Naamini Twanga watakuwa wanawashinda FM kwenye safu yao ya unenguaji tu, apart from that hamna kitu tena- wamekwisha siku hizi, naona kama wameishiwa tungo, wanaimba vitu visivyoeleweka, napenda kuwaangalia wacheza show wao tu, kwenye kunengua kwa kweli hawana mpinzani. Yani siku hizi wamechoka hadi hakuna kiingilio kwenye bonanza lao leaders na pamoja na kuwa ni bure, kumedorora kichizi.
Kitu kikubwa ninachowapendea FM ni safu yao ya waimbaji- Jose Mara, Pacho, Nyoshi, Pablo, King Blaise, etc. vyote hivi ni vipaji vya kutisha. Wakati vyombo vya Twanga vimechoka na kila ukiwasikiliza wakipiga live inakuwa kama ni makelele, FM ni tofauti kabisa, mtambo wao I think its the best in the country- ukiwasiliza live utadhani unasikiliza CD, very clear.
FM Academia, wazee wa mujini, wazee wa pamba, wazee wa blingbling- mambo yao iko juu ila wameudhi- si walipromise kuja huku UK hii easter? Mbona kimya?