Muuzaji wa duka la dawa anatakiwa

Muuzaji wa duka la dawa anatakiwa

Ligamba

Member
Joined
Jul 4, 2021
Posts
16
Reaction score
19
Eneo la Kazi ni Kibiti Pwani, awe msichana anayeweza kufanya kazi kt mazingira ya kijijini kidogo. Biashara ni ndogo na inaanza ila kwa eneo lilivyo baada ya muda mfupi nategemea matokeo makubwa. Akiwa mkristo ni lazima ahudhurie kanisani, na akiwa muislamu hali kadhalika.

Mshahara kwa kuanza utakuwa elfu 60 kwa mwezi, kula na kulala ni juu yangu, mshahara utakuwa unapanda kadri biashara inavyokua.

Karibu PM kwa mwenye kuhitaji. Mungu awabariki.
 
Unamaana ya sh 2000 kwa siku? Kama atapatikana usije na uzi wa kufilisiwa kwa hilo duka kwa kuibiwa
 
Aisee hata kama ndio biashara inaanza ongeza mshahara. Hiyo kazi ni lazima mtu awe na taaluma ya madawa ndio umpe elfu 60 hata kama anakaa kwako?
 
Mtu alilipa millions of money kuja kulipwa 2000 kwa siku na kupewa chakula & malazi. Sitoi lawama kwa yeyote
 
Mtu alilipa millions of money kuja kulipwa 2000 kwa siku na kupewa chakula & malazi. Sitoi lawama kwa yeyote
Always life is not fair at all, pesa yote mtu anayolipa kusoma madawa, muda wote, hustle zote za kusoma na kufaulu then ajira iyo mtu unalipwa 60,000.

Mungu atupambanie sana sisi watoto wa masikini.
 
Aisee hata kama ndio biashara inaanza ongeza mshahara. Hiyo kazi ni lazima mtu awe na taaluma ya madawa ndio umpe elfu 60 hata kama anakaa kwako?
Nishauri ifike ngap angalau? Hatokaa kwangu, nitampangia na kumnunulia kila kitu na chakula
 
Mpe 150k mshahala na posho ya siku mpe 2500 hyo ndo level ya dispenser, 1year in pharmaceutical studies.

Kumbuka level ikipanda mshahara unapandaga, kwa 60k labda umpe yote Kama nauli sio mshahara huwez pata mtu kwa hyo hela.
 
Back
Top Bottom