Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MUZIKI ULIOCHELEWA WA OMARI KUNGUBAYA
Omari Kungu Baya alikuwa mpiga guitar maarufu katika miaka ya 1970.
Nyimbo yake, "Salaam za Wagonjwa," ilikuwa ikifungua kipindi cha Radio Tanzania Dar es Salaam, chenye jina kama hilo.
Alikuwa akipiga mziki wake Manzese kwa Mama Mary sasa kunaitwa Uwanja wa Fisi.
Ukitembelea sehemu hizo nyakati za jioni miaka hiyo hutoweza kukosa kusikia muziki wake.
Upigaji wa guitar wa staili wa Kungubaya haukuwa maarufu sana Tanganyika ulishika sana Kenya na pakawa na wapigaji wengi kama George Mukabi na Daud Kabaka.
Bahati mbaya sana Kungubaya alipiga muziki wa aina hii wa guitar moja wakati wake ukiwa ushapita sana.
Muziki huu wa guitar moja na chupa ikigongwa uliingizwa Tanganyika mwanzoni miaka ya 1950 Radio Dar es Salaam ilipoanzishwa mwaka wa 1952.
Huu ndiyo wakati Frank na Dada Zake walipoanza muziki wao uliokuwa maarufu sana.
Lakini Frank Humplink hakudumu sana katika upigaji huu wa guitar moja Peter Colmore alimchukua Nairobi katika bendi ya Jambo Boys iliyokuwa na wanamuziki kama Edward Masengo, Fundi Konde na Fadhili William.
Nyimbo za kwanza kusikika za mtindo huu katika Sauti ya Dar es Salaam zilikuwa za Mwenda Jean Bosco ambazo alirekodi Hugh Tracey na santuri zake kutengenezwa Afrika ya Kusini na kampuni ya Gallatone.
Bahati mbaya Omari Kungubaya amefariki bila kuacha nyimbo zilizorekodiwa kama hii ya wagonjwa.