Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na Muungano wa Siria na Ejibti walioungana 1958

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na Muungano wa Siria na Ejibti walioungana 1958

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni muungano wa kupigiwa mfano duniani na muungano uliodumu miaka 55 kwa sasa.

Ni dola mbili huru zilizoungana Tanganyika walipata uhuru wao Desemba 9/1961 na wapata kiti chao cha Umoja wa Kimataifa tarehe 14/Desemba 1961 namba ya kiti chao (GA Resolution 1667 (XVI)) na Zanzibar nao walipata uhuru wao tarehe 9 Desemba 1963 na wakapata kiti chao cha Umoja wa Kimataifa 16 Desemba 1963 namba ya kiti chao (GA Resolution 1975 (XIII)). Uhuru wao ulifikia April 26 mataifa mawili huru waliungana na ikawa Tanzania lakini 2 November 1964 kupitia Wizara ya mambo ya nchi za nje waliandikia Umoja wa Mataifa na kutaka kwamba iondoshwe Zanzibar na iondoshwe Tanganyika na kujulikana kama Tanzania.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na Muungano wa Siria na Ejibti walioungana 1958 na ni sawa na muungano wa Yemeni ya Kaskazini na Kusini walioungana 1990 na kwa bahati mbaya muungano wa Siria na Ejibti ulivunjwa mwaka 1961 (ulidumu kwa miaka 3).

Kwa sasa muungano wa Tanganyika na zanzibar umefikia hatua nzuri na ni mfano wa wakuigwa duniani lakini miungano ipo mingi imefanana na ndio Tanzania ukapatikana muungano uliofanana nayo.
Hata hivyo pamoja na kuwa muungano huu una muundo wa kipekee na kuwa umedumu kuliko miungano mingi iliyowahi kuwapo Africa.

Muungano wa kwanza ulikuwa ni ule wan chi za afrika Magharibi, mwishoni mwa miaka 50 na mwanzoni mwa miaka 60, ulioanza na nchi mbili Ghana na Guinea na baadaye Mali ikajiunga nao. Muungano huu ulitokana na vurugu la umajimui wa Afrika (Pan Africanism), vinara wake wakiwa kwame Nkurumah wa Ghana, Sekou Toure wa Guinea na Modibo Keita wa Mali.

Novemba 1958 uliundwa muungano wa Ghana na Guinea mara muungano wa Ghana na Guinea mara baada ya mkutano wa watu Afrika (All African Peoples Conference). Ghana ilitoa fedha nyingi na kuipa Guinea ili ijitoe haraka kutoka katika utegemezi wa Ufaransa.

Mei 1959 ikatangazwa kuwa umoja huo utatambulika kama umoja wa Dola za Kiafrika. Ilipofika April 1961, Mali nayo ilijiunga na umoja huo. Muungano huo ulivunjika mwaka 1962 kutokana na vita baridi, ambapo Guinea ilionekana ikinyooshea mikono Marekani wakati wenzake waliku wakifuata mrengo wa kusho wa Karl Marx / Lenin.

Muungano mwingine wan chi za Africa ulifanyika mwaka 1981 baina ya nchi za Senegal na Gambia, uliojulikana kama Senegambia ambao ulikufa mwaka 1989.

Kwa mfano muungano wa Cameroon waliungana mwaka 1961 Cameroon ya mashariki na Cameroon ya magharibi ambayo wakati wa ukoloni Cameroon ya mashariki ilitawaliwa na Ufaransa na Cameroon ya magharibi ilitawaliwa na Uingereza ambao muungano wao upo mpaka sasa ni miaka 59.

