Mvutano wazidi kuendelea kati ya Serikali ya Kenya na Mahakama kuhusu kurudishwa Miguna Miguna

Mvutano wazidi kuendelea kati ya Serikali ya Kenya na Mahakama kuhusu kurudishwa Miguna Miguna

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Mahakama Kuu ya Kenya imeamuru kurudishwa nchini humo kwa mwanasheria maarufu, Miguna Miguna ambaye alifukuzwa mara baada ya kumuapisha kiongozi wa NASA, Raila Odinga.

Jaji Luka Kimaru ameamuru Dkt. Miguna arudishwe Kenya kwa kuwa Serikali ilikaidi agizo la mahakama la kutakiwa kufikishwa mahakamani kwa mwanasheria huyo baada ya tukio la kumuapisha Raila Odinga.

Amesema kuwa hatua ya serikali kumfukuza Miguna ni kinyume cha katiba na sheria za kimataifa na kwamba mtu hawezi kupokonywa uraia wake.

Aidha, Miguna ni mzaliwa wa Nyando, Kaunti ya Kisumu lakini alipata uraia wa Canada alipoenda kusoma elimu ya juu na kuanza kufanya kazi za sheria.

Hata hivyo, kwa upande wa serikali imesema ilipaswa kumchukulia hatua kama hiyo Miguna baada ya kupata taarifa kutoka kwa usalama wa Taifa, kuwa mtu huyo ni hatari kwa usalama wa nchi.
 
Akubaliwe arudi tu, jamaa keshakosana na Raila kwa kusema kuwa wendani wa karibu wa Raila, Ndii na Magaya ni wasaliti na wanafanyia kazi Jubilee. Hii afrosinema ni ya ajab! Akirudi atajua demokrasia ndani ya NASA ni ya sampuli gani 😀
 
Serikali inatumia nguvu nyingi sana kwa huyu jamaa hadi wananiboa, huyu ni mropokaji tu ambaye anafanywa kuwa maarufu kila siku kwa sababu ya haya makelele.
Wampuuze alipuke lipuke atatulia, maana muda usio mrefu mtaona akifurushwa na wafuasi wa Raila maana na huko ameanza kuchokonoa.
 
Serikali ya Kenya leo imekubali kufata agizo la mahakama, la ku'deposit' pasipoti yake mahakamani. Lakini hamna cha kusherehekea. Pasipoti yenyewe ilishakuwa 'perforated'. 😀 Hii ni kulingana na sheria za uhamiaji pindi tu mtu anapokuwa 'deported'! Hata akirudishiwa hataweza kusafiri nayo, wameshaiharibu. Hadi pale atakapokabidhiwa nyingine mpya. Uliza na nani? Na Serikali hiyo hiyo! 😀 Afrosinema haijafikia kikomo. 😀
 
Duh lakini uraia wake wa Kanada unampa nguvu, kumbuka Canada inafuatilia kwa makini kila mtakachomfanya, na ipo tayari kumlinda.
 
Duh lakini uraia wake wa Kanada unampa nguvu, kumbuka Canada inafuatilia kwa makini kila mtakachomfanya, na ipo tayari kumlinda.
Mimi siungi mkono huo upuuzi hapa serikali imechemsha. Nafatilia nikijiuliza watamuacha arudi Kenya lini. Miguna Miguna ni kama Kalembe Ndile tu, wote ni kama wale walevi ving'ora, dawa yao ni kuwaachia wapige kelele hadi wachape blackout!
 
Back
Top Bottom