Nimesikiliza BBC leo jioni, Mzee Nassoro Hassan Moyo akihojiwa. Picha ninayoipata ni kuwa Hati ya muungano haionekani au haijulikani ilipo. Mzee Moyo anasema, waliokuwapo siku hiyo kama mashahidi ni yeye, mzee kambona, mzee lusinde, mzee munanka, na mzee mmoja alikuwa anajulikana kama haluwa na hati hiyo walishuhudia ikisainiwa na Karume na Mwalimu. Cha ajabu ni kuwa wote hawajui ilipo na ilikuwa inasemaje.

Jamani kwa anayejua naomba atujuze hati hii ilipo, na sisi wana muungano haki yetu ni ipi katika swala zima linalohusu hati ya muungano, aidha kujua inasema nini au nakala zake kuwekwa mahala ambapo tunaweza kuisoma.

Naomba nilipokosea nisahihishwe.

Nawakilisha.

Akhsanteni.
 
Ya nini? huyo babu aliyehojiwa ndo anakusumbua akili? punguzeni mikwara mbuzi, tunawajua.
kama kuna marekebisho ya katiba au katiba mpya sawa, hiyo haki.
porojo nyingine za kujadili kugawa nchi hiyo sahau.
Kikwete mwenyewe Ubavu hana.
 
Ya nini? huyo babu aliyehojiwa ndo anakusumbua akili? punguzeni mikwara mbuzi, tunawajua.
kama kuna marekebisho ya katiba au katiba mpya sawa, hiyo haki.
porojo nyingine za kujadili kugawa nchi hiyo sahau.
Kikwete mwenyewe Ubavu hana.

Pharaoh acha jazba mkuu, tunachotaka ni majadiliano na kujuzana mkuu. kwani sisi kama watanzania hatuna haki ya kujua hati ya muungano ina content gani?? au ndo kuuziwa mlio wa mbuzi kwa bei ya mbuzi??
 
Pharaoh acha jazba mkuu, tunachotaka ni majadiliano na kujuzana mkuu. kwani sisi kama watanzania hatuna haki ya kujua hati ya muungano ina content gani?? au ndo kuuziwa mlio wa mbuzi kwa bei ya mbuzi??

Shida sio hati. Kwa nini tutafute hati ya kitu ambacho hakitakiwi, hati itasaidia nini? Labda kama unataka kuisoma kama historia.
 
Kwani waliificha/wanaificha wapi hadi haijulikani ina nini?
 
Hapa sijui nani wa kualumiwa. Kama yeye Nasoro Moyo alion a ikisainiwa lakini na karume akaondoka na nakala yake, basi angeulizwa Karume alikopeleka hati ile. Kwa vile hayupa basi baraza la mapinduzi la zanzibar ndilo liulizwe kwa vile ndilo lililokuwa linaunza serikali ya Zanzibar. Kupotea kwa nakala ya hati za Muungano hakubatilishi Muungano hasa kwa vile huyu Mzee katia ushahidi kuwa hati zilisainiwa.

Mtu aliyejua sana kulalamika, huwa hakosi cha kulalamikia. Iwapo malalamiko yanayohusu muungano yatakuwa mute, basi kutotakoea malalamiko mengine. Historia inaonyesha kuwa muda mfupi Baada ya mapinduzi ya Zanzibar, kisiwa cha pemba kilitangaza kujitenga na kuunda serikali yao ikijulikana kama Jamhuri ya Watu wa Pemba. Bendera yao ilikuwa hii hapa chini:

View attachment 28318

Nina wasi wasi na hawa walalamikaji kuishia kulaumia kisiwa kimoja dhidi ya kingine na mwishowe tukawa na Jamuhuri ya watu wa pemba kwani wale wapemba wote walioko Dar watyalazimika kurudi kwao.
 



"-Equal number kwa vigezo gani? Idadi ya watu? Tuelezene mlivyokuja na hiyo soultion equal number of people".


Kwa sababu Zanzibar ni equal partner katika huu "muungano" na sio sawa na Kagera.

Kama huu wewe huutaki, sisi tumeukataa zamani sana.

Daini Tanganyika yenu haraka kabla hamjaamka siku moja mkakuta hamna Tanzania wala Tanganyika.
 
