Muungano haujawahi kuwepo-Zanzibar ni "sovereign state" tangu siku ya muungano

Mdanganywa

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
620
Reaction score
342
Kuna watu wanadhani Zanzibar ni nchi tangu mwaka 2010 ilipobadili katiba yake. Nimevutiwa na uchambuzi wa gazeti la RAIA MWEMA lililotufafanulia kwamba kumbe Zanzibar ilibaki kama sovereign stat kama nchi yoyote duniani kwa jinsi nilivyoelewa:

Makala zilizoeleza hilo ni RAIA MWEMA toleo 338 na 339. Naomba mnisaidie kuielewa kwa kuwawekea hapa

GAZETI: RAIA MWEMA
TOLEO: 338
HEADLINE: TATIZO SI WINGI WA SERIKALI BALI SOVEREIGNTY YA ZANZIBAR
WEBSITE: BONYEZA HAPA

**************
JE, uhaini unaweza kufanyika Zanzibar? Je, Zanzibar ni Sovereign State? Je, haiwezekani ZFA kuwa mwanachama wa FIFA hadi ije Katiba Mpya?

Uzito wa hoja hii utanilazimisha ninukuu sana maneno kama yalivyoandikwa nilikoyatoa.

Oppenheim's International Law: A Treatise Vol. I, Peace, 5th Ed, uk. 113, inasema: {"sovereignty is the supreme authority, an authority which is independent of any other earthly authority"}. Yaani, "sovereignty ni mamlaka ya kuwa na kauli au maamuzi yasiyostahili kutenguliwa na yeyote hapa duniani".

Mimi ni mkatoliki. Nikisikia mtu au jamii ina "sovereignty", basi najua kwamba utashi wake hudhibitiwa na Mungu tu.

"Sovereignty" ilianzaje? "Roman Empire" ilipoanguka mwaka 476, umuhimu wa Papa ukaongezeka. Desemba 25, 800, Papa Leo III, alimsimika Charlemagne awe "Holy Roman Emperor", aliyeishi sana Ujerumani ya sasa.

Wafalme wengi wakazidiwa hadhi na "Emperor" huyu. Hapo "Sovereignty" ilikuwa moja tu, ya Papa ambayo hutumia jina "Holy See".

Mwaka 1050, Wamisionari waitwao "Order of Saint John" sasa wanaitwa "Sovereign Order of Malta", walijenga hospitali yao Jerusalem ihudumie Wakristo wanaohiji nchi takatifu. Februari 15, 1113, Papa Paschal II aliwapa Wamisionari hawa mamlaka ya kueneza hospitali zao bila kuingiliwa na mtawala au askofu yeyote duniani.

Huduma zao ziliwafanya waitwe "Hospitallers", kama "Society of Jesus" tunavyowaita "Jesuits".

Vita ya "Crusades" iliwang'oa "Hospitallers" Jerusalem na walikohamia, waliitumia ile ruhusa waliyopewa na Papa iitwayo "extra-territoriality". Hii "extra-territoriality" wengine huiita "diplomatic immunity".

Mwaka 1618, Ulaya ililipuka vita iitwayo "Thirty Years War". Vita ilipoisha, mwaka 1648, ikatungwa mikataba inayoitwa "Peace of Westphalia".

"Westphalia" iliagiza kwamba, dola ya taifa lolote, yaani "state", itakuwa na mamlaka ya mwisho, yasiyoingiliwa na mamlaka nyingine yoyote hapa duniani. Mfano, sasa mfalme wa France, akaacha kuwa chini ya "Holy Roman Emperor". Hivyo, huo 1648 ndipo mataifa mengi Ulaya, yalipopata "State sovereignty".

"Hospitallers" walikuwa sasa wameshahamia kisiwani Malta, wanapatawala kama Netgroup ilivyokabidhiwa kuiongoza Tanesco.

Napoleon alipoivamia Malta, Juni 11, 1789, aliwapindua madarakani "Hospitallers", akaiingiza Malta kimabavu kwenye muungano na France.

Septemba 20, 1870, Jeshi la Italy, liliuteka Roma, mji mkuu wa "Church States", likampindua "Sovereign" wa nchi hiyo, Papa Pius IX, na kumfanya aikimbie Ikulu, akaanza kuishi parokiani Vatican.

"Church States" sasa ikawa ni jimbo tu ndani ya Italy. Ikulu aliyoikimbia Pius IX, iitwayo "Quirinal Palace", ikataifishwa kuwa Ikulu ya Muungano mpya wa Italy hadi leo.

Vatican alikokimbilia Pius IX, pakaitwa "gereza la Italy" kwa yeye kujiita "Prisoner in the Vatican".

