''Mvulana wa Messi'' atorokea Pakistan

Malcolm X5

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
1,639
Reaction score
2,752
Eheheh walimwengu ni watu wa ajabu sana....

===================

Mvulana mwenye umri wa miaka 5 ambaye picha yake ilisambaa katika mitandao ya kijamii akiwa amevalia shati ya Lionel Messi ametorokea nchini Pakistan.


Babaake Murtza Ahmadi amesema kuwa alipata vitisho vya kutekwa nyara ikiwemo kutoka kwa wahuni waliokuwa wakitaka pesa.

Baada ya mvulana huyo kuwa maarufu kutokana na shati yake yenye mistari ya bluu,nyota huyo wa Argentina alimpatia jezi mbili alizozitia saini pamoja na mpira.''Nampenda Messi''.



''Ni mfalme'',Murtaza ambaya ana matumaini ya kuonana naye aliiambia BBC.Babaake Murtaza anasema kuwa waliondoka nyumbani kwao huko Ghazni kwa sababu hali ilikuwa hatari kwake.

''Siku chache zilizopita nilipata simu kutoka kwa muhalifu mmoja .Alidhani kwamba kwasababu mwanangu alipokea Tisheti hizo kutoka kwa Messi pia alipata pesa na hivyo akataka agawiwe'',Arif Ahmadi aliambia BBC.

Sasa familia inahisi kwamba Quetta itatoa makaazi mazuri kwa maisha ya Murtaza na ndugu zake saba ambao wote wanalala chumba kimoja.

Chanzo: BBC Swahili
 
Huyo ndiye the KING after the KING Maradona's....full stop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…