Muungano siyo utengano

Joined
Feb 7, 2013
Posts
16
Reaction score
5
MUHUNGANO SIYO UTENGANO


Siyo siri pamoja na kuwapo kwa tafsiri na aina tofati ya miungano duniani kote miungano yote yenye mafanikio ni ile iliyoweza kuzaliwa na kukua kupitia tafsiri na falsafa sahihi ya muungano yaana kuacha kujitegemea au kuwa pekee na kuwa pamoja au kitu kimoja, hii huambatana na kuachana na matakwa, nia au fikra za kinafsi. Ni kweli kwamba kumekuwa na miundo mbalimbaliya miungano lakini katika miundo hiyo mamlaka kuu imebaki kuwa moja. Zipo dola kubwa na ndogo zilizofanikiwa katika hili pamoja na uwepo wa changamoto za kawaida. Mataifa mengi yakiwemo Urusi, Marekani, Canada, Australia, Ujerumani, Ufaransa, Uispaniora,Uingereza,Vietnam, malasyia, Ukraine, Bulugaria, China, India, Serbia, Manchuria na mengine yamekuwa mifano mizuri ya miungano duniani. Hata hivyo hofu ,mashaka, ubinafsi na kutokuhaminiana vimekuwa adui wakubwa wa miungano mingi duniani, mfano wa miungano ilioweweseka kutokana na sababu hizo ni pamoja na ule wa Moldova na Romania, Romania na Transylvania na mingine mingi. Kwa Africa muungano wa Senegali na Gambia kuzaa Senegambia kati ya Januari 1, 1982 hadi September 30 ,1989 ulivunjika hasa kutokana na kutokuaminiana na hisia za kibinafsi. Muungano wa Tanganyika na zanzibari uliothibitishwa april 26,1964 ,baada ya mkataba wa muungano kutiwa saini april 22, 1964, kuputia sheria ya muungano namba 61 ya mwaka 1964 ulizaa taifa moja liloitwa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania tangu Octoba 20, 1964. Hata hivyo Muungano huu una historia pana na umepita katika changamoto nyingi. Moja ya chagamoto kubwa ni mjadala uliodumu kwa mda mrefu na uliopamba moto hasa baada mchakato wa mabadiliko ya katiba kuanza tangu mwaka jana juu ya swala la muundo wa muuungano. Wapo wanaoona serikali mbili ndiyo suruhu na wengine tatu na hata wengine kuwa na mawazo tofauti kabisa na hayo. Muundo wowote wa muungano uliojikita katika maslihi binfsi ya kisiasa ama madaraka hauna mwelekeo mwema na hivyo hauna faida kwa wananchi kwani umejaa matamanio binafsi na unafiki. Muundo wa muungano wa serikali zaidi ya moja na viongozi wakuu zaidi ya mmoja ni dalili za hofu, kutokuaminia, ubinafsi na unafiki uliobebwa na maslahi ya kisiasa zaidi kuliko maendeleo ya wananchi. Na hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi huendelea kutazama maslahi mapana binafsi na hisia za kujitegemea katika maswala ya kimipango, usimamizi na utekelezaji wa maswala mbalimbali. Kuna matokeo mengi hatari ya serikali zaidi ya moja katika taifa moja mbali na migongano ya marakwamara ya kiitifaki, kimadaraka,kimamlaka na kimaslahi; swala la gharama hasa katika nchi maskini kama yetu si la kufanyiwa janjajanja, na hii inatokana na ukweli kwamba gharama hazitoishia tu kuendesha serikali bali kulea rundo la viongozi wakuuu wastaafu baada ya miaka kadhaa na hili si swala dogo. Ukiachana na hilo changamoto ya demokrasia ya mfumo vyama vingi si swala la kutazamwa juujuu.Tujaribu kufikiri vipi ikitokea serikali hizi tatu zikaendeshwa na vyama vyenye ilani,sera, itikadi na misimamo tofauti ambovyo tumekuwa tukivishuhudia kutokuhaminiana na kurumbana kwa mambo ya kawaida, vipi kila moja kwa chama ckake na serikali yake. Tusijaribu ‘kuyatikisa' maisha ya watanzania. Sababu zinazosemwa na wengi kuhalalisha ‘kutokuwezekana' kwa muundo wa serikali moja ni pamoja na madai kuwa "wenzetu hawatakubali", "hile ni nchi kamili, ina historia na utamaduni wake". swali la msingi la kujiuliza ni hipi nchi isiyo na sifa hizo? na je nini haja ya muungano kama hizo sababu ni muhimu zaidi?. Kama kuna kingine tuambiwe. Muungano siyo utengano . Nchi zilizoungana na kuwa na serikali kuu moja na kiongozi mkuu mmoja zimekuwa na utulivu kimamlaka,kiutendaji, na zinapiga hatua kubwa kimaendeleo,pamoja na kuwa kabla ya kuungana zilikuwa na tofauti kubwa za kihistoria, kidini, kilugha,kijamii na kiutamaduni. Miongoni mwa faida muhimu za serikali moja katika taifa ni pamoja na; kurahisisha mgawanyo wa madaraka,mamlaka,rasilimali utendaji na shughuli zote za kimaendeleo, kuondoa tofauti mbalimbali, hofu, na kutokuaminiana, kujenga, kukuza na kudumisha umoja na utamaduni imara, kuwa na nia na matarajio thabiti yanayofanana kutokana na sera na ajenda za kitaifa zilizozaliwa na serikali moja, kupunguza gharama za kuhudu serikali na hivyo kutumia fedha nyingi kwa wananchi, huduma za kijamii, miundombinu na maendeleo kwa ujumla,kukuza usawa, makubaliano thabiti, utaifa ama uzalendo na kujenga dola imara. Viongozi, wanataaluma mbalimbali na watanzania wote,tuchague kuishi pamoja, tuchague kuishi kwa upendo, tuyathamini maisha yetu na ya vizazi vyetu kuliko matakwa ya mda mfupi ya wanasiasa waroho; na haya ndio matarijio ya watanzania tuliowengi, kwani tunaipenda nchi yetu. Kwa kufanya maamuzi sahihi tutakiokoa kizazi kilichopo na vingi vijavyo baada yetu. Katika kitabu chake , kiitwacho TUJISAHIHISHE, (May 1962) baba wa taifa hayati Julius.K. Nyerere aliandika ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayotabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Emanuel Gabriel Someke 0753191035
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…