Muungano wa Sovieti na kuibiwa kwa ndege vita aina ya Mikoyan-Gurevich MiG 25.

Muungano wa Sovieti na kuibiwa kwa ndege vita aina ya Mikoyan-Gurevich MiG 25.

Raphael focus

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2018
Posts
779
Reaction score
4,564
Habari ya muda huu wanajanvi.
Kama mada inavyo jieleza hapo juu , ni kisa kinacho muzungumzia rubani wa ndege vita ya Usovieti aliye iba ndege hiyo na kuitoloshea nchini Japan. Ungana nami Alseneta sir.


Munamo tarehe 6 mwezi septemba mwaka 1976 , ndege kilionekana ghafla kutoka kwenye mawingu kalibu na mji wa Hakodate katika kisiwa cha Hokaido kasikazini mwa Japan.



View attachment 1125157










Ilikuwa ndege yenye injini mbili lakini haikuwa ndege ya kawaida ambayo watu wa Hakodate walikuwa wamezoea kuiona.

Ndege hiyo kubwa iliyokuwa na alama za muungano wa Usovieti haikuwa imeonekana eneo hilo
apo kabla.
Ilituwa katika uwanja wa Hakodate. Kutokana barabara ya uwanja huo ilikuwa fupi hali iliyo ilazimu ndege hiyo kuchimbua aridhi na kusimama mwisho kabisa mwa uwanja wa ndege.

Rubani akachomoza kutoka chumba cha rubani na kufyatua risasi mara mbili hewani kutoka kwa bastola yake.
Dakika chache baadaye maafisa wa uwanja wa ndege wakamkalibia .Huu ndiyo wakati rubani mwenye umri wa miaka 29
Luten Viktor Belenko wa jeshi la wana hewa wa Usovieti alitangaza kuwa alitaka kuhama nchini yake.


Ndege hiyo aina ya Mikoyan-Gurevich- MiG 25 ndiyo ndege yenye usiri zaidi kuwai kuundwa na muungano wa Usovieti.

Viktor Belenko, alikuwa raia wa Usovieti aliye zaliwa mara baada ya vita vya pili vya dunia eneo la milima ya Caucasus.
Alijiunga na jeshi na kufuzu kama rubani wa ndege za kivita cheo ambacho kilikuwa na hadhi ya juu kuliko cha mwananchi wa kawaida.

Akiwa baba wa mtoto mmoja wakati huo na akikabiliwa na talaka, pia alikuwa na maswali mengi kuhusu jamii ya Usovieti.
Belenko alifahamu kuwa ndege kubwa ya kijeshi ambayo aliitumia katika mafunzo ndo ingekuwa njia rahisi ya kumuwezesha kukimbia.

Akiwa katika kambi ya jeshi la hewa ya Chuguyevka kalibu na mji wa Vladivostok, mashariki mwa Usovieti. Japan ilikuwa umbali wa kilometa 644 . Ndege hiyo uku ikiwa na injini kubwa inamaana haingeruka mbali sana hadi kutua katika kambi ya Marekani.

Tarehe 6 mwezi septemba, 1976 Belenko aliondoka na marubani wenzake kufanya mazoezi.
Maramoja akatafuta njia ya kupita kwa sababu ndege yake ilikuwa na mafuta ya kutosha.
Alilusha ndege angani na dakika chache baadaye alikuwa safarini kuelekea nchini Japan.

Ilikukwepa mitambo ya rada ya Usovieti na ile ya Japan, Belenko aliruka chini kima cha futi 100.
Lakini alipoingia anga ya Japan alipanda hadi futi 20,000 ili aweze kuonekana kwa rada za Japan. Mda mchache baadae wakati ndege za japani zikiwa tayari kumfwatiria; Belenko alitoweka na kuingia ndani ya mawingu na kutoweka kwa rada za Japan.
Belenko alikuwa na nia ya kuluka hadi uwanja wa Chitose lakini ndege yake ilikuwa imeishiwa na mafuta , hivyo kupelekea kutua uwanja wa kalibu wa Hakodate.
Ghafla Japan wakajikuta wakiwa na rubani aliye hama na ndege ya kivita ambayo imekuwa ikikwepa
mashirika ya ujasusi ya nchi za Magharibi.

Uwanja wa ndege wa Hakodate toka wakati huo ukawa wenye shughuli nyingi za ujasusi jambo
ambalo hata shirika la ujasusi la Marekani ,CIA halikuwamini.

Hitimisho;
Belenko hakuludi USSR wala ndege yake hiyo. Alieuhusiwa kuhamia nchini Marekani baada
ya kupewa uraia na Raisi Jimmy Carter ambapo alipewa cheo cha mhandisi wa ndege pamoja na mshauri wa jeshi la Marekani.
Kitambulisho na yale yote aliyo yaandika wakati akiwa safarini kuelekea nchini Japan yapo kwenye makavazi, maonyesho ya CIA mjini Washington DC.



By Alseneta sir.
 
Umefanya nimkumbuke Robert mbona huyu mzee ndio alikuwa mtu wa kwanza Africa kuweza kuificha Mig -21 isionekane kwenye radar mwaka 79 times za kagera war
 
Umefanya nimkumbuke Robert mbona huyu mzee ndio alikuwa mtu wa kwanza Africa kuweza kuificha Mig -21 isionekane kwenye radar mwaka 79 times za kagera war


Hujampa heshima yake yote mkuu


Ni retired full general Robert Mboma, mkuu wa majeshi ya Ulinzi mstaafu na katika historia mkuu wa majeshi pekee kutoka nje ya kamandi ya vikosi vya nchi kavu
 
Nimejaribu ku goggle Victor Belenko nikasoma taarifa zake na list ya watu walio defect au kukimbia nchi zao.
Nikagundua kuwa wote walitoka nchi za eastern bloc au nchi za ukomunist enzi za vita baridi na nchi za magharibi kama Marekani.
Nimejiuliza kwanini? nchi za kikomunist wakati huo zilikuwa zinaendeshwa kidikteta hakuna uhuru wa kutoa mawazo.Wananchi wake walikuwa wanaishi katika ufukara mkubwa ndio maana wanaopata kanafasi hawakaachii.
Hata leo hii angalia wananchi wa Korea kaskazini wako na maisha magumu sana dhidi ya wenzao wa Korea kusini.
Infact with exception of China na Urusi bado zinaitwa communist countries lakini zimeendelea sana sababu wamerefine ucommunist wao wamekubali hata makampuni makubwa kuwekeza kwao
 
Hujampa heshima yake yote mkuu


Ni retired full general Robert Mboma, mkuu wa majeshi ya Ulinzi mstaafu na katika historia mkuu wa majeshi pekee kutoka nje ya kamandi ya vikosi vya nchi kavu
Leta story yake boss.
 
Leta story yake boss.
Wakati wa vita vya Kagera alikuwa na cheo cha Major na ndio alikuwa mkuu wa jeshi la anga.Kwa ujumla vita vya Kagera watanzania tulikuwa wajanja haturushi ndege zetu hovyo hovyo kama mjinga mjinga Idi Amini maana jet fighter ni ghali sana.
Ila sisi tulikuwa na taaluma ya hali ya juu ya kutungua ndege za adui.Huyu mzee shujaa Mboma alikwenda kuipiga bank ya Libya iliyokuwa Jinja kwa shabaha sahihi akarudi salama na ndege yake mpaka waganda wakasema haindeshwi na mtanzania bali mcuba.
Ndege za Uganda zilizotunguliwa na Tanzania ni zaidi ya 20.Mzee wetu huyu bado yupo mungu amjalie afya njema.
 
Back
Top Bottom