Nadhani unachuki binafasi na Mwakyembe mkuu. Otherwise, it looks like you must be experiencing some serious pyschological problems; and I strongly suggest that you find some good professional counseling before things get even worse.

i dont like this ... please be kind to consider what you to say to others prior to posting anything .. and imagine how you would feel if someone sent you the same ... we are grown ups and we have other people reading what we write ... how sad to read that we take most things very personal and degrade each other for other peoples dhambis ... we keep the solidarity, respect and love as our aim is to fight against the mchwas eating our country
 
Hebu tuonyeshe uongo wa Mwakyembe uko wapi Harafu Mwiba usipapukie mambo kwa jaziba Mwakyembe kaeleza ukweli kuwa waziri mkuu alitoa maelezo kwa mujibu wa katiba inavyosema lakini akina Shamuhuna wenye uelewa finyu kama wako wakaifanya ni issue binafsi ya pinda. Halafu unapo fananisha jambo la ufisadi wa Lowasa na Issue ya Pinda unaonekana wewe ni wa ajabu huelewi kuchambua mambo kuhusu ufisadi wa Lowasa kamati ya bunge ilieleza kile kilichochunguzwa na kikaonekana, ndugu yako lowasa aliambiwa ayapime na aseme yeye anavyo elewa lakini kwakuw ukweli nunauma akawa na jaziba na hasira zilizo mfanya asielewe kilicho elezwa na kamati kama wewe ambavyo jaziba yako na chuki binafsi imekufanya usimwelewe Mwakyembe.Acha kukurupuka huo Mwiba usije ukakuchoma mwenyewe
 
Mwiba nahisi wewe upo katika kundi la Lowasa au ulikuwa unaneemeka kama Mtikila alivyo kuwa ananeemeka kwa RA.
Mwakyembe kaongea ukweli mtupu hapo hii ndo aibu inayo wakumba marais wetu kuweka mawaziri wasio kuwa na sifa,yule waziri wa ZNZ ni bomu hafai hata kwa bure Karume mtimue huyo anakuharibia kibarua chako kwa wananchi.
 

I admit this guy so Called Mwiba had and still has pyschological problems and need professional counciling. Haihitaji akili ya ziada kujua alichokisema Mwakyembe kuhusu watumishi wa Umma kuhoji kauli ya Waziri mkuu kuwa ni utovu wa nidhamu kwa Serikali na kwa PM mwenyewe. Mwakyembe alitumwa kuchunguza mchakato wa Richmond na kutoa report na pia yeye sio Mwajiriwa wa serikali bali ni msimamizi wa serikali. Hivyo kumtaka Mwakyembe aadhibiwe ni utovu wa nidhamu mwingine na nashawika kuwa huyu ni mwiba ni Mwathirika wa vitendo vya uwajibikaji wa mafisadi na hii thread inamwelekeo wa kifisadi na ukosefu wa ueledi wa mambo
 
Utangulizi
Tafadhalini msiutete uzembe japo unauma ,na ikiwa ni watu wa Jazba hamtafika pahala katika kujadili.
Hivi huyu hakusema kama kuna mambu aliyaweka kando katika taarifa yao,na kama angeyasema basi serikali kwa maana na wengine wangekuwa matatani ?
Ni jambo gani lililompelekea kuwataja akina Lowasa na ufisadi wao na kuwawacha wengine ?
Msiwe mnababaika na viongozi walioficha baadhi na kuyaeleza baadhi.Ni kosa kuwaunga mkono watu wa aina hiyo,kwani hakuitenda katika ripoti yake iwe iwavyo kuwa kina Lowasa wamehusika,sikatai lakini kuna mambu huyu mheshimiwa aliyaficha kwa kauli yake mwenyewe ,hilo ni kosa wakati umeaminiwa au umekabidhiwa tatizo la nchi kulitolea ripoti halafu baada ya ripoti na watu kuekwa kiti moto ,unaruka kama mwanamke alieshikwa mbavu , oo mengine sikuyataja kwa sababu bwamkubwa nae angekuwa matatani . Sasa mtu wa aina hii utamwamini kwa lipi kama si mpika majungu.

