Muziki wa dansi Ulipokuwa Muziki!!!

Naamini bado bongo dance inaweza ikarudi kivingine cheki twanga photo...Mzee bado anawasha moto na ana trend kisasa kabisa thru njia zilezile za vijana...ni suala la promoters na business people kuwekeza kwenye band na kutumia media Kwa nguvu kama wakati ule enzi za akina Kwa fujo djz,majizo foshizo,et al
 
M
Ila muziki wa dance kwa Tz Ulrich an game has na Wakongo!
Mimi nakukatalia,muziki was dansi ukiacha was kikongo ulianza kupata umaarufu baada ya KISA CHA MPEMBA ya African Stars Twanga Pepeta.Unawakumbuka Diamond Musical?

Labda nikutajie baadhi ya bendi zilizokuza mziki wa bongo na Kwa asilimia karibu 100 walikuwa wabongo:-
1.Twanga Pepeta
2.TOT Band/TOT Plus
3.Chuchu Sound
4.Diamond Musical
5.Pamo Sound
6.Mchinga Sound
7.Mviko Sound
8.TamTam

Hivi unawakumbuka wanamuziki hawa
1.Ally Choki
2.Banza Stone((RIP)
3.Badi Bakule
4.Mwinjuma Muumini
5.Waziri Sonyo
6.Luiza Mbutu
8.Rashid Mwenzingo
9.Jado FFu
10.Amina Ngaluma
11.Abdul Misambano
12.Leila Khatib (RIP)
13.Msafiri Diouf
14.Robert Hega katapila


Hivi unawakumbuka watu hawa
1.Gaby Katanga (RIP)
2.Deo Mwanambilimbi
3.Sheba Juma
4.Amigolasi Baba Sophy
5.Shaka zulu
6Andy Sekidia
7.Adolph Mbinga
8.Joseph Watuguru
N.k
Nyimbo kama hizi unazikumbuka?utamu wake vp?
1.Kisa cha Mpemba
2.Mtaji wa masikini
3.Jirani
4.Mgumba
5.Fadhila Kwa wazazi
6.Hodi hodi
7.Masimango
8.Fainali uzeeni

Jamani tumesahau mchango wa watu kana Master J kwenye kutayarisha mziki wa dansi mpaka ulipofikia hatua ile ya kupendwa,FM Studios,Enrico (kama nimekosea kuandika nisahihishwe).

Mchango wa Iron Lady Asha Baraka no mkubwa sana tena sana katika muziki wa dansi kamwe mchango wake hautasahaulika.
Marehemu Kapteni Komba pia alitoa mchango mkubwa chini ya usimamizi wa TOT Band/Plus.

Ushindani uliokuwepo kipindi hiko ndyo ulionogesha sana mziki wa dansi.

Huku Twanga Pepeta Huku TOT Band
Huku Ally choki Huku Banza Stone
Vijembe vya hapa na pale...Leo huyu akirusha hiki kesho mwingine amejibu basi inakuwa burudani kweli.

Kwa kifupi ukiangalia hapo waliofanya muziki wa dansi upate soko enzi hizo wala siyo wakongo Bali ni Watanzania.

Muda mwingine huwa natamani sana zama zile zingejirudia aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…