Mvuvi hodari

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
1. Ndimi mvuvi halisi, Kulla vuvi nalijuwa Nivuwaye mikambisi, na papa wenye khatuwa Wala sivui vingisi, mishipi haisumbuwa Nimekwambiya elewa

2. Sivuwi bahari ndogo, hatia nanga fuoni Havisimbika vigogo, vilivyozama majini Na wala Sivuwi ngogo, vidagaa na mbinini Siwavui asilani

3. Jabali hulijilisi, jishipi nikalitupa Haotea mifulusi, na nguru na mijipapa Si kasikazi Si kusi, khabari yangu nakupa Wala sivui kwa pupa

4. Na nivuapo malema, huingia ndani ndani Maji yangu ni ya pima, thalatha u thalathini Na ndiyo ninayozama, lema halibwaga tini Uliza mimi n'nani?

5. Na nivuapo maziyo, mavuvi ya kizamani Kwa hino hali niliyo, huvua kwa kutamani Hatafuta kiteweyo, cha wali mwema kombeni Haandaa siniani

6. Ela uvuvi wa juya, kuvua siutamani Sababuye 'takwambiya, ufahamiwe mwendani Ni kwambakwe huingiya, samaki waso thamani Kama wewe mwafulani

7. Ni Kuu yangu bahari, elewa sana elewa Huko hakwendi vihori, wala vyenu vimashuwa Shoti nahodha hodari, kisha ende kwa ngalawa Na milango kuijuwa



Cc Filipo
 
Aisee! Hiyo misamiati ya uvuvi, majina ya samaki na nchi kavu yamenitoa jasho! Good work portraying typical coastal culture.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…