Mv Liemba yenye umri wa miaka 113 yarejea ziwa Tanganyika

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Meli ya kihistoria MV Liemba, yenye umri wa miaka 113, imerejea katika Ziwa Tanganyika baada ya kukamilishiwa ukarabati mkubwa uliogharimu Sh bilioni 34. Ukarabati huo umehusisha injini, jenereta, mifumo ya kisasa ya urambazaji na usalama pamoja na maboresho ya huduma za abiria. Meli hiyo sasa imeanza safari zake tena, ikitarajiwa kuchochea usafiri, biashara na shughuli za kiuchumi kati ya Tanzania na nchi jirani zinazozunguka Ziwa Tanganyika.
 
Meli kama hiyo mpya NI BEI GANI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…