Balozi zote zilizokuwa nchini "Church States", hasa jijini Roma, sasa bila kupenda, zikajikuta ziko nchi nyingine kabisa, Italy.

Je, balozi zile zilifungwa? Maana "Church States" haipo tena na Papa waliyemfuata pale hana hata uraia wa Italy, ameshabaki tu "Prisoner in the Vatican".

Kweli "Church States" ilishakufa, lakini "Sovereignty" ya Papa (Holy See) haikufa, kwani hakuporwa na Italy jukumu la kuendesha Kanisa Katoliki.

Hivyo, balozi pale Roma, Italy, hazikufungwa. Ziliendelea kuitwa "Ubalozi wa NCHI kwa Papa", mfano "Embassy of France to the Holy See", huku Italy ikilazimika kuzipa hadhi ya "extra-territoriality".

Uhusiano na Papa, ukaongezeka hadi ubalozi wa "Holy See" ukafunguliwa barani Afrika, Liberia, Desemba 15, 1927, miaka 57 ma-Papa wakiwa bado "Prisoners in the Vatican".

Hata "Sovereignty" ya "Hospitallers" nayo haikufa ule mwaka 1789, kwani hawakuikabidhi France lile jukumu la kuendesha huduma zao za afya.

Kumbe, jukumu unalolihodhi, hata kama ni moja tu, litakupatia "sovereignty", maadam dunia ithibitishiwe kwamba halidhibitiwi kwa namna yoyote na mamlaka nyingine yoyote hapa duniani.

Wapo wahadhiri duniani, wanaodanganya kwamba, Italy iliposaini "Lateran Treaty", mwaka 1929, ndipo Papa akapata "sovereignty", kwa kupata nchi iitwayo Vatican City State!

Uongo huu hukaribisha uongo mwingine usemao hata balozi tunazozijua ni za Vatican, wakati Vatican iliyoanza juzijuzi tu mwaka 1929, haijawahi kufungua ubalozi kokote duniani!

Balozi zote duniani, ukiwemo uliopo hapa Tanzania, ni za "Holy See", ukipenda ziite "Ubalozi wa Papa", wakatoliki tunaziita "Apostolic Nunciature of the Holy See".

Anayeng'ang'ania uongo ule, basi akutajie nchi "Sovereign State" iliyowakilishwa na mabalozi wa Papa toka 1870 hadi hiyo 1929, kipindi Papa alipobaki tu "Prisoner in the Vatican".

Muulize tena, je, hawa mabalozi 104 wa "Hospitallers" duniani, wanawaikilisha nchi au "Sovereign State" ipi?

Unayemuuliza maswali haya, akujibu, asikatishe mazungumzo au kubadili hoja, kama walivyo waongo wote duniani wanaoitwa "relativists" wanapobanwa na ukweli.

Hakuna binadamu duniani anayeweza kukujibu maswali haya mawili, kwa sababu haijawahi kuwepo nchi iitwayo "Holy See" na nyingine " Sovereign Order of Malta".

Mfano wa "Holy See" na "Hospitallers" huthibitisha kwamba, umiliki wa jeshi, polisi, bendera, wimbo wa taifa au nchi yenye mipaka (territory), kamwe si vigezo vya lazima ili upate "Sovereignty".

Tumeona hata wanadiplomasia (Oppenheim's), hawafafanui "sovereignty" kwa vigezo hivi, wala hata hawavitaji.

Tuzilinganishe sasa Zanzibar, "Holy See" na "Hospitallers". Zote zilikuwa na "sovereignty" ya kutawala nchi kabla ya miungano.

Zote zikapata mabadiliko hivi: "Hospitallers" (Juni 12, 1798), "Holy See" (Septemba 20, 1870), Zanzibar (Aprili 26, 1964).

Kwenye tarehe hizo, tumeona "Holy See" haikuporwa jukumu moja tu kwenye muungano wa kuimeza "Church States". Ilibaki nalo kama mwanzo bila kuingiliwa. Hii ndiyo "Sovereignty".

"Hospitallers" nayo, haikukabidhi jukumu moja tu kwenye muungano wa kivamizi, siku France ilipoimeza Malta. Ilibaki nalo kama mwanzo bila kuingiliwa. Hii pia ndiyo "Sovereignty".

Vipi sasa kuhusu Zanzibar? Aprili 25, 1964, Baraza la Mapinduzi Zanzibar, liliujadili na kuukubali Mkataba wa Muungano, uliotaja mambo 11 tu ambayo Zanzibar itayakabidhi kwenye Muungano wa hiari.

