Mamndenyi
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 43,242
- 60,939
Mods, chonde chonde, huu uzi nakuombeni muuache hapa hapa.
Leo tutengeneze mvinyo wa rozela; Kutengeneza mvinyo wa rozela .......... lita 20.
Viambaupishi;
rozela gramu 200;
sukari kilo 12;
chungwa 2
limao 1
hamira vijiko vidogo 6
sufuria,
ndoo ya lita 20
dumu la lita 20
air lock 1
mwiko 1
jiko na mkaa au kuni
NAMNA YA KUTENGENEZA
1. chemsha maji pamoja na rozela, chuja weka kwenye ndoo, ikianza kupoa weka sukari, juisi ya chungwa, limao juisi yake pamoja
na maganda ya nje yaparue (hii ni kwa ajili ya fleva), hamira, koroga funika vizuri.
2. koroga kila siku mara moja kwa muda wa siku sita
3. siku ya saba chuja, tia kwenye dumu la lita ishirini, weka air lock ikiwa na maji ndani (kama huna air lock unaweza
kutumia mrija ambao utauingiza kwenye chombo chenye maji) hii ni kwa ajili ya kutoa hewa ndani ya mvinyo wako;
4. Mvinyo mzuri ni ule uliosindikwa ukakaa muda wa kutosha ....... miezi sita na kuendelea.
5. baada ya miezi sita unaweza kufunga tayari kwa kuuza; ukitaka chupa, lebo, sili unaweza kuniuliza zaidi.
Karibuni kwa maswali maoni na ushauri.
Nawakilisha.