Muziki wa Taarabu umekufa kifo cha mende

Ray waniache

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2017
Posts
737
Reaction score
507
Yaani taarab qwishney toka mfalme aache habari ni kuwa sasa hivi hakuna jipya tena
Mashabiki walivunjika moyo mno kiasi kwamba wengi wakaanza kupoteza mood kbs
Huyu isha mashauzi naye hana jipya baada ya kuimba rhumba na kubuma sasa hivi kageukia umama ntilie

Hivi vibendi vingine vinaimba copy na taradance tu vingi vimeshachoka hoi bin taaban walitegemea wakizindua albam bhas cd au kanda zikiuzwa bhas wanapata pesa pia kupitia show

Sasa hivi nani anunue cd? watu wanaban cd bhana! maflash, memory card, bluetooth, na kudownload imekua habari ya mjini hivyo wanakosa income kwa upande huo
Haya walitegemea show sasa hivi uchumi ni mbaya nimeenda show nyingi za taarab kiingilio ni bia tu au soda

Sitasahau nilikwenda bendi moja kiingilio kilikua maji ya uhai, unaweza kushangaa
Mashabiki wamepungua tangu mzee aondoke ushindani hakuna. Kwenye show wengi ni mashahidi pesa hakuna Dsm hii hawafiki hata watu 40 halafu hapo bendi ina waimbaji 8 wapiga vinanda 4 mwenye bendi, na bado director wa bendi yaani you can cry aki vile

Hali ni tete hata ukipiga bure watu hawaji sijui ni kwanini
Kwahiyo mziki wa taarab unajifia polepole

Mkubwa fela aliitelekeza yamoto band akaanzisha bendi ya taarab inayoitwa YAH TEMEKE MODERN TAARAB alianzisha tu baada ya kusikia mzee ameacha kuimba alidhani hiyo bendi ndo itakuja juu iwe kinara wa, mziki huu lakini wapi sijawah hata kusikia ikizungumziwa hapa jf yaani sasa hivi mambo ni magumu

Tatizo watunzi kazi kutunga mipasho tu na manyimbo ya ajabu hata hazina ladha ya mziki wa taarab unategemea nani atasapoti kazi zao zilizododa? Taarab inajifia polepole kifo cha mende
 
tbt[emoji121] [emoji121] [emoji121] [emoji121]
 
Na hapo ndio utaamini kwamba wanamuziki wengi wanatumia nguvu za giza, freemason na king solomon magical powers ancient egypt science.

Angalia Mzee yusufu alivyokuwa na nguvu kaondoka kwenye bendi tuu muziki wote umekufa. Mwache atubu huwezi jua alitoa kafara kiasi gani za kishetani
 
Hali ya kipesa ndio sababu kubwa. Jero imerudi kuwa miatano.... chezea maguu weeewe!

Hureeeeee eti laki si pesa.... nani kasema...
 
nilikua shabiki wake namba 1 alivyoacha niliumia sana
 
Hali ya kipesa ndio sababu kubwa. Jero imerudi kuwa miatano.... chezea maguu weeewe!

Hureeeeee eti laki si pesa.... nani kasema...
acha tu mkuu bend kiingilio maji ya uhai
 
Mambo yanabadilika kila wakati,hata muziki WA dansi umeondoka na TX Moshi na Maalimi Gurumo
 
Wewe ndie ambaye ulileta thread kuhusu Le Mutuz majuzi..?
Kama ni wewe basi ni halali yako kwa aina hii ya thread
 
Una maana unanunua maji ya uhai unaanza kuserebuka hadi kuche! uwiii sasa tutacheza disco la Yesu
wanaweka maji ya uhai hapo km biashara ukija ukitaka userebuke shutu ununue maji ya uhai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…