Muwasho sehemu ya haja kubwa na ndogo

Muwasho sehemu ya haja kubwa na ndogo

Lady

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2010
Posts
282
Reaction score
62
Habari wana Jf,
Nina mdogo wangu wa kike ana miaka 24, amekuwa akilalamika muda mrefu kidogo anasumbuliwa na muwasho sehemu ya haja kubwa na ndogo, anaweza kuwa na tatizo gani?
Natanguliza shukrani!
 
kabla aujampeleka hospital akapime minyooo kwanza,minyooo huwa inachangia pia
akipima kama anayo anywe dawa kama bado mpeleke Hospital
 
Thanks, nitaenda kumpima minyoo.
 
Siyo minyoo, hizo ni fangaz - si tatizo kubwa kama hazijaenea sana, kuna dawa na kupaka na kudumbukiza sehemu ya haja ndogo. na kama imeenea sana kuna vindonge anaweza tumia.
 
Habari wana Jf,
Nina mdogo wangu wa kike ana miaka 24, amekuwa akilalamika muda mrefu kidogo anasumbuliwa na muwasho sehemu ya haja kubwa na ndogo, anaweza kuwa na tatizo gani?
Natanguliza shukrani!

ninachowapendea wabongo, wana tafsida sana...mtu akiwa na tatizo lake binafsi kabisaaa, anasema sio la kwake ni la mdogo wake, mwingine anasema la rafiki yake, mwingine anasema ni la mtu fulani, etc alimradi tu message iwe sent.
 
Kama walivyosema baadhi yafuatayo yanaweza kuwa sababu nikianzia na sehemu ya haja kubwa:

1. minyoo inabidi akapime na kupata dawa; namna ya kupima ataelekezwa na daktari aidha kupeleka choo kubwa au kubandika plaster wakati wa kulala na kuibandua asubuhi halafu inaenda kupimwa kwani miyoo mingine ina kuwa ndani ya ngozi lakini juu juu;

2. afanye sit bath - awekwe maji ya joto la kukanda kidonda halafu ake humo kwenye beseni kwa muda wa dakika 5 mpaka 10, hii itasaidia na mbele pia;

3 apime kipimo cha endoscope kuangalia kama kuna michaniko au kunaota vinyama na baadae kupewa dawa kama suppositories;

4. afanye mazoezi;

5. ale chakula chenye fibre kama mboga za majani, brown bread na kunywa maji kwa wingi;

6. aende haja kubwa kila anapojiisikia, asijaribu kuibana aua kuairisha - choo kigumu uleta michaniko kwenye njia ya haja kubwa;

7. asitumie toilet paper tena baada ya haja kubwa, atumie maji tu - kwa maneno mengine awe msafi sana.

Haja ndogo ni kwamba akapime - maana huko kuna njia mbili: ya uzazi na mkojo sasa sijui shida hiko wapi, hapa hakuna ujanja ni kupima tu. Na awe muwazi na asione aibu kwani mficha ugonjwa kifo umuumbua!
 
Thanks, nitaenda kumpima minyoo.

Ndugu yangu..hongera kwa kumsaidia nduguyo katika shida yake hii.

Hata hivyo naomba kukupa ushauri nje ya hili - Mdogo wako ana miaka 24 ikimaanisha kuwa ni mtu mzima. Nina maana kuwa katika hali ya kawaida huyu angeweza kuwa mama mwenye watoto wake na familia.Kama hawezi kujitambua kwa mambo yanayomhusu itakuwaje pale anapotakiwa kuwahudumia wengine?

Nakuomba sana...umkazanie nduguyo huyu kujibidisha kutafuta taarifa hasa zinazohusu afya yake. Awe na kawaida kujisomea makala mbalimbali na sasa magazeti mengi hadi ya udaku huwa na makala zenye kuelimisha kuhusu magonjwa mbalimbali.

Pamoja na wengine kukushauri akapime minyoo, naomba umshauri pia swala la kuzingatia usafi wa nguo za ndani na usafi binafsi huko kunako kwa maana ya kuoga na kunawa na maji safi, kuvaa cotton underwears, kuzingatia usafi siku zake na kupata ushauri zaidi wa mtaalamu wa magonjwa ya wanawake (Gynecologist).
Samahani sana kama ushauri wangu utakukwaza ni katika kuelimishana tu.
 
Thanks Woman os Substance, nadhani nitamtilia msisitizo swala la usafi pia na kujijua afya yake!
 
Huko haja ndogo labda usafi na fangasi
but huko haja kubwa isije kuwa kaanza ule mchezo.....
Just a thought.....
 
Mmh! sijui, manake nisiusemee moyo!
 
Habari wana Jf,
Nina mdogo wangu wa kike ana miaka 24, amekuwa akilalamika muda mrefu kidogo anasumbuliwa na muwasho sehemu ya haja kubwa na ndogo, anaweza kuwa na tatizo gani?
Natanguliza shukrani!


Atakua na fungus.
Awe anakausha sehemu hizo na taulo kila baada ya kuoga au baada ya kutawaza.
 
hili tatizo hata mimi limenitoke na hivi sasa natumia dawa nyingine ni za kuchomeka mkunduni!
 
Back
Top Bottom