Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Bunge Maalum la Katiba limegeuka kituko. Bungeni kuna kelele,ubabe,misimamo na zomeazomea. Bunge halifanyi linachotakiwa kufanya.Linafanya kinume na matarajio ya watanzania. Kila mmoja wetu aweza kutafuta na kupata sababu zake juu ya kinachoendelea Bungeni. Na mimi nina sababu yangu moja niionayo kama kuu kabisa
Sababu yenyewe ni muundo wa Bunge hili Maalum la Katiba. Katika mfumo na wakati wa sasa wa vyama vingi,isingetakiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi kufanya sehemu ya Bunge Maalum la Katiba. Kufanya hivi ni kurudia kilichofanyika mwaka 1977 ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilijigeuza kuwa Bunge Maalum la Katiba. Ni yale yale tu.
Mwaka 1977 lakini mambo yalikwenda salama salmini.Kwakuwa kulikuwa na chama kimoja na msimamo mmoja.Lakini sasa mambo ni tofauti.Bunge la sasa lina mchanyato mkali kabisa.Wa kivyama na taasisi mbalimbali.Ni vigumu kupata muafaka katika mazingira ya sasa.
Hoja yangu kuu ni kuwa Wabunge wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hawakupaswa kuingia moja kwa moja katika Bunge Maalum la Katiba. Nani hajui tamthilia na komedi zilizokuwa zikiendelea katika Bunge leytu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa imeshakuwa ndiyo tabia ya Wabunge hao ambo sasa ni sehemu ya Bunge Maalum la Katiba.
Kuwaweka hawa pamoja na wageni ni kuuita mchuano mpya.Wao wanajiona wanajua kila kitu,wanazijua taratibu zote za kibunge,wanahaki ya kuonge na kusikilizwa kuliko Wajumbe wengineo na kadhalika na kadhalika. Wajumbe waliotokana na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ndiyo tatizo.Wamejaa kiburi na ujuaji mno. Na wageni hawatakubali kushindwa na kufunikwa.
Ni dhahiri mivutano itashamiri kila uchao. Na kupata Katiba mpya kutafifia kadiri siku 70 zinavyoenda ukingoni.Ilibidi Wajumbe wote wachaguliwe na wananchi au wateuliwe.Angalau wangekuwa wapya watupu toka taasisi na kada mbalimbali za kimaisha. Nasema,Wabunge ndiyo tatizo Bungeni (Bunge Maalum la Katiba).Na ukweli huu utajidhihiri hivi punde!!