Tman900
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 589
- 1,897
Alichoniadithia Babu Yangu mwaka 1996 Mwezi wa 6. Siku ya Juma Pili.
" Kulikua na Mvuvi ametoka baharini kuvua, amebeba Samaki watatu wazuri sana.
Akiwa anatembea alikutana na mfalme.
Mfalme kawapenda wale Samaki akataka auziwe hao samaki.
Lakini Mvuvi alikataa kumuuzia.
Ndipo mfalme akamuuliza kwa Nini hautaki kuniuzia Hawa samaki
Mvuvi akamjibu mfalme kua Hawa samaki watatu.
Huyu samaki wa kwanza naenda kulipa Deni, na huyu samaki wa pili naenda kumkopesha, na Samaki wa tatu naenda kumtupa.
Mfalme aliposikia maneno ya Mvuvi akaona huyu Mvuvi ajielewi akaita watumishi wake akawaamulu wamshike wamufunge.
Baada ya Muda akawambia watumishi wake, mleteni huyo Mvuvi, akamuliza nieleweshe kuhusu Hawa samaki.
Mvuvi akasema " Huyu samaki wa kwaza naenda Kulipa Deni, yaani nampeleka kwa wazazi wangu.
Maana wazazi walinitunza, nami ni zamu yangu kuwatunza wazazi wangu. Ni Deni walinikopesha matunzo nami nalipa Fadhila za wazazi.
Na huyu samaki wa pili, naenda kumkopesha, nawapelekea watoto wangu, Nawakopesha mana sijui kama watoto wangu watanilipa kama nami ninavyowalipa wazazi wangu kwa kuwajari na kuwahudumia kwa chakula na mahitaji muhimu.
Na samaki wa tatu naenda kumtupa. Yaani, huyu samaki nampelekea mke wangu. Kitu chochote unachompa mwanamke usiki hesabu kama kitakua ni kumbu kumbu kwa Mwanamke bali hesabu kama kitu ulichokitupa. Chochote unachokifanya kwa Mwanamke usikiweke akilini tena, na usahau.
Asante:Babu Yangu.