josias
Member
- Jan 7, 2014
- 47
- 34
Nina sikitishwa na baadhi ya mawazo ya baadhi ya watu wanao jiita wana harakati na wasomi katika nchi hii, ni suala la ajabu sana kwa mtu mwenye uelewa mzuri kutetea uwepo wa serikali mbili au tatu.Nina penda kuuliza, endapo kila nchi zilizofanya muungano duniani zingekua na serikali kulingana na idadi ya majimbo au nchi zilizo ungana ingekuaje? Chukulia mfano rahisi wa nchi ya Marekani ambayo ni muunganiko wa serikali za majimbo(nchi) 52 zingekua na rais kutoka kila jimbo ingekuaje? Itakua kazi ngumu sana kuchukua maamuzi kwa nchi yenye muundo wa serikali 3 kwani kutakua na uhitaji wa kuzishawishi serikali shirika ili kufikia uamzi wa pamoja.
Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ingechukua maamzi mazito ya kubain udhaifu wa muungano uliopo kisha wakafanya maboresho ya muungano huu kwa kuondoa serikali ya Tanzania bara na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kisha kukawa na serikali moja ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania(Re-birth of the union) make sidhani kuwa misingi aliyoiacha muasisi wa muungano hayahitaji maboresho.
Kama muungano utashindwa kuwa wa serikali 1 basi zanzibar iachwe iwe nchi huru yenye serikali yake na bara kuwe na serikali yake huru yanye mamraka yake.