Ndugu wadau, naomba JF ianzishe mjadala mpana katika huu mtandao wetu ili tujue ni watanzania wangapi wanautaka huu muungano ili ndiyo tufikirie jinsi ya kuuboresha kwa kuwa na serikali 3, n.k vinginevyo tuuvunjilie.

Katika mjadala, baadhi ya mambo ya kuzingatia ni:-
1. Ni watanganyika wangapi wanautaka na wananufaikaje nao
2. Ni wazanzibari wangapi wanautaka na wananufaikaje nao
3. Je, Tanganyika bila muungano itaathirika vipi
4. Je, Tanganyika bila muungano itanufaika vipi
5. Je, Zanzibar bila muungano itaathirika vipi
6. Je, Zanzibar bila muungano itanufaika vipi (Labga inejiunga na OIC, jumuiya ya
nchi za Kiarabu, nk)
7. Je kwa Zanzibar kuwa na rais wao (bara hawana), bendera yao, wimbo wao wa
Taifa na vitambulisho vyao vya Taifa haiashirii kwamba kumbe hata huo
muungano tunaoupigia kelele kumbe haupo, ulishajifia zamani?
8. Ni kwa nini tusiuvunje halafu Zanzibar ikawa nchi ya 6 kwenye jumuiya ya Afrika
ya Mashariki?
9. Je ni watu wangapi walioshiriki kwenye mjadala ambao hatimaye ulizaa huu
muungano? Isije ikawa ilikuwa ni ndoa ya mkeka!
10. Kwa nini tusiwe na Referendum juu ya suala zito kama muungano?

Naomba kuwasilisha.
 
Tuuvunje Muungano au tuuboreshe ili ku address hayo mapungufu?

Hapa hapana cha kuboresha jambo lolote lile, uvunjike tu ili tuwaondolee mzigo mnaoupigia kelele kila siku.

Mnaing'ang'ania Zanzibar kwa sababu ina faida kubwa kwenu, kama ni vyenginevyo mngekwisha kuiwacha.
 
Written by Harith Ghassany

05/05/2011



Suala la kujiuliza "tunautaka Muungano wa aina gani"? Muhimu ni kukubaliana juu ya aina ya Muungano tunaoutaka Wazanzibari. Lakini kabla ya hilo ni lazima kwanza tukubaliane kuzaliwa kwa Tanganyika kwa sababu kama Tanganyika haikuzaliwa tutakuwa na Muungano na nani?

Wala si muhimu kwa hivi sasa kujiuliza na kujibu vipi Tanganyika itazaliwa tena. Tukubaliane juu ya mtizamo kuwa Tanganyika izaliwe na ikae tena na Zanzibar kama ni mshirika alie sawa sawa na Tanganyika, na kuamua juu ya mfumo wa Muungano baada ya kukubaliana kuwepo kwa nchi ya Zanzibar na ya Tanganyika zenye sifa zake kamili za Kitaifa na za Kimataifa.

Tuweze kufika hapo kwanza na tutakapofika hapo tutaweza kuzungumza kwa pamoja juu ya aina za taasisi za Muungano wa nchi mbili zilizo sawa, na aina ya executive organ kama itakuwa ni Supreme Council of Heads of Government, i.e. Presidents of Zanzibar, Tanganyika, Kenya….

Kisichotakiwa na cha kuvunjwa ni "general approach" ilionayo Tanzania Bara juu ya Muungano uliopo ambayo ni "approach" iliozoweleka yenye kutumia "force" "domination", kibri na dharau juu ya Zanzibar na Wazanzibari. Approach ndio kitu asasi na muhimu. Ile approach ya miaka 47 ya Tanganyika na baadae Tanzania kutumia ubabe, ni lazima ivunjike na badala yake uje mtazamo mpya wa Muungano unaotokana na ridhaa (consent) ya Wazanzibari.

Wazanzibari wanafahamu fika kuwa Muungano wa mabavu hautakiwi na umeshavunjika na unafaa uvunjwe. Lakini huu wa ridhaa pia hatutoupata bila ya kwanza kuzaliwa Tanganyika. Hili ndilo la msingi. Tuwe na jazba dhidi ya Muungano wa mabavu na wenye kuidhalilisha Zanzibar.

Lakini baada ya jazba ya halali yenye kuukataa Muungano wa kimabavu, tukubaliane juu ya "general approach" ya kuzaliwa kwa Tanganyika kwanza na baadae tujadili mfumo wa Muungao wa ridhaa. Tukiikamata njia hii basi tutajua wapi tunataka Zanzibar na Tanganyika zielekee na katika mfumo wa aina gani.

