Sijaona jibu la hoja iliyotolewa...kuwa kama Chadema haimo ni kwanini? binafsi nimependa umoja wa aina hiyo kwani unaleta upinzani wa kweli ila tatizo la umoja kama huu ni vyama kutoaminiana hasa katika ngazi za juu kama uraisi..nadhani hii inaweza kuwa na matokeo mazuri kwa muungano huo kwani Kenya walifanikiwa. kinachotakiwa ni dhamira ya dhati ya wanaoungana na sio kuwabeza kuwa wanaratibiwa na CCM kwani hiyo ni kuwakatisha tamaa...nadhani pia mgawanyiko uliopo unaweza kusababisha CCM kushinda coz wakiungana wote CCM atapata za wanachama wake tu na wao watapata za wapinzani wote..nadhani iko haja ya vyama kuunganisha nguvu ila kwakuwa kila mtu anataka ale yeye basi huwa hawawezi kuungana hata kwenye mambo ya msingi, walijaribu wakaishia hewani.