Ukiacha hayo 11 yaliyoondoka, mengine Zanzibar ilibaki nayo kama mwanzo, ikiwa na mamlaka kamili, bila kuingiliwa na yeyote duniani. Tena yaliyobaki Zanzibar, ni mengi kuliko yaliyobaki kwa "Hospitallers" na "Holy See".

Msomaji, rejea ufafanuzi (definition) wa "Sovereignty", rejea pia ulivyotumika kwa "Hospitallers" na "Holy See" kama tulivyoona, ili ujiridhishe mwenyewe kwamba "Sovereignty ya Zanzibar", nayo haikupotea siku ya Muungano. Iliyopotea ni ya Tanganyika.

Kumbe, hata leo, Wazanzibari wakipiga kura ya maoni, kuyaingiza mengine tena kwenye Muungano, lakini wakabaki na suala moja tu la AFYA, bado "Sovereignty ya Zanzibar" itakuwepo tu, kwani tumeona kuwa, AFYA ndilo suala pekee lililobakiza "sovereignty" ya "Hospitallers" toka 1798 hadi leo.

"Encyclopaedia Britannica" inanifundisha hivi: {TREASON, a general term for the crime of attacking the safety of a sovereign state or its head}. Ili kosa la uhaini lifanyike, lazima kwanza iwepo "sovereignty".

Uganda, uhaini hauhesabiki unapomdhuru Kabaka wa Buganda, kwani Buganda inavyojiendesha mambo yake kadhaa, yaani "self-autonomy", haina hata jambo moja lililo na "sovereignty".

"Sovereignty" inaposhambuliwa kutokea nje, tunaita ni uvamizi (invasion), wakati ikishambuliwa kutokea ndani tunaita uhaini (treason).

Gazeti la UHURU, Mei 03, 1971, Toleo la 2081, uk. 01, liliandika hivi: {"Genge la Mahaini 19 Ndani ya Unguja"} na siku saba baadaye, likaandika: {"Wahaini 19 Kula Risasi"}.

Aprili 07, 1972, Thabit Kombo alinusurika kifo alipouawa Rais wa Zanzibar. Alipozinduka, kauli ya kwanza alisema hivi "..mbona leo hivi; au nchi imekwisha pinduliwa?..": {Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha, ISBN: 9976603290, uk. 158, aya ya 04, sentensi ya 06}.

Hivyo, huhitaji kusitasita kutumia neno "uhaini" au "uvamizi" unapotaja jaribio la kuidhuru "Sovereignty ya Zanzibar" kama lililomuua Rais Abeid Karume.

Anayesema kwamba uhaini hauwezi kufanyika Zanzibar akirejea neno "nolle prosequi", muulize, je mzanzibari anayeidhuru "Sovereignty ya Zanzibar", kama haitwi mhaini, tumuiteje? Je, "mtanzania-bara" akifanya kosa hilohilo, ataitwaje?

Atakayesema kwamba Zanzibar haina "Sovereignty", basi atutajie ni lini, taifa la Zanzibar, lilijadili kama Aprili 25, 1964, kisha likautangazia ulimwengu kuwa, limekubali sasa lisiwe na Mamlaka kamili yenye kauli ya mwisho kwa masuala yote liliyobaki nayo mwaka 1964.

Anayechukia Muungano lazima akwamishe juhudi zozote, hata kwa kujifanya mkali, za kubakiza "sovereignty" moja tu nchini.

Kwani, "Encylopedia" inasema hivi: "..union between political units exists only through the sovereign and the exercise of his/her executive power.."{Encylopedia of Government politics, ISBN: 0-425-07224-7, uk. 338, aya ya 01, sentensi ya pili}".

Uhusiano wowote wa "Sovereignty" kadhaa, kama wa EAC, SADC au COMESA, ni ushirikiano tu unaoweza kuuita "Patner-ship", neno la Rais Aboud Jumbe kwenye kitabu chake (ISBN: 9987 8805 5 X).

Sifa kuu ya "Patner-ship" ni mshiriki kukabidhi huko masuala apendavyo, mradi abaki walau na suala moja tu ili asipoteze "Sovereignty" yake.

Historia imetufundisha kwamba, "Sovereignty" zilizoachia suala la ulinzi, ziliitwa "Protectorate". Zilizokabidhi suala la "Uhusiano wa Kimataifa", ziliitwa "vassal state", huku inayokabidhiwa "Uhusiano" ikiitwa "Suzerainty".

Ndivyo tulivyofundishwa hivi: "Suzerainty is kind of international guardianship, since the vassal state is either absolutely or mainly represented internationally by suzerain State" : {Encyclopaedia Britannica, 1964, Vol. 21, uk. 627, sentensi ya pili}.