Nchi za Ulaya si zile pale zimo katika European Union? Ndio zimechukuwa muda mrefu kufika zilipofika lakini zisingeliweza kufika hapo zilipofika kama wangelikuwa hawana "the right approach" na kutizamana kwa spirit ya usawa baina yao. Si wana Ufaransa, Ujerumani, nk, lakini si kila nchi ina chake na wana mashirikiano ya kiuchumi na kuyatatua matatizo ya pamoja? Lakini hakuna ujanja, wala dharau, wala majungu!

La kama tunataka kuanza kwa kusema tuuvunje Muungano bila ya kwanza kudai Tanganyika izaliwe na kudai Muungano wa ridhaa wenye mfumo wa nchi mbili zilizo huru na zenye sifa za Kitaifa na za Kimatifa, wa basi tutaonekena ni vichwa maji na si watu wa maana.

Tutaonekana Wazanzibari ni watu wenye kujuwa tusichokitaka lakini hatukijui tunachokitaka!
 
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na ni vigumu kwasababu si Wanzanzibar si wato tofauti ni watu walewale walioenda Zanzibar kwa utumwa au biashara. Wengi wao wana damu ya kiarabu lakini wa Zanzibar karibu wote wana damu ya bara. Kama wanataka kuondoka waondoke lakini waache mashamba yetu na watafute sehemu nyingine.
 
Unashamba wapi weye? Mbona sikuelewi hebu sema unashamba wapi? Labda shamba la bangi
 