Hapa naona mnachanganya mambo,na mnashindwa kupambanua ,mawazo na maoni yenu nimeyaona yote yamebase kwenye kwenye conclusion,kwama Mwakiyembe ni mtu safi & that is wrong , once he is on the side of Rulling party for me ,whatever ni mkweli kiasi gani basi ,sitakiwi kumuunga mkono kwa lolote lile mbele ya macho ya wananchi wapiga kura ni kuchoma na kuchoma tu, mpo ? Kama ni mpinzani wa kweli wa Chama kinachotawala hutakiwi kuwa upande wao hata siku moja ,kwa kila watakalolisema inabidi utafute chochote kile kutoka hicho walicho kisema ili ukifanyie kazi na kukiwekea pingamizi,mfano hata Raisi Kikwete akisema Mji mkuu wa tanzania ni Dodoma ,mimi nitaweka pembeni na kusema hapana Raisi amekosea Mji mkuu wa Tanzania ni Daresalaam na ushahidi nitatoa, hapo ndipo upinzani unaposhamiri na kuweka mikakati dhidi ya watawala.

Mambo ya ukweli upewe haki yake ,mambo hayo hayatakikani kufanyiwa Watawala hasa kwenye mfumo wa vyama vingi na ndio system za Ulaya katika upinzani zinavyofanya kazi ,wapinzani wanatakiwa watoe chochote kutoka kwa watawala na kukipinga kama raisi anavyotoa hotuba ya kila mwisho wa mwezi basi wapinzani walitakiwa na wao waisambaratishe hotuba juu chini,sio kukaa na kupiga makofi bungeni hayo ndio yatatufikisha pa kumuona Mwakiyembe na wengine wote ni watu safi na hivyo akina Mwakiyembe kuufikia umma kiurahisi ya kusema .....si mmeona hata Chadema na CuF na vyama vyengine vinatufagilia..........Amkeni wapinzani msiwe na jazba someni between ze line.

Baada ya Utangulizi.

Kama huyu Mwakiyembe ni hodari kuona kiongozi anakashifu ,atwambie kwa nini hakusimama na kusema Kikwete amekashifu Kiti cha Uraisi wa Tanzania ?
Kama yeye ana ubavu wa kweli kutetea Viongozi kwa nini hakusimamia utekelezwaji wa makubaliano ambao hao hao akina Shamhuna na wenzake waliupiga na chini na kumtoa Muungwana Kapa na kumkatisha matumaini.
Kama kuhatarisha Muungano ,Mwakiyembe angekuwa imara na kusimamia ulinzi wa Muungano pale wahafidhina walipodai warudishiwe ASP yao ,nini maana ya turudishieni ASP yetu na nyie mbakie na Tanu ,alete kina cha maana ya kauli hiyo.

Mwakiyembe alimsikia Shamhuna peke yake ! mbona Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar nae alilonga ,mbona Raza nae anaunguruma na kufika kusema wabunge wa Zanzibar warudi Zanzibar ,hayo Mwakiyembe hakuyaona.
Je Mwakiyembe hakuyasikia waliyosema kuwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar ni kama wimbo wa kwaya na serikali yake ni sawa na timu ya mpira,Mwakiembe hakuyaona hayo au angeliwaudhi wenziwe ? Hapa ahkudharauliwa raisi wala waziri kiongozi bali imedharauliwa nchi nzima na ni moja ya sababu ya kuzidisha malumbano na kuchochea ,Mwakiyembe angelisimama na kuwaita hawa kuwa ni wachochezi ,alifika kuwaita kusema hayo ? Au anaficha na akisema wengine watakuwa matatizoni ndio nikasema hafai isipokuwa anapalilia mlo wake au ulaji.

Mwakiyembe inaonyesha ni mgeni wa demokrasia na hafahamu haswa maana halisi ya demokrasia ,hivi na afike Uingereza kuna uwanja unakwenda unasema na kusema mpaka tosha yako ,kama unaponda basi huna mipaka utamponda kila unaemuona hafai.
Na hapa Tz ikiwa tumeamua kufuata demokrasia basi isiwe vibaya kumkosoa mtu na ndio neno alilotumia Mwakiyembe ,sasa alitaka watu wanyamaze kimya,kumnyooshea mtu kidole na kusema aadhibiwe hilo ni kosa hasa kwa kiongozi ,watu wanasema na wamesema mengi kuhusiana na hili la Zanzibar ni nchi au si nchi ,ikiwa Katiba mbili kila moja inasema kivyake sasa ulitegemea kuwa Shamhuna au wengine wamesema uwongo,ikiwa Pinda ametegemea Katiba ya Muungano wao wanosema Zanzibar ni Nchi wametegemea katiba yao Kosa lipo wapi la kuadhibiwa mtu.

