Mvua za msimu huu (Februari, 2022) hazieleweki

Papaa007

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2016
Posts
1,103
Reaction score
1,737
Habarini wanandugu wa JamiiForums nimekuwa nizifwatilia mvua za msimu huu kama mjuavyo kwa ajili ya kilimo lakini inashangaza sana kwani hazieleweki.

Kama huku Arusha yapata siku 4 mvua haijanyeshi sasa na jua lipo lali kama kawaida je ndo mvua za masika zimeisha? Ama hapo baadae mwez wa 3 zitaendelea?

Karbuni wataalam kwa ufafanuzi zaidi
 
Labda tumepewa mapumziko kidogo ya kukausha nguo na mazao yanayohitaji jua
 
Wa3 na 4 ndio miezi ya mwisho ya msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini..hivyo mvua bado ipo..imeachia gap kidogo tu itarudi hadi utaichukia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Haya ndiyo hasa mnatokea ya mabadiliko ya tabia nchi (climate change). Misimu halisi ya mvua za masika na vuli imebadilika na jambo hili linawachanganya sana wakulima wanategemea mvua. Kwa kawaida mikoa mingi hupata mvua za masika kuanzia Machi mpaka May/June. Sasa this time mvua zimeanza January mpaka February jambo ambalo limefanya hata maandalizi ya mashamba kuwa changamoto. Mamlaka ya hali ya hewa na Wizara ya Kilimo (maafisa kilimo/ugani) walitakuwa kuwaongoza wakulima kwenye nyakati sahihi za kupanda mazao..
 
Mkuu kiuhalisia mi huwa napenda mvua maana bora inyeshe ya kutosha jua likitoka ardhi ibakie kuwa na maji
 
Haya ndiyo hasa mnatokea ya mabadiliko ya tabia nchi (climate change). Misimu halisi ya mvua za masika na vuli imebadilika na jambo hili linawachanganya sana wakulima wanategemea mvua. Kwa kawaida mikoa mingi hupata mvua za masika kuanzia Machi mpaka May/June. Sasa this time mvua zimeanza January mpaka February jambo ambalo limefanya hata maandalizi ya mashamba kuwa changamoto. Mamlaka ya hali ya hewa na Wizara ya Kilimo (maafisa kilimo/ugani) walitakuwa kuwaongoza wakulima kwenye nyakati sahihi za kupanda mazao..
Na ndo maana nkataka wataalam watujuze maana kama ndio hvi aisee njaa itakuwa kubwa maana amna standardization ya mazao flan kwa kipind flan au mifugo flan ni changamoto kwa kwel ila Allah anajua zaidi..
 
Back
Top Bottom