BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Wabunge wa Somalia wamemchagua spika mpya leo Alhamisi Aprili 28, 2022 huku kukiwepo hali ya mivutano kati ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika AU dhidi ya Polisi.
Mivutano hiyo inadhihirisha mpasuko uliopo katika vyombo vya usalama vya Somalia, kutokana na kucheleweshwa kwa uchaguzi.
Aprili 27, 2022 Polisi watiifu kwa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kwa jina la Farmaajo, waliwazuia Wabunge waliokuwa wanajaribu kuingia kwenye ukumbi wa uwanja wa ndege ambapo uchaguzi ulikuwa unafanyika, wakiwaambia kwamba uchaguzi huo ulikuwa umeahirishwa.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble ambaye amekuwa katika mzozo wa madaraka na Rais Mohamed kwa miezi mingi, alikuwa amewaamuru walinda usalama kulinda sehemu uchaguzi ulikokuwa unafanyika ili kuwaruhusu Wabunge kushiriki zoezi hilo, hatua ambayo imesababisha kutokea msukumano kati ya maafisa wa usalama.
Baadaye, wabunge wamemchagua Sheikh Adan Mohamed Nur kama Spika wa Baraza Kuu la Bunge.
Source: VOA