Muungano uliopo sasa sio ule tulioachiwa na waasisi wa Muungano

Muungano uliopo sasa sio ule tulioachiwa na waasisi wa Muungano

George J Minja

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
289
Reaction score
203
Wadau wengi wanabishana kuhusu serikali mbili au tatu au hata wengine kwenda mbali na kutaka serikali moja hii ni mitazamo ambayo kwangu sioni kama ni tatizo watu kutaka nchi yao iweje kwa mapenzi yao japo wale wa Lumumba inaonekana sio mapenzi yao binafsi ila ni mapenzi ya wakuu wao wanapokea kumeza na kuanza kusema wasiyoyaelewa.

Naona tatizo kubwa kwa wale wanaosema tuendelee hivi tulivyo bila kuelewa hivi tulivyo sio aina ya Muungano tulioachiwa.

Sasa hivi tuna NCHI MBILI NA SERIKALI MBILI sio Muungano huu,swala hapa sio serikali whether mbili au sita tatizo ni nchi mbili jambo ambalo hatuwezi kuendelea nalo.Zanzibar ni nchi na wazanzibari hawako tayari hata kidogo kubadili hilo.

Kwa Hali ilivyo sasa SERIKALI TATU haziepukiki,tukiendelea na Serikali mbili na Nchi mbili kama tulivyo sasa miaka michache ijayo Muungano huu utavunjika kero zake hazitatuliki hasa Katiba ya Zanzibar.
 
Jaji jana ametoa majibu ya kwa nn serikali tatu!

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamie
 
magamba kazi wanayo maana makejeli sn swala serikali tatu bila kusoma alama za nyakati.
 
Back
Top Bottom