Kama walivyosema baadhi yafuatayo yanaweza kuwa sababu nikianzia na sehemu ya haja kubwa:
1. minyoo inabidi akapime na kupata dawa; namna ya kupima ataelekezwa na daktari aidha kupeleka choo kubwa au kubandika plaster wakati wa kulala na kuibandua asubuhi halafu inaenda kupimwa kwani miyoo mingine ina kuwa ndani ya ngozi lakini juu juu;
2. afanye sit bath - awekwe maji ya joto la kukanda kidonda halafu ake humo kwenye beseni kwa muda wa dakika 5 mpaka 10, hii itasaidia na mbele pia;
3 apime kipimo cha endoscope kuangalia kama kuna michaniko au kunaota vinyama na baadae kupewa dawa kama suppositories;
4. afanye mazoezi;
5. ale chakula chenye fibre kama mboga za majani, brown bread na kunywa maji kwa wingi;
6. aende haja kubwa kila anapojiisikia, asijaribu kuibana aua kuairisha - choo kigumu uleta michaniko kwenye njia ya haja kubwa;
7. asitumie toilet paper tena baada ya haja kubwa, atumie maji tu - kwa maneno mengine awe msafi sana.
Haja ndogo ni kwamba akapime - maana huko kuna njia mbili: ya uzazi na mkojo sasa sijui shida hiko wapi, hapa hakuna ujanja ni kupima tu. Na awe muwazi na asione aibu kwani mficha ugonjwa kifo umuumbua!