Lakini kwa Tanzania matatizo ya muungano yalionekana mengi na hata baadhi ya wazanzibar kuulalamikia na kujitokeza wanazanzibar 10 kwenda Mahakani na kudai mkataba wa Muungano halisi wa tarehe 26 April 1964 na kuambiwa au kujibiwa na mwanasheria mkuu ndani ya mahakama kuu ya Zanzibar kuwa hakuna mkataba wa muungano huo halali ilipokwenda kesi hiyo na kuambiwa na mahakama kuwa suala la muungano ni kama ardhi kwa sababu muungano ni wanchi na nchi ni sehemu na inaweza kuhojiwa ndani ya miaka kumi na mbili (12) huwezi kuhoji kwa maana hiyo ni halali kwa mujibu wa sheria ukizingatia waliohoji mwaka 2004 sawa na miaka 40 toka 1964 mpaka 2004.

Kwa hiyo hata masuala ya ardhi kama mtu atamiliki kwa miaka 12 bila ya kuhojiwa basi itamuhalalishia, lakini katika suala hilo la mkataba wa muungano limekwisha pale Ikulu Dar es Salaam au ikulu ya Jamhuri ya muungano kutoa mkataba huo hadharani tarehe 14/4/2014 na kuoneshwa kwa waandishi wa habari na wananchi kuona kwa kupitia runinga zetu kama hiyo haitoshi bada ya bunge maalumu la katiba kuomba hati hiyo halisi ya muungano nao waliletewa tarehe 16/4/2014 na kila mbunge wa bunge maalumu la katiba alipatiwa nakala hiyo na mwenyekiti wa bunge hilo la katiba na kwa sasa suala hilo sio ishu tena kwa watanzania muungano halali na utazidi kuwa halali zaidi tutapomaliza kutunga katiba na wananchi na kupiga kura ya maoni na kuipitisha kwa kuikubali na kuanza kuitumaini kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba namba 38.

Lakini Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar umekumbwa na misukosuko mingi hususani kero za muungano huo zimezungumzwa kwa muda mwingi tena kwa pande zote mbili za Tanzania katika mabunge na mabaraza na wananchi kupiga kelele na kufikia kuundwa kamati ya kero za muungano ikiongozwa na makamo wa kwanza wa raisi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania akisaidiwa na makamo wa pili wa raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Tume hiyo iliyo na uwiano na pande zote mbili za muungano imepokea kero kumi na moja za muungano na kwa sasa wameshazitatua tisa zimebaki mbili ambazo ziko njiani kutatuliwa kwa hivyo kwa upande wa kero wamefikia hatua nzuri sana.

Hata hivyo Miungano mingi duniani inakuwa na kero lakini hutatuliwa kwa ushirikano wa pande zote mbili za muungano na kwa mantiki hiyo basi kero ni vitu vya kawaida katika muungano ya nchi kwa nchi mataifa na jamii kwa ujumla kwa hivyo watanzania tunakila sababu ya kujivunia muungano huu. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una faida kwa pande zote mbili za muungano na muungano unaozungumzika kwa mujibu wa sheria.

Tumeshuhudia wananchi wa pande zote mbili wakitembeleana bila bugdha kwa misingi ileile ya sheria na katiba ya Tanzania kifungu namba 17(1) kwa ufupi iloeleza mtanzania anaweza kuishi popote na kwenda popote ili mradi asivunje sheria na kwa hiyo kuonekana katiba ya Tanzania ni katiba ya watu na inajali utu kwa mujibu wa sheria. Na hiyo kifungu cha 15 cha katiba ya Tanzania pale iposema watu wote ni sawa mbele ya sheria na hakuna alojuu ya sheria sote tuko chini ya sheria kwa mujibu wa sheria na haya hata katiba iliyopendekezwa hayo yote yamo.

Na kwa hivyo kuonekana muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) unafuata sheria, katiba na haki za binadamu na kuwa na tawala bora na ndio utawala wa sheria. Kwa sasa taifa la Tanzania lina watu wasiopungua milioni 44, na kwa upande wa Zanzibar pekee watu wasiozidi milioni moja na laki 3, bado muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar unategemea rasilimali watu kwa kujenga mustakabali mzima wa uchumi na wa kisiasa kwa kuwa na mustakabali wanchi yenye amani na utulivu na bado kwa sasa waafrika na duniani kote wanausifia muungano huu kwa kuigwa mfano kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana na yaliyoshikamana amani na utulivu kwa kuepukana na migogoro iliokuwa haileti maendeleo kwa taifa letu.