Hili ndilo tatizo la Muungano wetu. "Sovereignty" mbili ndani ya nchi moja. Kiuchumi, endapo tungetajirika kuliko Japan, tukazimudu hata serikali hamsini, bado lilivyo, lingetusumbua na usomi wetu, si ajabu zaidi ya tulivyosumbuka.

Kumbe, aliyejiapiza kuingia Bunge la Katiba akabakize "Serikali mbili", basi ajue anajitengenezea historia kwa dunia kumshuhudia uelewa wake. Tujenge hamu ya kuiona "research" aliyotuandalia, inavyobakiza "Serikali mbili", huku ikitatua pia tatizo sugu la "sovereignty", inayotakiwa kubaki moja tu nchini.

Vilevile, anayeleta "Serikali tatu", atuthibitishie tutakavyobaki na "sovereignty" moja tu, na si kutuongezea ya tatu kwa ajili ya Tanganyika.

Kikatiba, Rais wa India anapowateua Waziri Mkuu (ib. 75(i)), Gavana wa "State" (ib. 155) na Luteni-Gavana wa "Union Territory" (ib. 239(i)), inaonekana wazi jinsi "Sovereignty" moja tu inavyotenda kazi nchini.

Tungeiiga India, Rais wa Muungano, angekuwa anamteua Kiongozi wa Zanzibar, ambaye angesaini miswada ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Vivyo hivyo pia kwa Tanganyika kama ingekuwepo.

Wolfgang Dourado, AG (Mwanasheria Mkuu) wa zamani wa Zanzibar, aliwahi kupinga Muungano wetu kufananishwa na Northern-Ireland ilivyo ndani ya UK (Uingereza). Alisema kwamba Tanganyika haikuivamia Zanzibar kama Britain ilivyofanya: {Zanzibar And The Union Question, ISBN: 9987697046, uk. 83}.

Siikubali sababu hii, maana sielewi kwa nini Dourado hakuitaja Scotland ambayo haikuvamiwa na England. Lakini vilevile, siwatetei kabisa anaowabishia, yaani wale wanaofananisha. Kwa nini?

Nchini UK, miswada ya Muungano (Britain), Scotland, Wales na Northern-Ireland, husainiwa na "Monarch" ambaye sasa ni Elizabeth II, yaani anaipa "Royal assent". "Royal assent" inafanya hivyo hata kwenye "states" za muungano wa Australia.

Ukifananisha Muungano wetu na ilivyo Northern-Ireland, basi Rais wa Muungano, angekuwa anasaini miswada yote humu nchini, ikiwemo ya Bunge la Muungano, na ile ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Hii ndiyo moja ya tofauti, tena kubwa tu.

Hivyo, "Sovereignty" moja tu nchini kote India, kama inavyotakiwa, inadhihirishwa kwa kudhibiti uteuzi, wakati ile ya UK au ya Australia, inadhihirishwa kwa kudhibiti "legislation" yaani upitishaji wa sheria.

Tukutane wiki ijayo kwa maelezo yatakayogusa pia suala la ZFA na FIFA.

**************
GAZETI: RAIA MWEMA
TOLEO: 339

WIKI iliyopia tuliona maana ya neno sovereignty. Tukaona ukiwa na sovereignty, halafu ukakabidhi masuala yako mengi hadi ukabaki na suala moja tu.

Kama ni nchi bado utaendelea kuitwa sovereign state.

Nilionyesha hospitallers, walivyoendelea kuwa na sovereignty yao toka Juni 12, 1798 hadi leo kwa mtindo huo.

Tumesikia taarifa za kumlaumu Jaji Joseph Warioba kwamba kamsaliti Julius Nyerere kwa rasimu yake kupendekeza serikali tatu.

Kumlaumu hivi ni kunatokana na kutojishughulisha kutafiti alichosema Nyerere kuhusu msimamo wa serikali mbili.

Mwaka 1995, Mwalimu Julius Nyerere aliitangazia dunia kwamba muundo wa serikali mbili unafaa kuendelea kuwa msimamo wa CCM walau hadi Agosti 01, 2004 {Ushahidi: Our leadership and destiny of Tanzania, ISBN: 1-77901-091-5, uk. 04, aya ya 03, sentensi ya kwanza}.

Usomeni huo ni ushahidi mhakikishe kwamba hakusema msimamo huo unatakiwa kudumu milele.

Nimekosolewa kwamba Baraza la Mapinduzi Zanzibar, halikuwahi kuujadili na kuuafiki Mkataba wa Muungano. Hivyo Muungano huu ni batili!