May 6, 2011 by zanzibardaima

i
Rate This​


ALASIRI moja nikiwa kwenye hoteli niliyoshukia mji mkuu wa Sudan, Khartoum Hilton, nilishuhudia vurumai kubwa katika sehemu ya karibu na lifti. Watu wakikimbilia huko wakiambizana kwa msisimko kuwa ‘sheikh amefika, sheikh amefika.’
Afisa wa serikali ya Sudan aliyekuwa na jukumu la kunihudumia (ambaye pia huenda alikuwa shushushu) naye alipiga mbio kumkimbilia huyo sheikh na mimi sikuwa na budi ila kupiga mbio na kumfuata.
Tulipofika kwenye lifti nilimwona huyo sheikh akiwa amevaa kanzu na bushti jeupe. Uso wake uliokuwa na ndevu kama za tambi ulikuwa mwembamba na ukiangaza chini. Nakumbuka alipiga kilemba lakini chake kilikuwa kidogo si kama ile milemba inayopendwa na Wasudani.
Kwa nukta chache sana nilimshuhudia huyo sheikh akiingia kwenye lifti na ndevu zake za tambi huku akizungukwa na kundi la waliokuwa wakimyenyekea. Huyo sheikh alikuwa Osama bin Laden. Siku hizo hakuwa na umaarufu, au sifa ya uovu, aliyoipata miaka michache tu baadaye.
Wakati huo Rais Omar Hassan al-Bashir alikuwa akiandaa mijadala mbalimbali ya kuleta demokrasia na katiba mpya nchini humo. Lakini sidhani kama Osama bin Laden aliwasili Sudan kwa minajili hiyo; kwani sikumbuki kumshuhudia tena kwenye vikao mbalimbali vilivyofanywa kwa zoezi hilo.
Kwa hivyo, siwezi kusema kwamba niliwahi kuonana na bin Laden lakini mtu niliyemuona mara kwa mara na niliyebahatika kuzungumza naye kwa faragha kwa muda wa saa mbili alikuwa sheikh mwengine, Hassan al Turabi ambaye wakati huo alikuwa na mahusiano mazuri na bin Laden.
Tukiwa kwenye chumba cha maktaba yake nyumbani kwake katika sehemu za kaskazini za Khartoum, Turabi alizungumza kuhusu mahusiano ya Zanzibar na Oman. Katika masimulizi yake alinihadithia mengi kuwahusu Mwalimu Julius Nyerere na Mfalme Qaboos bin Said wa Oman. Sitoyanukuu aliyoniambia kumhusu Qaboos.
Ama kumhusu Nyerere, mwanasiasa huyo wa Sudan ambaye sasa ni mpinzani mkubwa wa serikali ya huko ambaye juzi tu alifunguliwa gerezani, alionyesha kuitilia shaka dhamira ya Nyerere ya kuziunganisha nchi za Tanganyika na Zanzibar.
Turabi aliniambia kuwa dhamira halisi ya Nyerere kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni kuuvunja Uislamu katika Afrika ya Mashariki. Hiyo ni shtuma nzito na nyeti hasa sasa ambapo udini umeingia katika siasa za Tanzania. Ulimi wangu niliufyata.
Sina shaka yo yote kwamba Nyerere mwenyewe angeliisikia shtuma hiyo angekasirika bila ya kiasi. Yeye akishikilia kwamba kuziunganisha nchi hizi mbili ilikuwa hatua ya kuelekea lengo la kuleta umoja wa nchi zote barani Afrika.
Nyerere alianza kuuimba wimbo huo kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika uliofanywa Cairo mwaka 1965 alipozikaribisha nchi nyingine za Kiafrika ziingie kwenye Muungano huo. Kwa bahati, sijui nzuri au mbaya, hakuna nchi yo yote iliyomsikiliza. Hata Zambia iliyokuwa na fungamano kubwa na Tanganyika haikujiunga.
Historia inamsuta Nyerere. Inaonyesha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuundwa kwa dhamiri ya kuleta umoja wa Afrika.
Kwa mfano, nyaraka za Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, zinaonyesha ushahidi wa jinsi Marekani na Uingereza zilivyomtaka Nyerere auunde huo Muungano kwa manufaa ya nchi za Magharibi. Nchi hizo, hasa Marekani na Uingereza, zikihofu Zanzibar, chini ya serikali ya Mapinduzi, kugeuka na kuwa ‘Cuba ya Afrika.’
Kwa ufupi, madola hayo ya Magharibi yakihofia kwamba Zanzibar ingeweza kuyasambaza mapinduzi ya Kikoministi katika bara la Afrika. Si kwamba mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ya Kikoministi lakini hizo ndizo zilizokuwa fikra finyu za madola hayo katika enzi hizo ambapo Marekani na washirika wake walikuwa wakichuana na maadui zao Wakikoministi.
Maelezo ya uundwaji wa Muungano ni mengi — ya kweli na ya uongo yamekuwa yakitiwa sana hewani kiasi cha kwamba waliozaliwa baada ya Muungano kuundwa wanababaika; hawajui wayashike yepi wayaache yepi.
Visiwani Zanzibar, kwa mfano, kuna wenye kuamini kwamba viongozi wa Tanganyika walikuwa na njama ambayo hadi leo wanayo. Nayo ni njama ya kuiona Zanzibar inatoweka, kwamba wakitaka, na eti bado wanataka, kuifanya Unguja iwe sehemu ya Mkoa wa Pwani na Pemba iwe sehemu ya Mkoa wa Tanga. Yaani kwa ufupi wanataka kuimeza Zanzibar.
Lililo bayana ni kwamba waasisi wa Muungano, yaani Nyerere na Karume, hawakuwa na misimamo sawa kuhusu Muungano.
