Muundo wa Katiba

Muundo wa Katiba

Gabriel Gavu

Member
Joined
Aug 18, 2017
Posts
10
Reaction score
3
Napenda kujadiri:- Haya malumbano ya kila mmoja mwenye wadhifa kutoa matamko yake bila kuzingatia taratibu yanatokana na mamlaka kubwa wanayokabidhiwa na idadi ndogo ya watu anaowajibika kwao mteuliwa. Wazo langu ningependa katiba kwenye utawala iseme hivi:-

1 Jaji Mkuu na mwanasheria mkuu wa serikali, awekwe na majaji wenzake asiteuliwe na Rais - hii itasaidia kuwawezesha majaji au jopo la wanasheria kumuhoji Jaji mkuu pale wanapoona taratibu zinapindishwa. Pia anaweza kuwa na nguvu ya kumpinga Rais kama kutakuwa na kuhitilafiana juu ya masilahi ya nchi. mfano Marekani Trump wameweza kumpinga baadhi ya mambo kwa kutumia pawa kama hizo za uhuru wa chombo husika.

2 Mbunge cheo cha mwisho kiwe ubunge ili dhana ya kujiosha kwa wakuu wa nchi ili sikumoja aje apewe uwaziri ife wabaki wanag'ang'na kuwatetea wananchi. Baraza la mawaziri watoke kwenye Taaluma zao za wizura husika.

3 Baadhi ya watenda wa serikali watazamwe upya kama siyo kuondolewa Mfano katibu tarafa, kati ya mkurugenzi na katibu tawala wilaya pia watazamwe uwepo wao.

4 Mwana siasa yeyote asiruhusiwe kufanya biashara na ngazi anayoiongoza kama tenda/zabuni ili kuondoa shinikizo la matumizi yasiyo sahihi na kuongeza nguvu ya kuwahoji kama kutakuwa na halufu ya matumizi mabaya au rushwa.

5 Bunge la katiba lisihusishe wabunge waliopo madarakani kwa sababu wao wameapa kuilinda katiba iliyopo hivyo ni vigumu kuikosoa kwa sababu pia hata wao wana masilahi ndani yake.

6 Tume ya uchaguzi isiteuliwe na Rais badala yake jopo la majaji, wakuu wa taasisi mbalimbali, uongozi wa bunge, na wawakilishi walioandaliwa na wananchi wakae pamoja ili kupendekeza na kuiteua tume ya uchaguzi huru.

7 Kuwepo na Serikali moja ya Tanzania na kufuta baraza la mapinduzi hii ya kudai serikali za mashilikisho zihusu nje ya Tanzania. Lakini wananchi wapewe haki ya kuelimishwa juu ya taifa lao nje na mfumo wa kisiasa ambao unaendeshwa kikampeni kwa kutetea sera za vyama vyao.

Kwa uchache Nipo tayari kuelimishwa, kukosolewa na kujifunza nikajua ambapo sikupaelewa. Karibuni.
 
Back
Top Bottom