Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,523
Risasi zarindima Kariakoo
POLISI Dar es Salaam jana walilazimika kufyatua risasi hewani baada ya kutokea mtafaruku kati ya wafanyabiashara ndogondogo, mgambo wa jiji na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) waliokwenda sokoni Kariakoo kuweka mtego wa kuwakamata mgambo wanaodaiwa kuwakamata machinga hao na kuwadai rushwa.
Vurugu hizo zilitokea mtaa wa Gerezani majira ya saa tisa alasiri baada ya machinga kwenda Takukuru kupewa fedha za mtego ambazo zilimnasa mgambo ‘mtarajiwa.'
Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla ya polisi kuingilia kati machinga walirushiana mawe na mgambo wengine wa jiji ambao hawakukubali kuona mwenzao anachukuliwa na askari wa Takukuru. Vurugu hiyo ilisababisha magari kusimama kwa muda na watembea kwa miguu kujificha dhidi ya ‘mvua ya mawe.'
Kabla ya tukio hilo inaelezwa kuwa machinga walikwenda ofisi za Takukuru ambako walipewa maofisa watatu waliokwenda nao Kariakoo na muda mfupi baadaye mgambo walifika eneo walilozoea kukamata na kupewa rushwa ndipo mambo yalipowageukia wakati wakiwanyang'anya wafanyabiashara hao bidhaa zao baada ya maofisa hao kuonyesha vitambulisho vyao na kuwaamuru kwenda Kituo cha Polisi Msimbazi.
Wakati walipokuwa wakiwapeleka kituoni mgambo hao hawakukubali ndipo vurugu zilipoanza kati ya machinga na mgambo hali iliyosababisha mgambo waliokamatwa kupigwa na machinga kabla ya wenzao kuingilia kati na baadaye polisi kuja kutuliza ghasia.
My take
Watanzania wamechoshwa na kuonewa na mafisadi, mawe yalianzia Tarime Rev Mtikila na Sengodo Mvungi kwenye uchaguzi wa mbunge na Diwani. Mzee wa kaya naye alioona adha ya mawe Mbeya, waalimu nao hawako nyuma kwenye kurusha mawe pale walipoona kiongozi wao amewasaliti kwenye mgomo, mawe mengine yamerushwa na hao vijana wa kimachinga zidi ya waonevu wao Mgambo...haya mawe kwanini yasihamie 2010 kuwanyima hao wanaoleta hizi dhiki kwa wanatanzania...huu ni mwanzo mzuri
Ushi