Shabdullah
Member
- Feb 17, 2020
- 65
- 52
Habari zenu wana JamiiForums,
Kama tunavojua leo ni siku ya maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanzania.
Muungano huu unajumuisha pande mbili ambazo ni Zanzibar na Tanganyika.
Vijana wengi sasa hivi wanaelewa kuwa muungano huu ni wa zanzibar na tanzania bara na kulisahau jina la Tanganyika.
Hali hio imetokana na upande mmoja wa muungano kutaka kupoteza historia ya jina tanganyika na kulizamisha kwenye Tanzania kitu ambacho kinapotoa na kinabadilisha maana halisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pande zote mbili za muungano zina malalamiko mbali mbali zinazoelezea changamoto hizi.
Changamoto moja kubwa ni ile ya muundo wa muungano huu. Kuna mawazo tofauti kwa raia wa Kitanzania
Wapo wanaotaka muungano huu utengeneze serikali moja yani iwe tanzania tu kusiwe na zanzibar wala Tanzania bara (Tanganyika)
Pia wapo wanaotaka ziwe serikali mbili ambazo ni kama hizi za sasa ikiwa inaitambua serikali ya zanzibar na Serikali ya Muungano ambayo inaondoa serikali ya Tanzania bara (Tanganyika)
Na wapo ambao wanataka ziwe serikali tatu ambayo ni serikali ya zanzibar na serikali ya tanzania bara (tanganyika) na iwepo na serikali ya muungano wa tanzania ambayo serikali hii inakuja kusimamia mambo ambayo yanahusu muungano tu.
Wazanzibari wengi waliopo hivi sasa, hawapendi kuusikia hata harufu yake jinsi unavyo endeshwa hadi kufikia leo MIAKA 56 kwasababu ya muundo wa Muungano huu.
Watanzania bara (watanganyika) wengi hawaelewi juu ya muungano huu na kuona kuwa kwanini zanzibar inatajika sana kuliko tanganyika au tanzania bara huku wakisahau kuwa Tanganyika imezama ndani ya "Tanzania" na kuzaliwa jina "Tanganyika".
Wengi wanaona kwanini Zanzibar inapata jina zaidi kuliko Tanzania bara wakisahau kuwa mpini wa Zanzibar umeshikiliwa na Tanzania bara kutokana na muundo wa serikali uliopo.
Wewe kama Mtanzania aidha ni Mtanzania bara au mzanzibari unaelewa nini kuhusu muungano huu?
Na unaona faida gani?
Na kuna changamoto gani unazoziona au kuzifikiria juu ya muungano huu?
Sent using Jamii Forums mobile app