Ndugu wadau, mimi naomba nichokoze hoja ya muundo wa serikali ya Tanzania. Napendekeza iwe na serikali moja na wala si mbili wala tatu. Tumeona jinsi kero za muungano wa Jamhuri wa Tanzania zilivyowashinda aliyekuwa waziri Mkuu na waziri Kiongozi. Na baadaye akakabidhiwa makamu wa rais naye ameshindwa. Kwa hiyo binafsi napendekeza serikali moja t ambayo itakuwa na waziri Mkuu na kwa znibar atakuwa waziri Kiongozi. Hii inamaana kuwa seriali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar zitaongozwa na mawaziri. Kwa Tanganyika atakuwa Waziri Mkuu na kwa Zanzibari atakuwa waziri Kiongozi.
Kwa hiyo swala la serikali mbili au tatu litakufa kifo cha mende. Nimemsikiliza Dr. Shein wakati akifungua madhimisho ya miaka 50 ya Muungano akiwa zanzibari, akawa anajiumauma. Anasema kero za muungano zitatatuliwa. Na nani na lini? Wakati tumeshawatumia Makamu wote wawili na mawaziri Mkuu na Kiongozi na wote wameshindwa kutatua kero hizo za Muungano. Mimi nadhani ili kuepuka mkanganyiko huo, kwanza tujindae kuwa na serikali moja na zanzibari ikubali kuwa sehemu ya jamhuri wa Tanzana na Tanganyia irudi. Hivyo ni lazima katiba ya zanzibari ifumuliwe na katiba ya Tanganyika iandikwe kwanza.
Nawasilisha