Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
Tuweni wakweli sababu hasa ya Zitto Kabwe kutaka hasa muungano wa vyama vya upinzani ni kwa kuwa muungano huo utawafaidisha zaidi ACT na siyo kwamba ana nia ya dhati kuona upinzani ukifanya vizuri.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 pamoja na kwamba vyama vya upinzani viliungana na kusimamisha mgombea mmoja lakini ACT Wazalendo walisimamisha mgombea wao peke yao Mh. Anna Mghwila.
ACT inakubalika kidogo mno Tanzania Bara, ila upande wa Zanzibar ina nafasi nzuri kwa influence ya Maalim Seif. Kwa mfano mkoa wa Kigoma CHADEMA ina ushawishi kuliko ACT japo ACT ndiyo mkoa wanaoutegemea. ACT kwa Bara inakubalika kidogo mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, hata hivyo ukubalikaji huo siyo wa kiasi kile kiasi kwamba kama CHADEMA ikisimamisha wagombea kwenye majimbo husika basi ACT haiwezi kupata wabunge katika mikoa hiyo.
Kiujumla kwa upande wa bara ACT Wazalendo bila kuachiwa majimbo na CHADEMA inaweza kupata jimbo moja tu la Zitto Kabwe peke yake.
Hivyo basi katika muungano wa CHADEMA na ACT, CHADEMA haitabenefit sana kwani maeneo ambayo CHADEMA ina nguvu kama DSM, Arusha, Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Mara nk ACT haina nguvu yoyote ile. Ila katika maeneo yote ACT inayokubalika ukiondoa Zanzibar CHADEMA pia ina nguvu na pengine zaidi ya ACT mfano Kigoma.
Zitto Kabwe anajua tayari Zanzibar chama chake kina ushawishi, hivyo anahitaji angalau apate majimbo mawili matatu kwa kupitia mgongo wa ushirikiano na CHADEMA ili wamuongezee viti maalumu. Hii ndiyo sababu ya kulilia zaidi muungano wa vyama.
Kinachofanyika sasa ni Zitto Kabwe kuiblackmail CHADEMA kwa kumchukua Membe anajua CHADEMA itaogopa Membe kugombea ACT kwa hofu ya kugawa kura. Hivyo anajua kwa vyovyote vile CHADEMA itamtafuta Zitto Kabwe ili washirikiane kuepuka Membe kugawa kura za Urais.