Naona Mwakiyembe hakuwa shupavu kumueleza Pinda kuwa kusema mambo anayarudisha CCM sio sahihi wakati hili si jambo la CCM ,au Mwakiyembe alinyanyua mdomo kumwambia Pinda kuwa umetenda kosa kusema hivyo ,Mwakiyembe ni mwoga anaogopa kusema kwani hao ndio wenzake au sivyo ?

Mwakiyembe anaogopa Raisi kunyooshewa kidole machoni (anaogopa kusema kutiwa kidole machoni maana ndio lugha sahihi ya msemo huo) ,sasa kama raisi hajaelezewa hajanyooshewa kidole wakati yeye ndio mhusika mkuu wa taifa hili nani mwengine ambae ataweza kusikia au kusikiliza,tumewaona wanafunzi,walimu na wengine wote wanalia na Raisi ,Mwakiyembe hafahamu kama huku ni kunyooshewa kidole kwa Raisi,kelele za kuwafikisha mafisadi mahakamani ,hizi zote anaelekezewa kidole Raisi ,je Mwakiyembe hayaoni haya.

Kusema nina chuki binafsi na Mwakyembe hilo sikubaliani nalo wala mimi si mfuasi wa Shamhuna ,lakini Mwakiyembe amekwenda mbali na hili analolifanya ni kuhimiza udikteta ambao ulikuwa siri ndani ya Chama cha CCM lakini sasa subira zimewashinda wanawindana mchana kweupe ,zamani wakiitana kwa vikao vya ndani na kupeana mawaidha wengine wakikaripiwa kama wanavyosema wengine wakiambiwa wajiuzulu na kikao baada ya kumalizika wengine hushikwa na magonjwa na kufa.

-------------------------------------
Alisema endapo Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi wa Baraza la Mawaziri akiamua jambo na kulitolea ufafanuzi, hairuhusiwi kwa waziri yoyote kupinga maamuzi hayo, kwani kwa kufanya hivyo ni kutoheshimu kiongozi huyo na ni utovu wa nidhamu.
------------------------------------------
Sasa nini faida ya watu hawa ikiwa kupinga maamuzi ni utovu wa nidamu ?

Hayo hapo juu ni maneno ya Mwakiyembe yaliopo kwenye gazeti ,hivi hivyo ndivyo inavyoendeshwa serikali ,heshima hiyo ndio iliyowapa ruhusa akina Mwakiyembe kuwapandisha mkenge wenzao maana kuuliza,kuhoji na kupinga ni utovu wa nidhamu ? Hivi kama hivyo ndivyo anavyoona Mwakiyembe hamwoni kama akina Lowasa walizulumiwa. Maana ni utovu wa nidhamu kwa aliechini kusikika akipaza sauti kupinga akina Mwakiyembe na wenziwe walishindwa kutumia aidha wakiogopa kuwa watovu wa nidhamu.na Kumwacha Waziri Mkuu Lowasa atumbukie,na ndio hawahawa akina mwakiyembe wanaogopa kumshauri au kumpinga Raisi kwa kuwa watakuwa watovu wa nidhamu na hawana adabu ,hivyo hata wakimuona Raisi anatumbukia kwenye shimo ,WaTanzania wasitegemee kuwa Raisi wao atasshauriwa vilivyo ili kuepuka mradi raisi kasema haya twendeni basi watakwenda wanaogopa kumvunjia heshima raisi ,wanaogopa kumshauri raisi,wanaogopa kumhoji Raisi wanaogopa kumuelekeza Raisi ,sasa nini faida ya akina Mwakiyembe ? Jawabu ni kusinzia kwenye vikao wakishituliwa na makofi na wao wanaamka na kupiga makofi hata hawajui kinachozungumzwa.
 
