MV Nyerere yazama

MV Nyerere yazama

mndemeimran

Senior Member
Joined
May 7, 2017
Posts
112
Reaction score
74
KIVUKO CHA MV NYERERE CHAZAMA

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama muda huu, huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hicho hazijajulikana.

KUZAMA KWA KIVUKO
Shughuli za uokoaji abiria waliozama katika Kivuko cha Serikali cha MV. Nyerere kilichokuwa kikitoa huduma za safari ndani ya Ziwa Victoria kati ya Kisiwa Kikubwa cha Ukerewe na Ukara, kilichopinduka na kuzama leo, zimeanza ambapo hadi sasa zaidi ya watu 20 tu waliokuwa nje ya kivuko hicho wakining'inia, wameokolewa.

Sababu za awali za kuzama kivuko hicho inadaiwa kuwa ni idadi kubwa ya watu waliokuwa wamepanda pamoja na idadi kubwa ya mizigo ya magunia ya mahindi na mifuko ya saruji.

Taarifa kamili baadaye.

IMG-20180920-WA0016.jpeg
 
Asante kwa taarifa poleni watanzania wenzangu tuendelee kuijenga nchi yetu
 
HILI SUALA LA OVERLOADING HADI LINI??kuanzia Mv Bukoba na Spice zote sababu ni hiyo hiyo.Umefika wakati wahusika kuwajibishwa kwa adhabu kali zaidi kama kunyongwa hadharani au kifungo cha maisha.
TUMECHOKA KUPOTEZA NDUGU ZETU WASIO KUWA NA HATIA KWA SABABU YA UZEMBE WA WACHACHE
 
Muhusika ni serikali.
Kwani watu wanapenda kujazana kwenye meli?
hawapendi ila watafanyaje na ndo kivuko hicho hicho kimoja.
 
Mkiwa mnazungumzia Overloading msisahau kabisa daladala nda ya miji yenu hasa dar
 
Back
Top Bottom