Lakini Thabiti Kombo, anakisimulia kitendo cha Rais Nyerere kwenda Zanzibar Aprili 22, 1964, kusaini Mkataba ule kwa maneno haya: "..Wakati huo sisi katika Baraza la Mapinduzi tulikuwa tumekwisha kuyazungumza masuala hayo (ya Muungano) si mara moja wala si mara mbili. Na tulijua kuwa wananchi wa Zanzibar wanalingojea sana suala hilo (Muungano). Kuja kwa Mwalimu Nyerere (Aprili 22, 1964) kulikuwa kama kugonga muhuri katika maafikiano ambayo yalikuwako toka zamani": (Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha, ISBN: 9976603290, uk. 140, aya ya tatu, sentensi ya pili na ya tatu).

Ukurasa huo, aya ya mwisho, sentensi ya kwanza anasema tena hivi: "Hivyo, tarehe 26 Aprili, 1964, Sheikh Abeid Karume, akifuatana na mawaziri na wajumbe wa Baraza la Mapinduzi walikwenda Dar es Salaam kutia sahihi hati ya Muungano".

Sasa, utasemaje kwamba Baraza la Mapinduzi Zanzibar halikuridhia Mkataba wa Muungano!

Baadhi ya wasioafiki kuwapo kwa Sovereignty ya Zanzibar hutumia Mkataba uliopitishwa mwaka 1933, uitwao Montevideo Convention on Rights and Duties of States ambao hata hivyo ukiusoma wote hakuna popote ambako neno sovereignty limeonekana.

Hata hivyo, Ibara ya kwanza (articles) ya Mkataba wa Montevideo inasema ili mamlaka iitwe state ni lazima iwe na vigezo vifuatavyo: 1: Wakazi wa kudumu, 2: Nchi yenye mipaka 3: Serikali 4: Uwezo wa kuhusiana na states nyingine.

Mataifa mengi tu na hata UN, yanaipuuza hii "Montevideo", kwani, yamefungua ubalozi wa Holy See (Vatcan) wakati Holy See haina zile sifa tatu za kwanza. Yamefungua ubalozi na Hospitallers wakati inakidhi kigezo cha nne tu. Juzijuzi Palestina imepata hadhi kama ya Hospitallers pale UN ikiwa haikidhi kigezo cha pili.

Lakini hata vigezo hivi vingeheshimika duniani, je, kweli Zanzibar haikidhi vigezo vyote vya "Montevideo"?

Wanaoikosoa Zanzibar hutumia kigezo cha nne wakati uhusiano ni hali ya kutokuishi peke yako. Hata Mkataba wa Montevideo wenyewe hauhitaji idadi ya nchi unazotakiwa kuhusiana nazo ili ukidhi kigezo cha uwezo wa mahusiano.

Kumbe, ukiamua kuhusiana na nchi mmoja tu, ukaacha nyingine zote duniani, basi hayo ni moja ya matumizi ya uwezo wako.

Sovereignty ya Zanzibar iliridhika kutumia uwezo huo mahali pamoja moja tu hapa duniani yaani dola ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo, kuridhika huko hakugeuki kuwa kifungo cha kunyimwa sovereignty kwa sababu wengine duniani wameamua kuutumia uwezo ule kwa nchi au marafiki wengi.

Hivyo, vigezo vya Montevideo, unaweza kuvitumia kumuelimisha anayeviabudu jinsi vilivyo dhaifu.

Msomaji mmoja wa ile makala yangu, alisema ni mwanasheria, aliniuliza hivi, "Jose, je, ulishawahi kuona popote maneno yasemayo "Tanzania is one state and is sovereign United Republic"?.

Ndugu msomaji, kamwe hugeuki kuwa tumbili kwa sababu tu kuna mkataba umeusaini ambao sentensi ya kwanza inasema kwamba "Kuanzia leo wewe umeacha kuwa binadamu na umekuwa tumbili"! Tunachozingatia ni vigezo.

Nguvu ya vigezo ndiyo iliyofanya Pluto iachwe kuitwa sayari, japo wengi mnaosoma makala hii huenda mlifaulu mtihani au mkapewa zawadi, au mkapandishwa vyeo kwa kuandika kwamba Pluto ni sayari ya tisa katika mfumo wa jua.

Si, katika suala la sovereignty tu, bali katika jambo lolote duniani, nguvu ya vigezo, inajitegemea, wala haihitaji msaada au utetezi wa sentensi za ziada.

Niliombwa pia kutoa mfano wa sovereignty ya Marekani. Katiba ya Marekani haina neno sovereignty.

