Mvua zilizoambatana na upepo zaezua nyumba zaidi ya 100 Ulanga mkoani Morogoro

Mvua zilizoambatana na upepo zaezua nyumba zaidi ya 100 Ulanga mkoani Morogoro

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo mbalimbali zimeendela kuleta athari ambapo zaidi ya nyumba 100 zimeezuliwa paa na nyingine kubomoka baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha katika Kijiji cha Mavimba Kata ya Milola Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro.

Baadhi ya Wahanga waliopata changamoto hiyo wamesema mvua hiyo iliyoambatana na mawe ilinyesha ambapo nyumba na miti vikiharibiwa

Soma pia: Polisi - Morogoro wathibitisha watu wawili wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Hassan Ally amesemaa baada ya mvua hiyo kunyesha wamelazimika kulala nje hadi Sasa huku jitihada mbalimbali zikiendelea.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Aulaudi Hasham, ametembelea katika Kijiji hicho kujionea athari zilizojitokeza ambapo amewataka Wananchi kuchukua tahadhari hasa kipindi hiki Cha mvua.
Screenshot 2025-02-06 130522.png
Screenshot 2025-02-06 130452.png
Screenshot 2025-02-06 130548.png
 
Poleni sana wakazi wa Moro. Mh. Salim niliona jana anaqeka ahadi za kujenga madarasa yaliyoezuliwa sasa sijui ni sound tu
 
Back
Top Bottom