Nyerere aliwahi kuulizwa na mwandishi Colin Legum wa gazeti la Observer la Uingereza mwaka 1968 iwapo ataridhia pindi Zanzibar itataka kujitoa kutoka kwenye Muungano huo. Alijibu kwamba hatotumia nguvu na hatowapiga mabomu Wazanzibari waukubali Muungano ikiwa hayo yatakuwa matakwa yao.
Nyerere aliyasema hayo wakati Karume akiwa hai. Ingawaje, miaka baada ya Karume kufariki Nyerere alisema kwamba angeweza kuvumilia watu wake waangamize kila kitu ikiwa pamoja na Azimio la Arusha, lakini hakuwa tayari kuuona Muungano unavunjika.
Mzee Karume, kwa upande wake, aliufananisha Muungano na koti. ‘Unalivaa unapolihitaji na unalivua likikubana,’ aliwahi kusema.
Juu ya tofauti hizo, hamna shaka yo yote kwamba waasisi wa Muungano wakitambua vyema kwamba Muungano waliouunda ni wa mataifa mawili yaliyo huru.
Siku mbili hizi kumekuwa na tetesi nyingi kwenye magazeti mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Muungano na hatima yake. Kwa bahati si uhaini kulizungumza suala hilo wala kuzungumzia uwezekano wa kuvunjika kwa Muungano.
Hali kadhalika tunaona wenye kulijadili suala hili kwa jazba na wenye kuliangalia kwa makini. Kuna wenye kutaka pawepo na serikali moja tu nchini Tanzania, wakimaanisha kwamba serikali ya Zanzibar ifutwe. Kuna wenye kutaka Muungano uvunjwe. Na kuna wenye kushikilia kuwa muundo wa sasa wa Muungano usigeuzwe.
Lakini huu muundo wa sasa ambao umekuwako kwa muda unaokaribia nusu karne ndio uliowafanya Wazanzibari wengi walalame kwamba wamemezwa na Tanganyika. Muundo huo pia umewafanya watu wa iliyokuwa Tanganyika walalamike kwamba Zanzibar imekuwa mzigo mkubwa kwao kuubeba.
Kwa hakika ni jambo la kusikitisha kusikia kuwa kuna viongozi Tanzania Bara ambao bado hawataki kukubali kuwa Wazanzibari wana hisia za uchungu dhidi ya Muungano.
Kwa mwenye macho ni wazi kwamba mfumo uliopo sasa hauridhishi na kwamba umezusha mashakil mengi kuliko natija. Hivyo, panahitajika mfumo mpya wa mahusiano baina ya Tanganyika na Zanzibar, nchi mbili zilizo huru katika Muungano huu.
Wazanzibari wengi wanahisi kwamba ili udumu Muungano utabidi ubadili muundo wake na uwe na muundo wa serikali tatu. Tena katika mfumo mpya pasiwe na nchi moja itayojipa jukumu la kuiongoza nyingine, yaani pasizuke hali kama iliyozuka karibuni pale serikali ya Muungano ilipojaribu kuufikisha muswada wa kuipitia katiba bila ya kuishauri serikali ya Zanzibar.
Na kwa hili la katiba viongozi wa serikali ya Muungano lazima watambue kuwa mjadala tu wa kukusanya maoni ya wananchi hautoshi. Unahitaji kufuatiliwa na kongamano la kitaifa litakalowajumuisha wanasiasa, viongozi wa kidini, wawakilishi wa jumuiya na asasi za kiraia na jumuiya za kupigania haki za binadamu.
Katika nchi zote kulikofanyika mkutano wa kitaifa wa kuandika katiba mpya, kumewezekana kuwekwa misingi imara ya demokrasia na utawala bora. Mfano mzuri ni Benin. Hii ni nchi ambayo iliwahi kujinata kuwa ya kwanza Afrika kufuata nadharia ya Marx na Lenin wakati wa utawala wa Mathieu Kerekou mnamo miaka ya 1970.
Licha ya hayo, Benin iliibuka kuwa nchi ya kwanza barani humu kulikubali wimbi la mabadiliko. Pakafanywa mkutano wa kikatiba mwaka 1990 uliofuatiwa na uchaguzi ambao ulimuangusha Kerekou 1991. Miaka mitano baadaye Kerekou alirudi madarakani alipomshinda Nicephore Soglo.
Mbali na Benin, kuna nchi pia kama vile Botswana na Mauritius, ambazo zinaweza kuzifunza nchi nyengine kuhusiana na demokrasia na utawala bora. Zinaweza kufanya hivyo kwa vile zina katiba zinazofuata misingi ya kisheria na si matakwa ya anayetawala. Na katiba hizo zinafanya kazi sawasawa.
Kwa Tanzania pamoja na hayo kuna haja kubwa ya kuzingatia utungwaji wa katiba utakaokwenda sambamba na suala la Muungano kwa pande zote mbili. Masuala haya mawili ni chanda na pete. Haitowezekana kupata katiba bila ya kupata suluhisho la suala la Muungano.
Inavyoonyesha ni kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaweza tu kuokolewa endapo katiba ya Muungano itafanyiwa marekebisho ili pawepo mfumo wa serikali tatu. Kilicho muhimu zaidi ni madaraka na mamlaka gani itapewa serikali ya Muungano na gani yatapewa serikali za kila moja ya nchi mbili katika Muungano huo.
Itakuwa kosa kuiendeleza ile dhana ya kwamba hakuna njia au mfumo wowote mwengine wa kutetea na kuhami maslahi ya Tanganyika na maslahi ya Zanzibar nje ya Muungano kama ulivyo sasa.
Itakuwa pia ni upuuzi mtupu kushikilia kuwa urekebishwaji wa katiba utaoipa Zanzibar madaraka na mamlaka zaidi utahatarisha amani, usalama na ufanisi wa Tanganyika au kwamba Zanzibar itaweza kutumiwa na madola ya nje kuyadhuru maslahi ya Tanganyika.
Makala ya RAIA MWEMA ya tarehe 4 Mei 2011
 

