Mvua za vuli kua chini ya wastani

Mvua za vuli kua chini ya wastani

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Habarini wakulima wenzangu.
Mimi mkulima mpya (form one) nimejiandaa haswaa na kilimo kipindi hiki kuelekea mvua za vuli.
Hofu yangu kuu ni mvua kwani kilimo nilichopanga kufanya kinategemea mvua.
Watu wapo site wanaissafisha pori eka za kutosha tu tena wamepiga kambi.
Narudi kwenye kurasa za mamlaka ya hali ya hewa ndio nakutana na taarifa kua mvua za vuli maeneo mengi ya nchi yetu zitaanza kwa kusuasua na zitanyesha chini ya wastani.
Nahisi kuchoka ninaposoma taarifa hizi.
Natamani nisitishe zoezi kabla sijapata hasara zaidi.
Ewe mkulima mwenzangu mzoefu hebu nipe neno lako nitalizingatia.
Nipige chini heri nusu shari, au niendelee kukomaa tu tutajua mwisho wa safari?
 
Unataka kulima zao gani, kwa ukubwa gani, na unapatikana mkoa gani wewe?
 
Back
Top Bottom