Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Mkuu, haiendi hivyo .... huku ninakofanya kazi gharama ya uzalishaji pipa moja ni less than $35; na huku ni Marekani ... offshore Gulf of Mexico ... na hiyo $35/barrel ni kwa kisima cha urefu wa zaidi ya 18,000 feet! .... Tanzania labour charges ni cheap, na isitoshe nimeona seismic images za baadhi ya maeneo ya Bongo ... looks like visima vyake havitazidi 12,000 feet ... so it will be even cheaper!
Kuna haja ya viongozi wetu kujifunza kutoka kwa Joseph Kabila na Vladimir Putin, hawa wakubwa huongea maneno machache sana tena kwa tahadhari kubwa. Ukweli kauli ya mh.Pinda imeleta mtafaruku mkubwa zanzibar, kauli hiyo ilipaswa kutamkwa na jk au ak.
Kwanini kusiwe na kipya? Wazanzibari wametunisha misuli na hivyo itabidi walainishwe na kwa upande wa Bara watatakiwa kuacha mchezo wa kuwadharaulisha SMZ mbele ya wananchi.
Hata hivyo kiburi cha CCM Bara kimeshaiponza CCM Zanzibar kwani 2010 mikakati ya mizengwe huenda Wazanzibari wengi wasikubaliane nayo safari hii na mshindi wa kweli wa uchaguzi kupatikana ili suala hili la Muungano lipate utatuzi. Kwa Wazanzibari Uzanzibari kwanza na vyama vitafuata.
Mpaka pale tatizo hili litapopatiwa usuluhishi wa kutowa madaraka zaidi kwa Zanzibar nachelea CCM ina wakati mgumu,
Has anyone ever asked themselves what will happen in our next general elections if the majority winner of house of representative and presidency of Zanzibar is not CCM?
It is still uneconomical. Kuna factors nyingi. Lazima wafanye research, mbona mbishi wewee? Lazima pia wajue kuna kiasi gani, na kisima kitakuwa na umri gani. Waangalie na cost za decomissioning (kama wanajali).
Kwasasa hivi kampuni haliwezi kutoka Canada kichwakichwa au marekani wakati kwao wanachimba kiulaini. Mafuta yapo ya kumwaga huko kwao, unachokonoa tu.
Incase huja notice, makampuni yanayopata blocks Tanzania ni makampuni yasiyokuwa na stakes kubwa duniani, wala hayajawahi kusikika dunia hii (this alone should tell you alot about Tanzania as a country). We unaweza kuniambia kwanini BP waliondoka Tanzania? Unajua wanafanya biashara gani Tanzania? What will happen, yakipiga jackpot, makampuni makubwa zaidi yatayanunua haya makampuni. Kuna vikampuni vingene vimenunuliwa kwasababu cost za kusearch wanapoteza hela. wamepewa blocks wakaingia kichwakichwa.
Sasa wewe inabidi utulie ungalie mchezo unachezwa vipi. Ila mafuta yapo, but its uneconomical so far. Wazanzibari wanajua wanataka nini.
P.s Makampuni makubwa TZ ni mawili tu. Wabrazil na kuna la wamarekani.
Kuna wana CCM wametoka kwenye mkutano ,ngoja tusubiri uzushi.Muda huu ndio wnatoka nje kwa ajili ya lunch, tunaweza kupata japo nyepesi nini kilikuwa kinazungumzwa na kujadiliwa humo ndani ya kikao...hii ni JF bwana....