Attachments

  • 1963 UN Zanzibar.jpg
    13.3 KB · Views: 29


Hujui hata unachokisema na si ajabu hata kuwa hata wewe hujijui?
 

Asante kwa kutujuza mkuu. Ila bana mara nyingi thread zako zinakuwa ndeefu unnecesarily. Unaanzia mbaali, mara nikashuka Khartoum, ama baada ya ..., na ..., na ... Nakumbuka kwenye mitihani mingi hasa ya vyuo sharti mojawapo muhimu ni "Go straight to the point" and "Avoid Verbosity".

Turudi kwenye mada:

1. Turabi alikuwa rafiki wa Osama (RIP): Ningekuwa Pilato aliyeandikwa kwenye Biblia ningerarua mavazi yangu straight away - kuna haja gani tena ya ushahidi? Hivi ulitegemea kauli ya Turabi iweje katika hili? Kama ilivyokuwa kwa Marehemu Sheikh Usama bin Laden, tayari Turabi yuko kwenye "kifungo" cha udini na asingesema aliyoyasema ingeshangaza.

2. Turabi/Usama sio manabii: Inaonekana ndugu yangu kwako kauli za hawa jamaa na watu wa aina yao unaziamini bila hata kuhoji kana kwamba wao ni manabii! Yaani watu wengine wote ni wapumbavu kuhusu suala la muungano ila hawa jamaa. Ndio maana hata wamerikani waliamua kwenda "kumzika" baharini kwani wasingekosekana wa "kufanya hija" kwenye kaburi lake kama angezikwa kikawaida.


3. Muungano ni mkataba: Muungano ni mkataba tena wa kimataifa na taratibu zake zilikuwa na ziko wazi na wajibu na haki za kila upande ziliwekwa wazi na suala la UDINI/DINI sidhani kama ni miongoni mwa mambo ya Muungano.

Hivi ulitegemea Turabi na Usama ambao kwao ni UISLAMU KWANZA waongeeje? Jifunze kuwa na mawazo huru ili uwe huru. Usiruhusu mwingine afikirie kwa niaba yako hata kama ni mkuu wako wa dini.
 
Kwa hivi sasa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni rais wa Tanganyika vile vile. Mamlaka yake yanaeleweka. Tukishaunda serikali tatu, rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na mamlaka gani? Kwa sababu hataweza kusimamia masuala ya Tanganyika na Zanzibar, na kwa sababu Tanganyika ndiyo iliyo na jeshi kubwa rais wa Tanganyika hatakubali mamlaka yake ya kuwa amiri mkuu wa majeshi yachukuliwe. Sasa huyu rais wa serikali ya tatu atakuwa na mamlaka gani? Au tumfanye tu awe ceremonial kama rais wa Israel, kazi yake iwe kutuwakilisha kwenye mazishi ya waheshimiwa wa nchi za je?
 


Sisi hatutaki tatu wala mbili wala moja.

Zanzibar irudi kwa wenyewe, mengine tutajuana baadae.
 
