MVP Jeah Ahoua au muite "Slow Motion"

MVP Jeah Ahoua au muite "Slow Motion"

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Huyu dogo nimemsema na bado naamini anahitaji aongeze baadhi ya tuvitu katika kabati lake la zana ila kuna jambo moja amefanya ambalo linaenda kuigwa na vijana wengi.

Naongelea upigani wake wa penati. Pamoja na kwamba yeye siyo wa kwanza kupiga penati vile ila upigaji ule ni "signature" yake. Kuna kipindi kulikuwa na challenge ya kudance kwa slow motion, huyu jamaa amekuja na challenge ya kupiga penati kwa slow motion. Haina tofauti kabisa.

Haya Baraka Mpenja, nimeshakupa jina hilo rukhsa kulitumia, Jean Ahoua "Slow Motion" au unaweza kucheza nalo kidogo ukamuita "Slow but Sure".
 
92c5f5c9bf0f436a84ec8bd7ce49605b.jpg
 
Kweli kuna vitu vinashangaza ko playmaker anasifiwa kwa goli za faulo na penalties na sio kutengeneza nafasi huyu ahuwa ni suala la muda tu Ila hamna kitu huwezi hata mlinganisha na chama aliyechoka
Ndani ya duru la kwanza tu la msimu, Ahoua kafikia takwimu za Chama za msimu mzima uliopita kwenye magoli na assist. Na Chama hakuwa anakaa benchi kama Ahoua.

Aliyetunga namba alikuwa na akili sana, binadamu akitumia hisia, njano atakwambia ni nyekundu.
 
Tusubiri hadi mwezi wa tatu atakapokutana na wazee wa gusa achia twende kwao tuone kama atakuwa na maajabu ila kwa sasa bado ni mchezaji wa kawaida sana coz ktk mechi ngumu sijaona akifanya maajabu
 
Tusubiri hadi mwezi wa tatu atakapokutana na wazee wa gusa achia twende kwao tuone kama atakuwa na maajabu ila kwa sasa bado ni mchezaji wa kawaida sana coz ktk mechi ngumu sijaona akifanya maajabu
Wale wamejichokea amino hivyo wanachofanya sasa ni kujitutumua tu. Tena hii break ndio imewaharibia kabisa
 
Ahoua ni mchezaji mdogo na mzuri sana. Ila nachokiona anahitaji kukaza sana aseeh. Ana skills lakini hana pace, ana ball knowledge ila hana ubunifu kitu ambacho kwa nafasi yake hatakiwi kukosa kabisa. MVP wote waliokuja wanakaza sio kukaa kizembe. Namuona mbali hata kufikia level za kina Chama kama ataamua kufanyia kazi haya mambo.
 
Back
Top Bottom