Shamuhuna Just A Pimp Of Karume Anajipendekeza Tu, Pia Hufanya Dirt Jobs Za Karume,ndiyo Maana Unaona Anakaujasili Ka Kibaraka He Must Be Strip Out ,ebu Tafuteni Ktk Kamati Ya Watu 18 Ilyo Ongozwa Na Sefu Bakari Yeye Alikuwapo Au Ni Mtoto Wale Thags Jinsi Anavyo Behave Kama Wale Jamaa Kwenye Ile Kamati Ya Mauwaji.
 

I'm sorry that you didn't like what I wrote--but that does not change my stand either--coz I sincerely believe that this guy (Mwiba) needs a good and immediate professional counselling.

I know we all have our bad days, but this man must truly be insane.
 
Huyo Mwakiyembe inaonyesha ni hodari wa kupika majungu na anaonyesha ana akili ya kidikteta , kijana kama ni mfuasi wa CCM basi majadiliano yatakuumisa maana ni kuchoma tu.Soma ujumbe uliokuwepo huku juu uone ukosefu wa Mwakiyembe na Chama Chake ,hawa ni watu waliobobea katika kupika na kupakua,kama msipoangalia watazidi kujikita na kujitanua katika kila pembe ya Tanzania CCM ni kikosi hatari kwa WaTanganyika na WaZanzibari lazima waondolewe.
 

Yakhe Mwiba wa Mwiba naona unachuki binafsi na mwakyembe weyeeh!! Tatizo nini hasa au kwakuwa kasema ukweli juu ya waziri wako? Kama wazanzibari wote ni kama Shamhuna, Raza na Mwiba basi mna kazi.
 
 
Mkuu Bill, kama huyu Mwiba kakusoma hapa na bado hajaelewa basi ni kweli kwa ushauri wa bure ni vema akapimwe yeye binafsi ajijue tatizo lake.
Maelezo yote yako wazi.
 
nafikiri huyu aliyeta hii mada hapa kakurupuka tu nafikiri asome vizuri kwanza kabla ya kuleta mjadala watu wengine tusipoteze muda buree...
 
Du, sikujua kama mtu anayeelewa mambo (kama ulivyo Mwiba, ingawa sikujui) anaweza kulinganisha vitu viwili tofauti. Sioni kama suala la Znz kuwa nchi lina uhusiano wowote na tuhuma za ufisadi. Nilishasema kuwa kina Shamhuna na mwenzake Raza ni hatari kwa nchi kwa matamshi yao. Wasipothibitiwa wataleta dhahama kubwa. Lakini wajue hakuna lolote watalopata zaidi ya kuchinjana wao kwa wao. Rais wa Znz yuko wapi kukemea hayo. Au anayaunga mkono kama alivyofanya Aboud Jumbe? Mwakyembe kanena.
 
Binafsi ninaheshimu sana watu ambao wana msimamo na kile ambacho wanakiamini na hawaogopi kusema hivyo mbele ya mtu yoyote bila kujali ni Rais au Polisi (hata kama mimi sikubaliani nacho). Sidhani kama PM kusema kuwa 'Zanzibar si nchi' alafu ikatokea mtu yeyote mwingine akasema 'Zanzibar ni nchi' basi mtu huyo anastahili kuitwa mtovu wa nidhamu. Woga wetu kwa viongozi wa juu wa serekali wa kuongea yale ambayo tunaamini ni kweli (hata kama si kweli) umetutia matatizoni kwenye masuala mengi, enzi za 'hewala bwana' zimeshapita!
 
Wakati, hoja zikiendelea hebu tafuteni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasemaje juu Nchi iitwayo Tanzania? hakuna nchi ya Zanzibar bali kuna Tanzania Zanzibar au tanzania visiwani mbona hili lipo wazi wala hali hitaji kuwa graduate!
 
Kwa kumsaidia Mwiba , Mwakyembe hakusababisha Lowasa ajiulu, bali tume iliyoundwa na Bunge na yeye kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo ndiyo iliyogundua uozo huo na kisha ikatoa taarifa yake kwa bunge ambayo pia iliambatana na mapendekezo kadhaa. zaidi jamani nchi yetu inaoongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania ambayo wabunge, wote,wanaapa kuilinda hali kadhalika baraza la mawaziri nalo lina Collective responsibility sasa anaye mtetea Shamhuna anajua haya au basi siku tumeamua kuongea kadri bongo zetu zinavyotutuma?
 
