafirishaji duni wa damu katika maeneo hayo.
 
Mkuu grafani11 kwa vijana wanasema ni fashion bana huwezi wanyima kuvaa hiyo mibanano
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ndiyo maana Vodacom wana kauli mbiu yao, "Kazi ni kwako". Waache wavae tu fainali uzeeni.
grafani11 huwa nawaangalia sana hao wanaovaa hizo mbanano najiuliza maswali sana wakati wa kuvua anavuaje na the way misuli ya miguu na mapaja ilivyobana haoni kuwa anazuia damu kutembea na mali halisi za wanaume ambazo zinahitaji kuwa free hawaoni kuwa wanazibana bana zinakosa mpaka hewa na kupumua
 
Last edited by a moderator:
Duh, kama hivi ndivyo ilivyo basi mimi sitakufa kwa matatizo haya labda mengine maana mimi hua sioni umuhimu wa kuvaa hata pichu, waht for? kufuli elfu kumi, kumi na tano? nani ataona kama nimevaa kufuli au sijavaa? huwa najiskia raha sana nikipata kaupepo naskia kanaua bactria, MIMI sivai kabisa hio kitu na nikilala ndio usiseme sasa au nikishinda home
 
mimi ni mwendo wa vibukta tu zenye material ya pamba chupi niliachana nazo tangu school suruali kitambaa hizi jeans za siku hizi hata siziwezi
 

teh teh...dah!...
 
Manufacturing na upumuaji vitafanyika usiku saa za kulala. Kama hizi kubana zingesababisha shida nahisi nisingezaliwa. Mzee Mtambuzi enzi zake alikuwa anavaa high heels aka raizoni na sarawili m'bato tena ya mpira!

Cc Kongosho
 
Last edited by a moderator:
hakuna muunganiko wa kichwa cha habari na habari uliyoandika!
 
He he he, si ndo maana unaona alizaa mtoto kavuta bhange from manufacturer?

Mie saa hivi ni madera hadi ofisini, unantaka!

Manufacturing na upumuaji vitafanyika usiku saa za kulala. Kama hizi kubana zingesababisha shida nahisi nisingezaliwa. Mzee Mtambuzi enzi zake alikuwa anavaa high heels aka raizoni na sarawili m'bato tena ya mpira!

Cc Kongosho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…