Uchaguzi 2020 Muziki na kampeni za Uchaguzi 2020

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Muziki ni kitu kinachotumika kuamsha hisia za wengi na kuandaa akili kwa ajili ya kupokea ujumbe fulani. Wakati mwingine kutokana na ushawishi wa muziki tu, mtu huamua kuchagua hata kifo badala ya kuishi. Muziki una nguvu ya ajabu sana.

Katika kampeni wakati wa uchaguzi, wale wanaofanikiwa kuutumia muziki vizuri, wanapata wafuasi wengi sana hata kama walikuwa hawajui hili. Hii sana inategemea na aina ya muziki unaopigwa.

Muziki wa sebene
Huu ni muziki unaoongoza kwa kuamsha hisia za watu wengi sana hasa maeneo ya kanda ya ziwa ambako asilimia 60 ya watu wanaishi. Kwa kawaida makabila yanayoishi huku yana ngoma zao ambazo midundo yao inafanana kidogo na rhumba. Mfano wasukuma wahaya na makabila mengine ya mkoa wa Mara. Huku ukipiga mchiriku na au bongo fleva hutaamsha hisia za wengi.

Vyama inabidi mjipange sana na kuwa na uwezo wa kusoma hisia za wengi. CCM walifanikiwa sana na ule muziki wa rhumba wa TOT. Watu ilifikia sebene wanasahau kabisa shida zao.

Nimesikia muziki wa chibonge umebadilishwa kuwa wa CHADEMA. Ila bahati mbaya aliyefanya hivyo ameuharibu na hauna mvuto tena. Uko juu juu sana.

Maeneo ya pwani wapigieni mchiriku na bongo fleva mtawapata zaidi.
Kaskazini wapigieni Rege na hiphop mtawapata.

Mikoa ya kanda ya ziwa, Tabora, Katavi na Mbeya pigeni sebene mtawapata sana.

Kusini wapigieni zile nyimbo zilizozieleka za kitamaduni na bongo fleva ndio nyimbo zao.
 
Uko sahihi, kisaikolojia muziki huteka hisia za mtu, na kwa kiwango fulani huchangia maamuzi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…