Mmkjj,
Unajua hata mimi mwanzoni sikukuelewa,nilidhani unamaanisha alichokiimba Dr.Lemmy kwamba;
Hata katika sherehe za serekali
mbele ya mwenyekiti kuhutubia
ni mziki unaanza kuwakusanya watu
mziki asili yake wapieeee
Nilijiwa pia na mawazo kwamba labda wataibuka na nyimbo zinazoshangilia kudhibitiwa kwa mafisadi, mfano wa ule wimbo wa enzi za Sokoine v/s wahujumu;
Bomu limeisha pasuka
wahujumu wanatangatanga
milanguzi nayo imo ndanieee
Nimefikiria pia kile ambacho Mpoto na mwenzake wanakiimba katika salamu kwa mjomba, kwamba;
Rushwa ni wimbo wa sumu
ulioenea katika ubongo
wa kila mwana Taifa hili
tuondolee wimbo huu tafadhali
turejeshee nyimbo zetu za makuzi
Vibwayaaa...[/I]
Mawazo mengine yalinituma kwamba sasa wazee wazima wameamua kutumia hazina waliyonayo na kuthibitisha ujuzi hauzeeki, maana nasikia mzee Makamba kilichomwibua hadi kufika alipo leo ni uongozi mahili wa kwaya. Hapo ongeza Mhe. Kolimba and ze TOT;
Tieni tieni
kwa moyo mmoja
nambari wani eeeh
Aidha kidogo niitimishe kwamba huenda mziki huo ukawa kama alichokisema Luck Dube R.I.P kwamba
But the music they played
was not good
for the Rastaman,yeah
was not good for the real jah man
I'm going back to my roots
ops,kumbe unamaanisha nyeti ambazo bila shaka soon utatushirikisha,fanya hima tafadhali.