Mvulana apigwa hadi kufa kwa kula mkate Kenya.

Mvulana apigwa hadi kufa kwa kula mkate Kenya.

Humble African

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
4,781
Reaction score
14,415
Mvulana apigwa hadi kufa kwa kula mkate Kenya

Saa moja iliyopita

Mshirikishe mwenzako

[http://ichef]Image captionRamani ya Kenya

Mtoto mmoja amefariki huku mwengine akiuguza majeraha baada ya kudaiwa kupigwa na shangazi yao kwa kula mkate katika kijiji cha Kiganjo kaunti ya Murang'a nchini Kenya.

Kulingana na runinga ya NTV nchini Kenya,Mtoto huyo wa miaka mitatu alifariki kutokana na majeraha aliyopata kwenye kichwa huku nduguye wa miaka 5 akiwa amelazwa katika hospitali ya Nyeri.

Wawili hao wanadaiwa kupigwa na shangazi huyo ambaye amedaiwa kuwa na akili punguani .

Majirani wanasema kuwa waliwasikia wavulana hao wakipiga kelele na kuelekea kuwaokoa kabla ya kuwapata wamelala ardhini wakiwa hawana fahamu.

Runinga hiyo inasema kuwa kulingana na mkaazi mmoja wa eneo hilo wavulana hao walikuwa wamewachwa nyumbani na bibi yao ili kukaa na shangazi yao.

Nilikuwa nimeenda kununua dawa ya mvulana mmoja kati yao baada ya ngozi yake kukumbwa na upele kabla ya kupata simu kutoka kwa mmoja wa jirani zangu akinielezea kilichotokea,alisema.

Kulingana na wakaazi wa eneo hilo Shangazi huyo aliwapiga wavulana hao baada ya kula mkate ambao ulikuwa wake.

Chanzo: BBC.
 
MTU MMOJA AUWAWA KIKATILI KUTOKANA NA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKOANI RUKWA - GUMZO TZ

Mtu mmoja ambaye ni mfugaji ameuawa kikatili na kundi la watu wenye hasira kali wa kijiji cha Kifone katika kata ya Mwimbi wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, baada ya kutokea kutoelewana kati ya wakulima na wafugaji.

Ukatili huo umetokea kufuatia kundi la Ngombe kuachiliwa kuingia kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu kiasi kikubwa cha mazao jambo lilizua taharuki ndipo kupelekea kifo cha mfugaji huyo.

Akizungumza diwani wa kata ya Mwimbi Claudio Mweupe, wamesema licha ya mfugaji huyo kuuawa kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga, lakini na mwenziwe naye Rehi Mwandu amejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na kundi hilo la wakulima,

Mpaka sasa majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga, huku msako mkali ukiendelea kuwatafuta watu wote waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mkononi.

Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura, akiongea kwenye kijiji hicho cha Kifone akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa chini ya mwenyekiti wake Bw Zelote Steven, amesema tayari wameanza kuwashikilia viongozi wa vijiji na vitongoji wanaoruhusu makundi ya Ngombe kuingia kwenye maeneo yao.
 
Back
Top Bottom