Last edited:

KKN, the gist here is what in leadership circles they call "collectice responsibility." wakati Kiongozi kama PM anapotetea katiba, na si msimamo wake, basi viongozi wengine wanapaswa kukubali kwa pamoja kuitetea hoja yake hiyo ndani ya katiba.

Hata hivyo, kama kuna mapungufu, mapungufu hayo yanaainishwa kama mapungufu ni ya katiba au ya Pinda binafsi. Kwa Shamhuna, alipaswa kuchambua udhaifu wakatiba zetu--zote za Znz na URT kwa njia iliyo sahihi ya kiuongozi kwa mujibu wa taratibu za kiutawala, na si kuanzisha zogo lilinaloweza kuhatarisha amani hasa unapoona watu wanataka kuandamana juu ya jambo ambalo hata wewe unajua fika haliwezi kutatuliwa kwa maandamano.

Aliyeuliza swali lwa Zanzibar kama ni nchi ama la ni Mzanzibari, na kwa lugha ya mitaani, alijua kuwa anawasha moto wa makusudi. Hii inakufanya ufikirie zaidi kama ni hivyo, what was the motive behind? Je yeye hajui kama zanzibar ni nchi au si nchi kweli? au ametumwa? Na nani? 44 yrs after Union, kwa nini swali hili liulizwe? Walikuwa wanaishi wapi...kwenye nchi au kusiko nchi?

Wanasheria mbali mbali, hata Wazenj wenyewe, na hata CUF seniro officials wanakiri kuwa Znz imekosa power ya kuengage na external world, kitu muhimu cha nne ili i qualify kuwa nchi. Hii ina maana ni semi autonomous island...ina hadhi ya kujiamulia mambo yake yenyewe lakini yale yaliyo nje ya Muungano tu. Yaliyo ndani ya Muungano, si nchi. Nje ya Muungano, si nchi.

Huu ndo muundo wa Muungano ambaosiku zote tumekuwa tukiambiwa ni wa aina yake duniani. Kama Shamhuna amekuwa akilijua hili siku zote, kumpinga Pinda ni kutaka tu cheap political credits. Ndo maana watu wanaojua utawala wanadhani kuwa alikuwa amaekosea kwa makusudi, na hivyo anapaswa kadhibiwa. Nyendo kama hizi zinaweza kusababisha rebellion katika nchi, na ni aibu kusababishwa na kiongozi.

Lakini, anaweza kuonekana shujaa pia kama akihama Chama, ili awe na msimamo wake na hataonekana kubanwa na collective responsibility.

Mrema, mzee wa inji hii, naye aliwajibishwa kwa kosa kama hili pia.
 
Pia ukisoma katiba ya Zanzibar sura ya pili ibara ya 9(1) inasema Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.
9(2)(a) inasema mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi ....
Tell me je tutafika?
 
The definition of sovereignty carries an absolute effect.

If Zanzibar is sovereign, why did it withdraw from OIC?

It seems to me they want t be sovereign, currently they are not.

Tatizo lenu nyinyi ni kuwa mnashindwa kuwaelewa Wazanzibari na kilio chao. Wewe hushangai kuwa wote wana maoni yanayoshikilia kuwa Zanzibar ni Nchi. Wamo wasomi humo wenye mashahada (tena siyo moja bali mashahada pengine matatu kwa mpigo). Wote wanaelewa vizuri dhana ya sovereignity, wanaelewa vizuri hisotoria ya Muungano, wanaelwa vizuri katiba ya Jamhuri ya Muungano, na wanauelewa vizuri mfumo unaotumika. Hao hawataki wawe na sovereignity (ya Zanzibar) kama unavyodhania. Please wasome (between the lines). Kelele zao ni kuwa -wanajua kuwa mdhibiti wa sovereignity yetu (kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ni Serikali ya Jamhuri ya Tanzania. Kilio ni Jee Soveregnity hiyo inatumika ipasavyo kukidhi haja na matakwa ya Watu wa Zanzibar(matakwa ya Baraza la Wawakilishi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Madaraka ya Rais na Baraza lake la Mawaziri). Jibu haitumiki ipasavyo hivi sasa. Dawa ni kutafuta ufumbuzi wa hiyo sovereignity itumike kama yalivyo matarajio yao. Usibeze -kwa hiyo kauli ya kuuliza Zanzibar Nchi au si Nchi. Don't take it literally Bro. dig between the lines.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…