Marekebisho ya 10 ya Katiba yanampa Gavana wa Jimbo mamlaka ambayo Rais wa Muungano hajapewa na wala Gavana hajakatazwa.

Mwaka 1962, George Wallace aligombea ugavana wa Jimbo au State la Alabama. Kilichomfanya ashinde uchaguzi huo ni sera yake kwamba atahakikisha Wamarekani weusi hawaruhusiwi kusoma kwenye vyuo vikuu vya Alabama. Sera ikashinda uchaguzi, akawa gavana wa Alabama.

June 11, 1963 ukaja usajili wa wanafunzi Chuo Kikuu cha Alabama. Mapema asubuhi, akasimama mlangoni pale chuoni na kwenye aya ya tisa ya hotuba yake alisema, "ninasimama hapa kama Gavana wa Sovereign State ya Alabama na sikubali mamlaka yangu kuingiliwa kimabavu na Serikali ya Muungano ya Marekani (Alabama Department of Archives and History, Governor George C. Wallace's School House Door Speech ).

Walipokuja wanafunzi wawili Weusi, Vivian Malone and James Hood, akawazuia yeye binafsi ili wasisajiliwe.

Rais wa Muungano, John F. Kennedy, akataarifiwa dakika ileile, na yeye palepale, akatoa amri, kwa majeshi yake yaitwayo Alabama National Guard kumfukuza Gavana Wallace pale chuoni.

Ndipo Gavana akasalimu amri, akaondoka akilalamika, huku James na Vivian wakiruhusiwa kujisajili wakilindwa na majeshi hayo ya Muungano.

Rais Kennedy, akawa ameithibitishia dunia kwamba, nchini Marekani kuna sovereign moja tu, nayo ni Serikali ya Muungano, wala si Serikali ya Jimbo (State).

Kulalamika kama Gavana Wallace wakati anafukuzwa pale chuoni ni sifa mojawapo ya kukosa sovereignty ya popote duniani. Mwenye sovereignty halalamiki, anatenda bila hofu.

Hapa nchini kukoje? Wiki jana nilieleza kwa kina hali ya sovereignty mbili zilizopo tangu siku ya Muungano.

Kitendo cha sasa kufikisha miezi 41 tangu Zanzibar kupitisha bila hofu Katiba yao, kinaweza kuishia kulalamikiwa na mtu au mamlaka yoyote hapa duniani, maadam mlalamikaji hana sovereignty ya jambo lile.

Sasa tuone sovereignty ya Zanzibar tuihusishe na FIFA. Kwanza si kweli kwamba sovereignty ndicho kigezo pekee cha kuwa mwanachama wa FIFA.

Taiwan iko FIFA, inatengwa na historia ya mahusiano yake mabovu na China, maana nako unaweza kuiita Taiwan kwa jina la "China-visiwani" na ile China tuijuayo wengi ikaitwa "China-bara". Bado kuna ugomvi wa miaka mingi wa sovereignty kati ya hizi "China-bara" na "China-visiwani".

Chechnya ni sehemu ya Russia lakini hata nako kuna ugomvi wa sovereignty ambapo lipo kundi linaitwa separatists wanataka utata huo uondoke iwe na sovereignty yake.

Macao ni mwanachama wa FIFA japo ilikuwa mkoa wa Ureno. Umbali wake baharini kutoka Ureno uliifanya ikubaliwe kuwa timu inayojitegemea. Lakini hata ilipobadili kuingia kwenye sovereignty ya China bado inaendelea kujitegemea pale FIFA.

Yafuatayo ni majimbo au mikoa ya nchi, ambazo ni wanachama wa FIFA lakini wako kwenye sovereignty moja yaani nchi moja na zilizomo kwenye mabano: Guadeloupe (France), American Samoa (US), New Caledonia (US), Martinique (France).

Montserrat nayo ina uanachama wa FIFA kama Waingereza wenzao yaani Wales, Scotland, Northen-Ireland na England, lakini yenyewe kwa kigezo hiki cha umbali.

Hivyo, utaona kwamba FIFA inaruhusu sababu kadhaa kwa baadhi ya timu, ambazo baadhi ni mikoa tu ya nchi-mama kuwa wanachama wake sambamba na nchi-mama.

Moja ya sababu niionayo ni historia na nchi nchi-mama kama wale wanne wa UK. Sababu ya pili umbali kutoka nchi-mama. Kwa sababu kwa umbali huo mikoa ile haiwezi kushiriki ligi ya nchi mama na hivyo FIFA ikiwanyima uanachama kwa kigezo cha sovereignty ya nchi-mama basi hakika itakuwa imewatenga na ulimwengu wa mpira.

