Wadau,
Rasimu ya pili ya katiba mpya imejikita kwenye katiba ya serikali ya Muungano kama muundo wa serikali utakuwa wa serikali tatu.
Je ikitokea muundo wa serikali tatu ukakataliwa, nini kitatokea? Tume ya katiba ambayo ndio ingeweza kupewa kazi ya kuiandika upya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa maana ya serikali mbili) tayari imeshavunjwa. Sidhani kama bunge la katiba litakuwa na wataalamu wa kuweza kuanza kuiandika upya katiba hiyo ya Muungano.
Pia sidhani kama bunge la katiba wataweza kuiandika upya katiba ya jamhuri yaMuungano (kwa muundo wa serikali mbili) kwa muda wa miezi mitatu. Ninasema hivyo kwasababu rasimu ilivyo sasa haina mambo hata nusu ya yanayotakiwa kama muundo wa serikali utakuwa serikali mbili.
Huenda tulifanya makosa tokea mwanzoni na tungeiruhusu tume ya kuandaa katiba mpya, ingeandaa muundo wa serikali zote tatu yaani serikali moja, serikali mbili na serikali tatu na kisha wao wakapendekeza serikali tau kama walivyofanya sasa. Ili kama serikali tatu inakataliwa basi tunaingia kwenye pendekezo la pili nk.
Kwa jinsi hali ilivyo sasa, kama serikali tatu itakataliwa basi huenda kazi nzima ya tume ya katiba ikawa imepotea.
Kwa wenye ujuzi na mambo ya katiba, je mna maoni gani na hii hali kama itatokea muundo wa serikali tatu ukakataliwa na bunge la katiba?