Muungano - wateja hawautaki, wadhamini wanapigia chapuo

Mkwai

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
306
Reaction score
96
Nimepitia hotuba ya jarioba jana, katika aya zinazohusu muungano tumeendelea kusikia mapendekezo kadha ambayo yamekuwa yakitolewa na tume mbalimbali, viongozi, taasisi, na hata vyama mbalimbali zinazopendekeza kubadilishwa kwa muundo wa serikali ya muungano uliopo.

Sura hizi na uoga wa kubadilika badilika na kutokujiamini kwa viongozi wetu (HASA WA BARA) hazikuanza sasa, ni za muda mrefu hata wakati wa kuundwa kwa muungano wenyewe. Kuna mzee mstahafu kutoka kwenye vyombo ya ulinzi na usalama aliwahi kuniambia kuwa muda mfupi baada ya muungano, mmoja wa waasisi aliyekuwa visiwani alimuomba/kumshauri mwenzake wa bara wafanye nchi moja; wa bara alisita, wa visiwani akamwambia usihofu juu ya itifaki za kiuongozi; tuanze, wewe uwe raisi na mimi makamo, lakini tuunde nchi moja. Hilo halikutekelezeka, inasemekana ni kwa sababu wa bara eidha hakuwa na msimamo au kuna mambo ambayo eidha aliyakwepa au aliogopa lawama ya historia mbaleni. Kwa mtazamo wa jicho la tatu, inaonekana viongozi na wananchi wa visiwani wana misimamo ya dhati ukilinganisha na wa bara; huenda bara wana ushwawishi hasa kutoikana na mfumo uliopo, lakini ki msimamo visiwano wapo vizuri zaidi.

Kwa mtazamo wangu baada ya kupitia kurasa kadha wa kadha za kabla, wakati na baada ya muungano; yaonyesha hakuna mahala penye uwazi wa 100% wa kuufunga muungano. Na viongozi wengi wa sasa wakiwa nje ya majukwaa hawapendezwi na aina muungano uliopo.

SWALI, JE! NI WADHAMINI NDIO WANAOTUSHINIKIZA TUENDELEE KUKUMBATIA AINA MUUNGANO ULIOIPO?
 
Huu muungano hauna tofauti na mashine za t.r.a kwanza mkataba wenyewe wameuficha kama wako tayari na mwendelezo wauweke hadharani ule mkataba halali wa mzee karume na mwlm julius nyerere pasipo kutafuna maneno hawana ubavu huo na safari hii ccm wamazipata za uso.
 
Kificho, speaker wa baraza la wawakilishi Zanzibar na waraka wake, na Kificho wa CCM Dodoma anakuwa wapi?
 
Mkuu huu muungano hauna mkataba wowote tunachotumia ni ile picha wanayoonekana Karume na Nyerere wakichanganya mchanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…