Na kuoenakana muungano uliokuwa una ustawi wa jamii kwa pande zote mbili za muungano.

Nchi nyingi duniani zilizoungana zimewea kupata maendeleo ya kasi kiuchumi na kiulinzi kwa kutumia maendeleo yao na kutumia rasilimali zao sambamba na rasilimali watu na kuweza kujikomboa kiuchumi na kupandisha uchumi wao.

Na kwa Tanzania kupitia muungano limewezekana hilo. Kwa hivyo watanzania wanatakiwa wauenzi muungano huu uliosiasiwa na maraisi wawili Mwalimu Nyerere na Marehemu Karume.

Muunguno huu ni wakuwaenzi marehemu hao ambao ni wakombozi wa Tanganyika na Zanzibar na vilevile majemedari hawa waliona mbali na wakafikia kuunganisha nchi zao kwa maelewano mazuri na kufikia kusema wewe utakuwa raisi na mimi nitakuwa makamo na walifanya hivyo kwa kujua kuna haki na usawa na kwa kuamini wakiungana hakuna atowachezea katika taifa lao. Kwa kuamini watakuwa na taifa moja madhubuti lilokuwa haliyumbi wala kuyumbishwa na ndo ilivyo hadi sasa ni fahari yetu kuwa muungano na ni fahari yetu kutimiza miaka 55 ya muungano na kwa kuitwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Vilevile Muungano huu wa Tanzania ulisifiwa sana kuwa muungano uliokuwa mbele kwa ukombozi wa nchi za Afrika na hata kufikia kuwa Tanzania ni kambi kubwa ya ukombozi wa nchi za Afrika.

Na bado kama kuna nchi ambazo zinataka kuungana basi zije kusoma Tanzania na watajua nini muungano wa dhati wakushibana na kiundugu wa kweli na ukweli ukitawala katika muungano wowote ule basi muungano huo hudumu milele.

Lakini kwa sasa miaka 55 tunasheherekea kwa upande wa Zanzibar wanaona Muungano umeelemea upande mmoja mpaka sasa hivi tunavozungumza haijawahi kuapta Zanzibar Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Majeshi, Mshika fedha mkuu tuliwambia wastahamili kamati ya kero za Muungano ipo inafanya kazi kisheria na wanaweza kuwafanyia kazi mambo yote hayo wanoyaona na mengineyo kwa mujibu wa sheria.

Hongera Dc. Magufuli na hongera Dc. Sheni kwa kuendeleza misingi ileile ya uhuru na kazi kwa kuudumisha Muungano huu kwadhati.

AHSANTE

RASHID YUSSUF MCHENGA
MWANASIASA MKONGWE/MWANAHARAKATI
NAIBU KATIBU MKUU THE TANZANIA DEMOCRATIC ALLIANCE (TADEA) ZANZIBAR

ZAIDI UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
= > Lipo wapi tatizo kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Tafakari!

= > Waliohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wafikia hatua gani?

= > Yajue mambo 22 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

= > Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar?

= > Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

= > Fahamu A-Z kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

= > Tuna Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tu, siyo Tanzania

= >
 
Nimekerwa na hizo pongezi kwa Magufuli na Shein , hawa hawana sababu za kupongezwa maana katika kipindi chao kero za muungano zimezidi na hata kumbukumbu ya muungano wenyewe wameizika
 
Nimekerwa na hizo pongezi kwa Magufuli na Shein , hawa hawana sababu za kupongezwa maana katika kipindi chao kero za muungano zimezidi na hata kumbukumbu ya muungano wenyewe wameizika
Muungano huu haufanani na muungano wa ijipti na siria
 
Back
Top Bottom