Sababu ya tatu ni tofauti kubwa sana ya utamaduni kati ya eneo na nchi-mama. Na sababu ya nne ni hii mizozo ya sovereignty ambayo ni wazi huziweka mbali na hata mahusiano ya kawaida ya wananchi.

Tumeziona sababu za mikoa mingi kuruhiswa uanachama FIFA sambamba na nchi-mama, tena mingine haina utata wowote wa sovereignty.

Watanzania tujipime, Zanzibar au ZFA ambayo nasikia iliwahi kuomba FIFA uanachama, inaangukia wapi katika sababu zile?

Kujibu swali hili ni lazima kujiuliza, je, Zanzibar tunaungana au kutenganishwa na nini katika mpira? Tuliona wiki jana kwamba siku ya Muungano yaliingia masuala 11 tu kwenye Serikali au Bunge la Muungano.

Suala la michezo halikuingizwa. Hivyo, michezo pia, ni moja ya mambo tele yanaounda ile sovereignty ya Zanzibar".

Hapa tunajijibu lile swali kwamba, kimichezo, Tanzania-bara tunatengwa na "Sovereignty ya Zanzibar". Sababu hizi sizipofafanuliwa kiuhalisia kule FIFA, basi Zanzibar nayo itaendelea kutengwa kabisa kisoka duniani wakati tumeona kuna mikoa duniani inashiriki FIFA.

Sijui kule ZFA ilipokataliwa uanachama kule FIFA vilipelekwa vielelezo gani vilivyoshindwa kuthibitisha sovereignty ya Zanzibar", kana kwamba hakuna vielelezo hivyo!

Nina shaka na ile nia ya kujiunga FIFA niliposoma rasimu hii ya katiba. New South Wales au jimbo lolote ndani ya muungano (Commonwealth) wa Australia haiwezi kushiriki FIFA kwani katiba ya Australia ina ibara ya 109 inayosema kuwa sheria yoyote kwenye jimbo lolote ikikiuka katiba ya Muungano, basi sheria hiyo itajirekebisha kulingana na ya Muungano.

Vifungu kama hivi huitwa supremacy clause na inabidi viangaliwe kwa umakini popote penye ugomvi wa sovereignty. Lazima tujiulize, je, sovereignty zinaweza kuendelea kuwa zaidi ya moja iwapo kifungu kama hiki kimeingizwa kwenye katiba iliyopitishwa kwa kura ya maoni.

Sasa kifungu hiki ninakiona kwenye ibara ya 8(2) ya rasimu hii. Ni bora kupata mwafaka hapa kujua tafsiri yake ipimwe na nia ya kutaka kuondoa au kutoondoa utata wa sovereignty zilizopo.

Na kama jibu litatoka kwamba ibara hii inaondoa utata wa sovereignty na sasa tutabaki na sovereignty baada ya kura ya maoni, basi wenye kutaka Zanzibar iingie FIFA waistarajie mteremko kwa hili.

Urahisi kuelekea FIFA utakuwa uko zaidi kwenye katiba ya sasa lakini si katiba inayokuja ikipita na kifungu hiki.

Kuna wanaolijua vizuri tukio la kuimba nyimbo za taifa majuzi kwenye mashindano ya Kombe la Kagame ambako timu za Tanzania-Bara na Zanzibar hushiriki.

Sikulishuhudia lakini ni wazi kwamba timu kama Zanzibar hazikupata taabu kuimba Wimbo wa Taifa. Je, kama tutaendelea hivi na serikali mbili bila kutatua sovereignty, timu ya Kili Stars (Tanzania-Bara) itaimba vipi?

Sijasikia Tanzania-Bara wakiruhusiwa kuima maneno "..Mungu ibariki Tanzania-Bara.." ambayo ukifika kile pale tusemapo "..wabariki viongozi wake.." kutakuwepo na utata kwani hakuna viongozi wa "Tanzania-Bara".

***************
 
MTOA HOJA ACHA KUHANGAIKA, NJE YA MUUNGANO HAKUNA ZANZIBAR KUNA WAO WAPEMBA NA WAO WAUNGUJA USIPOTOSHE MCHANA KWEUPE NAONA UNAMKAKATI WA KUUNDA JAMHURI YA UNGUJA NA JAMHURI YA PEMBA, huna jipya NYIE NDO WAPINGA MUUNGANO MAADUI WA WATANZANIA.
 
Mkuu umenena kweli

USIKUBALI KUBURUZWA NJE YA MUUNGANO HAKUNA ZANZIBAR KUNA WAO WAPEMBA NA WAO WAUNGUJA USIPOTOSHE MCHANA KWEUPE NAONA UNAMKAKATI WA KUUNDA JAMHURI YA UNGUJA NA JAMHURI YA PEMBA, huna jipya NYIE NDO WAPINGA MUUNGANO MAADUI WA WATANZANIA.
 
