Muungano hali, Azimio la Arusha chali: Matokeo ya maguvu ya ccm na policcm...?

Muungano hali, Azimio la Arusha chali: Matokeo ya maguvu ya ccm na policcm...?

Nara

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2009
Posts
1,067
Reaction score
297
Ndugu wana jf na wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii. Napenda kutoa angalizo.

Kwa kiasi kikubwa sana muungano umemomonyoka, na unazidi kuendelea kumomonyoka. Kufuatia rasimu mpya ya kaitba, mpka sasa hakuna matumaini kwamba muungano huu utaendelea kudumu.

Duru za siasa mkoani Arusha, maarufu kama A- town, zinaonyesha kwamba tokea ushindi wa ubunge wa cdm 2010 umaarufu waccm umeshuka sana, unaendelea kushuka sana kufuatia ushindi wa cdm katika kata za babati na mbulu. Ni wazi kwamba on 30th june, cdm wataenda kupigilia msumari kwenye kidonda.

Kwa kifupi tu, haya matukio mawili yanaishara kubwa sana kihistoria. Azimio la arusha la mwaka 1967 na Mungano wa zanzibar na Tanganyika wa mwaka 1964, ni matukio makubwa sana kihistoria kwa taifa na ccm. Kwa upande wa ccm, matukio haya unaweza kusema ndo hasa yaliyopelekea kuzaliwa kwa hichi chama mnamo mwaka 1977. Kwa hiyo, kihistoria, ukiachana na mambo mengine ya kiuchumi nk, Arusha na Zanzibar vimekuwa kama uti wa mgongo wa ccm. Kwa sababu hiyo, unaweza kuhusisha matumizi ya nguvu nyingi sana kutuliza upizani Arusha na Zanzibar na harakati ya kulinda historia hii.

Kama ccm wanasoma alama za nyakati basi wasikie neno hili linalosemwa, muungano chali, azimio la arusha chali, kinachofuata nini muasisi wa hayo, ccm. Automatically, Chama cha CCM kitapoteza maana pasipo hizi nguzo kuu, hawatakuwa na agaenda tena, wazee wao ambao ndo waasisi wamekaa kimya wakiongea hawasikilizwi. Tatizo hili ni kubwa kuliko watu wanavyodhani na ni wenye busara wachache sana wanaoweza kuliona. Sehemu moja ambayo imeathirika sana sana na maradhi ya ccm ni police, usalama wa taifa na wakuu wa mikoa. Hizi ni sehemu nyeti sana kwa taifa, lakini ccm wamezivuga kabisa.

Kwa wale wanao ijua ccm, bila azimio la arusha na muungano ccm itakufa tuuuu!!! Hii ambayo inaitwa ccm sasa hivi siyo ccm, ni kitu kingine kabisa, hilo watu inabidi wajue, hasa wale wanaosema ccm ndo imeleta uhuru. Nasisitiza tena, CCM inayoongoza bila azimio la arusha na muungano haiwezi kuwa ccm, ni chama kiingine kabisa, ndo maana tunashhudia vituko tu. Kwa sisi vijana wa sasa, ccm ni pongo la walarushwa, wezi, mafisadi, watu wasiona maadili ya uongozi, watu wasio na elimu wala ubunifu, watu wasio hekima, watu wanatumia vyeo vyao vibaya, wakabila, wadini, watu wasiojali watu wanaowaongoza, watu waliolewa madaraka, watu wenye majivuno na kiburi wasichostahili, washamba, watu wanaodhani kuwa kiongozi ni kuwa mungu mdogo, kuwa kiongozi ni kuwa superior, kuwa kiongozi ni kuwa juu ya wale unaowaongoza, watu majangili, wauwaji. Haya yote ni kwa sabu bila zimio la arusha na muungano, ccm siyo ccm.

Tafakari!!
 
Mtaji mkuu wa CCM ni wananchi; hayo yote yalifanyika kwa kuwa wananchi waliamini na wanaendelea kuiamini CCM; ridhaa ya wananchi ndio msingi mkuu wa CCM
 
I will repost it just for you!!
 
Nionavo mie pana unafiki mkubwa wa kumuenzi baba wa taifa hili. Baba wa taifa alikiri kutembea na vitabu viwili tu navo ni BIBLIA na AZIMIO LA ARUSHA, hakutueleza kutembea na katiba za chama na taifa lakini kinachofanyika ni kuutetea muundo mbovu huu wa serikali mbili ambao wananchi takriban wengi hawautaki na kuacha kulirejesha Azimio la Arusha ambalo wananchi wengi wanalitaka.
 
Back
Top Bottom