Mkuu tunakushukuru kwa mada yako nzuri. Ila kuhusisha uislamu,osama,turabi na muundo wa Tanzania ni kupotoka. Kiukweli Hamna mtu yeyote aliyewakataza wazanzibar wasilete waraka wa kujitoa ktk muungano na mbara akagoma,hamna! Hutosikia hata siku moja watanganyika wanaandamana kupinga z'bar kujiondoa ktk muungano. Nakuomba uweke udini wako pembeni,z'bar ikiwa na uislamu,itawaumaje watanganyika? Je kwani tanganyika haikuwa na haina waislamu wazawa?? Ni mwendawazimu pekee atakayehusisha udini na muundo wa Tanzania. Nami ningependa muondoke mkajitawale z'bar lakini wala si kwa kusema uislamu unahujumiwa. Sijawahi kuwaza wala sitegemei kuamini kuwa uislamu ni ughaidi au uuaji kama unavotufanya tuhamini unavo relate Turab, Osama bin Laden na uislamu. Japokuwa nimeanza kuona wanahoujumu uislamu wanatuhaminisha kuwa Osama kapata mazishi na heshima ya mwisho ya kiislamu, Tanzania misikiti na masheikh wahujumu uislamu wanalinda na kutetea serikali 'jangili',aya yote hayatanifanya niamini kuwa uislamu ni ughaidi/ukatili,hapana, mi naamini uislamu ni dini tukufu ya Mungu,mpaka hapo itakapofika kiwango cha kutosha kuamini kuwa akina Turab,osama,gadaff na mubarrak ndo wanaoufanya na kuutangaza ughaidi na ukatili kwa baraka za udini wao. Mkuu mkitaka kuondoka bara,ondoka tu. Pia haiitaji kuandika mukataba wa kujitoa. Mkiona viongozi wetu wana hamu ya muungano huu feki,mwaweza kuanza kwa kuondoka bara,kususa vikao,kuhamisha mali zenu na kugoma kuvuka kuja bara,mpaka serikali itatambua mahitaji yenu ya kujifungia zanzibar. Igeni kutoka kwa waafrika wa marekani wa "BACK 2AFRICA MOVEMENT" na nyie anzisha "BACK TO ZANZIBAR MOVEMENT"
 
Wakuu zangu msitake kuingiza uislaam ktk maswala ya Osama na huyo Turabi kwa sababu hamjui Uislaam ni nini.. na zaidi ya hapo hamjui kwa nini Osama alikuwa mpinzani wa Marekani na vibaraka wake..Kwa maneno haya simuungi mkono Osama kwa hatua alizochukua dhidi ya Marekani na dunia kwa ujumla isipokuwa sababu za msingi ambazo yeye aliziona kuwa cheche za mageuzi aliyoyataka..

Osama kama Osama alichukia nguvu ya Marekani ktk uchumi wa Saudia na hasa jinsi shirika la mzee Bush lilivyoweza kucukua mabillioni ya fedha kama mbia wa baba yake. Ni chuki ambayo hata wewe unaweza kuwanayo kwa Barricks au shirika lolote la nje isipokuwa tofauti inaweza kuwa maamuzi yako ktk kuitekeleza hiyo chuki..

Sisi wote tunamchukia Osama na wala hakuna mtu anayefurahia hawa kina Turabi jinsi wanavyowanyanyasa waislaam wenzao chini ya utawala wa huyo Bashir, na inaongezea nguvu zaidi kumwona mwandishi wetu hapa akijisifia sana kuonana na watu kama Osama na Turabi kisha kujiweka nao kundi moja kifikra na kuelezea maswala ya Muungano wa Tanzania.

Mtu huyu ni hatari na uhatari wake hauna Uislaam isipokuwa chuki na ghadhabu kubwa walokuwa nayo hawa member wa Al qaeda kiasi kwamba ananipa mashaka makubwa zaidi kuwepo hotelini siku ambayo huyo Osama anaingia Hotel hiyo hiyo pasipo yeye kuwekewa kashaka. Ina maana moja tu ni mwenzao hivyo kwa utangulizi wake tu tayari kisha nipa shaka kubwa dhamira yake kuhusiana na Muungano na yawezekana moja ya agenda za mkutano ulompeleka Sudan ilikuwa kuzungumzia Muungano wetu.

Isije kuwa huyu ni mshirika wa mabomu yaliyolipuka ubalozi wa Marekani nchini hivyo chuki yake haikuanzia ktk swala la Muungano ila inarudi nyuma zaidi ktk mahusiano baina ya Nyerere na Qaboos..Dhahiri mwandishi anatuonyesha jinsi Uoman wake unavyoweza kuathiri Muungano wetu kutokana na chuki zake binafsi au washirika wenzake, kisha utawasikia watu wakisema hizi vuguvugu za madai ya Muungano hayana mikono ya watu wenye nia mbaya na Zanzibar..Watu kama hawa ndio wanafanya Muungano ulindwe kwa nguvu zote kwa sababu Zanzibar kwao ni koloni ambalo watajaribu kwa kila njia kuonyesha uhalali wao kulitawala..

Nitaruidia tena kwenu watu wa kitabu (Wakristu), kuhusisha Uislaam na matendo wa watu waovu ni sawa na kuhusisha Ukristu na kulawiti watoto wadogo wakati mkijua fika kwamba Ukristu na vitu hivyo havihusiani ila ni akili mbovu ya wahusika wanaotumia dini kufanya maovu yao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…