Mkuu Q Man,
Nianze kwa kusema kwamba, kila unywele/nywele una sehemu mbili mzizi(root) na kishina chake(shaft).Na kila unywele huwa umejiviringa kwa vitu kama nyuzi nyuzi(strand) ambazo hujishikiza katika sehemu ya juu la fuvu la kichwa( scalp) kama follicle.
Kila follicle huwa na seli(pigment Cells) ambazo hutoa kemikali/kichochezi cha MELANIN.Hii huipa sehemu ya pili tuionayo kishina(shaft), ukuaji na rangi yake tuionayo mfano rangi nyeusi, nyekundu, kahawia n.k.
Ni melanin hii hii inayofanya rangi ya ngozi kuonekana jinsi ilivyo mfano(weusi, weupe, n.k).
Sasa kwa kadri muda(miaka inavyokwenda) chembe chembe chochezi hizi(pigment cells) hupungua kwa kufa taratibu katika follicles na hivyo kusababisha kiwango cha melanin ya nywele kuwa kidogo na hivyo kufanya muonekano ule tuuonao..MVI.
Sasa, katika kujibu swali lako kuna mambo kadhaa husababisha muonekano huo katika umri mdogo.Haya ni kama vile;
URITHI:
Wengi wa vijana wenye nywele za mvi, wazazi wao au wazazi wa wazazi walipata mvi pia katika umri huo(wakiwa vijana) kutokana na Genes ..seli zitoazo melanin(melanocytes) kushindwa kufanya kazi yake, na kurithiwa toka kizazi hadi kizazi(Ukoo).
UVUTAJI SIGARA:
Sigara huwa na kemikali iitwayo nicotine, ingawa sababu haziko wazi sana katika hili, tunahisi kuwa ni kutokana na kemikali hii kuwa katika damu kupunguza urutubishwaji wa kizizi cha unywele!
UPUNGUFU WA MAFUTA:
Sehemu ya juu ya fuvu la kichwa(Scalp) hutoa mafuta yaitwayo Sebum.Mafuta haya huzipa nywele mng'aro na rangi yake. Na hivyo upungufu wa mafuta haya husababisha nywele kuonekana zenye mvi.
Upungufu wa madini ya shaba(copper),Iodine, chuma(Iron)na Vitamini(Vitamin B) husababisha upungufu wa mafuta haya.
MAGONJWA:
Matatizo ya kiafya mfano upungufu vichochezi(Hypothyroidism), magonjwa/hali zinazoadhiri uzalishwaji/urutibishwaji wa melanin(Vitiligo)...n.k
Matibabu:
Cosmetic approach: Hutumia dawa kwa kupaka rangi na kupunguza muonekano wa rangi ya nywele(mvi).
Kutumia vyakula vyenye virutubisho(nilivyotaja hapo juu) kama vile karoti, ndizi samaki, maziwa n.k