Upeo wako wa akili wa kufikiri umefikia hapo kwa kupenda kucopy mawazo ya watu na kuja kuyaweka humu ndani huku ukidhani kuwa wao ni kama Miungu watu kana kwamba wanachoandika wao basi ukweli, hahaha acha kupotosha watu kuhusu muungano.������
 
Vipofu waliojiunga na mitandao hata mwezi haujapita ndiyo wanaosababisha ziwepo sheria za kufunga mitandao. Mjadala huu tuliumaliza mwaka jana.

Jay Milionea
Join Date : 19th April 2015
Posts : 117
Rep Power : 325
Likes Received
6
Likes Given
8
Unajaza saver ya JF duu huyu sijui kwao wapi?
Mwakaboko King
Join Date : 22nd April 2015
Posts : 83
Rep Power : 318
Likes Received
6
Likes Given
3
 
Vipofu waliojiunga na mitandao hata mwezi haujapita ndiyo wanaosababisha ziwepo sheria za kufunga mitandao. Mjadala huu tuliumaliza mwaka jana.

Jay Milionea
Join Date : 19th April 2015
Posts : 117
Rep Power : 325
Likes Received
6
Likes Given
8

Mwakaboko King
Join Date : 22nd April 2015
Posts : 83
Rep Power : 318
Likes Received
6
Likes Given
3

Wewe umetumwa sio bure kwa na jicho lako 1 linaloona ukungu,unajifanya kucopy and paste details ili zikusaidie nini?acha uoga!!! Afu topic kama imefungwa unafuata nini hapa?au imekuuma sana baada ya kuona uongo wenu umefikia mwisho?kwa kuendelea kudandia mada utaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu
 
SIDANGANYIKI2015
Join Date : 19th April 2015
Posts : 68
Rep Power : 316
Likes Received
3
Likes Given
0
 
SIDANGANYIKI2015
Join Date : 19th April 2015
Posts : 68
Rep Power : 316
Likes Received
3
Likes Given
0
Huko ndo kuishiwa hoja na kuanza kuangalia joining date za watu, kwani alokwambia kwamba kutangulia ndo kufika nani? Ndo nyie mliokuwa mkikariri darasani na mkafeli mwisho wa siku, suala muhimu hapo ni kujua kutema hoja nzuri zenye IQ kubwa, sasa wewe unaonekana huna kitu kichwani zaidi ya kufatilia who joined nad when? Utaishia hivyo hivyo pole sana profiles za watu hazitakusaidia kitu hata cku moja, acha kupoteza muda, muda huo bora ungeutumia kuisoma hiyo katiba ili ujue mambo mazuri yaliyopo ndani ama weka hoja za maana na sio hiyo kazi unayoifanya hapo.
 
Vipofu waliojiunga na mitandao hata mwezi haujapita ndiyo wanaosababisha ziwepo sheria za kufunga mitandao. Mjadala huu tuliumaliza mwaka jana.

Jay Milionea
Join Date : 19th April 2015
Posts : 117
Rep Power : 325
Likes Received
6
Likes Given
8

Mwakaboko King
Join Date : 22nd April 2015
Posts : 83
Rep Power : 318
Likes Received
6
Likes Given
3
Endelea kujadili profile za watu afu tuone mwisho wa siku utafaidika nini? Hapa unapewa dozi tuuu kama umeishiwa hoja lala
 
SIDANGANYIKI2015
Join Date : 19th April 2015
Posts : 68
Rep Power : 316
Likes Received
3
Likes Given
0

Pole, umedanganywa na nani mpaka unaitwa Mdanganywa. Why do you like to be called Psychological name? hii ni shiiiiiiiiiiiiiiiiiiida!
 
SIDANGANYIKI2015
Join Date : 19th April 2015
Posts : 68
Rep Power : 316
Likes Received
3
Likes Given
0

Muungano haujawahi kuwepo!!!!!!!! na wewe dotcom unashadadia jambo usilolijua na post zako njaaa,kazi ku-like post za watu wengine bora uhamie forum nyingine!ndo maana toka 2009 una post 88 hii inaonyesha uwezo wako mdogo wa kupambanua mambo umri wako haulingani na mchango wako wewe umedumaaa ha ha ha ha tokaaaaaa!!!
 
Hahahahahaaha nimeipenda hiyo asee, ni kweli maana kuna watu humu ndani akili ndani hakuna ndo wanapost ujinga tuuu kutwa.
 
Back
Top Bottom