Muundo wa Bunge ndiyo kiini cha tatizo

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Bunge Maalum la Katiba limegeuka kituko. Bungeni kuna kelele,ubabe,misimamo na zomeazomea. Bunge halifanyi linachotakiwa kufanya.Linafanya kinume na matarajio ya watanzania. Kila mmoja wetu aweza kutafuta na kupata sababu zake juu ya kinachoendelea Bungeni. Na mimi nina sababu yangu moja niionayo kama kuu kabisa

Sababu yenyewe ni muundo wa Bunge hili Maalum la Katiba. Katika mfumo na wakati wa sasa wa vyama vingi,isingetakiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi kufanya sehemu ya Bunge Maalum la Katiba. Kufanya hivi ni kurudia kilichofanyika mwaka 1977 ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilijigeuza kuwa Bunge Maalum la Katiba. Ni yale yale tu.

Mwaka 1977 lakini mambo yalikwenda salama salmini.Kwakuwa kulikuwa na chama kimoja na msimamo mmoja.Lakini sasa mambo ni tofauti.Bunge la sasa lina mchanyato mkali kabisa.Wa kivyama na taasisi mbalimbali.Ni vigumu kupata muafaka katika mazingira ya sasa.

Hoja yangu kuu ni kuwa Wabunge wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hawakupaswa kuingia moja kwa moja katika Bunge Maalum la Katiba. Nani hajui tamthilia na komedi zilizokuwa zikiendelea katika Bunge leytu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa imeshakuwa ndiyo tabia ya Wabunge hao ambo sasa ni sehemu ya Bunge Maalum la Katiba.

Kuwaweka hawa pamoja na wageni ni kuuita mchuano mpya.Wao wanajiona wanajua kila kitu,wanazijua taratibu zote za kibunge,wanahaki ya kuonge na kusikilizwa kuliko Wajumbe wengineo na kadhalika na kadhalika. Wajumbe waliotokana na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ndiyo tatizo.Wamejaa kiburi na ujuaji mno. Na wageni hawatakubali kushindwa na kufunikwa.

Ni dhahiri mivutano itashamiri kila uchao. Na kupata Katiba mpya kutafifia kadiri siku 70 zinavyoenda ukingoni.Ilibidi Wajumbe wote wachaguliwe na wananchi au wateuliwe.Angalau wangekuwa wapya watupu toka taasisi na kada mbalimbali za kimaisha. Nasema,Wabunge ndiyo tatizo Bungeni (Bunge Maalum la Katiba).Na ukweli huu utajidhihiri hivi punde!!
 
Laiti wangekubali pendekezo la CHADEMA kuwa Rais asiwachague hawa viumbe Leo Hii pengine tusingeona huu upuuzi na uvundo unaoendelea. Pengine aliewachagua na yeye ni kama wao!!!!
 
Kama simiyu yao ni mbunge unategea nini? Mburura kuwakilisha watu
 
Tatizo ni Wabunge toka Zanzibar ni wabishi na wakorofi sana lakini Nadhani wametumwa maksudi ili wacheleweshe katiba ya muungano ili katiba ya Zanzibar izidi kujimaarisha zaidi wapo Dodoma kuvuna Posho huku wakiwashangaa Tanganyika kuhangaika na Katiba ya Muungano wakati Tanganyika Binafsi haina katiba yake ! Wanajiuliza wapi zitapatikana Pesa za kuja kuandaa katiba ya Tanganyika baadae ! Kwa kweli uwezekano wa kupata katiba yenye kukemea Yale mabaya Kama Ushoga Uvaaji wa hovyo hovyo kwa wanawake wa siku hz utakuwa Mdogo sana Sababu katiba itaandaliwa haraka haraka na kusahau Maadili ya Mtanzania matokeo yake ni Uvaaji mlegezo Kuwa rasmi na kuzalisha Kizazi cha ajabu
 
Katiba Mpya ikitamka Kuwa Mwaka 2015 uwe Ndio mwisho wa Serikari kuishi Dsm wahamie Dodoma Mara moja hakika itakuwa katiba Bora kinyume na hapo katiba itakuja kulalamikiwa kwa kushindwa kuihamisha Serikari na kulinusuru jiji la Dsm na kero ya Foleni kubwa .
 
Hiyo katiba Mpya ije na Utaratibu mpya wa kuhakikisha Wabunge wanakuwa wakazi harisi wa Jimbo husika na Katiba ikataze Wabunge kuhamia Dsm Mara baada ya kupata Ubunge angalau sasa wabunge wataishi huko Majimboni na kupunguza Msongamano jiji Dsm
 

Mambo yafuatayo ni kiini cha tatizo
1. Uwepo wa wajumbe kutoka Bunge la JMT na BLW
2. Kuruhusu mijadala kama ile ya wakati wa kutoa maoni iendelee kuwepo tena na watu ambao ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, mbaya zaidi inafanyika mjini Dodoma, kama ile maamuz ya CC n.k! Angalau ingekuwa inafanyika mikoa mingine mbali na Dodoma ingekuwa afadhali!
3. Hili linashabihiana na namba1, kuruhusu wajumbe wa kuteuliwa, wengi wao ni wanasiasa waliopitia mlango wa nyuma kwa kupitia asasi mbalimbali kama ile yenye utata inayoitwa: Kundi la watu Wenye Malengo yanayofanana.
 

Sahihi kabisa Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…