Mwabukusi: Kamati ya Nidhamu ilinihukumu sababu ya kukosoa viongozi wa juu wa serikali, hakuna aliye juu ya Sheria na Katiba

Mwabukusi: Kamati ya Nidhamu ilinihukumu sababu ya kukosoa viongozi wa juu wa serikali, hakuna aliye juu ya Sheria na Katiba

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Mwabukusi anasema aliadhibiwa kwa kwenda kinyume na maadili sababu ya kuwakosoa viongozi wa juu kwenye mkataba wa DP World, kuwa mkataba unaoiba rasilimali za tanganyika kiyume cha sheria.

Mwabukusi ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kamati kufafanya maamuzi ya kumuengua katika kinyang'anyiro cha kugombea Urais wa TLS

==

"Ukweli ni kwamba uamuzi wa Kamati ya Nidhamu, ambao ni uamuzi uliotolewa kwa njia ya kunionea ulinihukumu kwa sababu eti nimewakosea viongozi wakuu wan chi, hata kama ninazungumza ukweli sikutakiwa kuzungumza nitasababisha vurugu!

"Sasa ujinga wa namna hiyo ukiubeba kama wakili na kuamini ni hukumu halali.. nani alikwambia kuna kiongozi wa juu kuliko sheria na katiba ya nchi yetu? Kila mtu anakosolewa, cha muhimu ni kuwa ninapokukosoa nikukosoe kwa kweli.

"Mimi msimamo wangu niliadhibiwa kwamba ni unethical (kinyume na maadili) eti kwasababu nimewakosoa viongozi wa juu, lakini mimi sikuwakosoa viongozi wa juu kwa kuwaonea, nilisema kweli na ndio msimamo wangu kwamba mkataba ule wa IGA uliosaniwa kati ya Tanzania Bara na Dubai ni mkataba unaoiba rasilimali za Tanzanyika kinyume cha Sheria. Hatuwezi kwenda kinyuma na cha sheria au kuamua vinginevyo.

"Kwahiyo huwezi kunitisha kwa cheo chako ili niache ukweli. Mini nilikuwa nanukuu vifungu kwahiyo kama kweli ile kamati ilikuwa inaniona mimi nina makosa ilitakiwa kamati ile inioneshe sheria niliyovunja.

"Hakuna sheria yoyote inayokataza kukataza viongozi wanaotumia vyeo vyao kuiba katika mifuko na fursa walizopatiwa kijamii, tutawakemea na nitaendelea kuwakemea kwa macho makavu bila kupepesa. Hii nchi siyo yao na sisi siyo waalikwa. Wote sisi tuna haki sawa kwa mujibu wa shria katika taifa letu."



Pia soma ~ Wakili Kibatala: Nitasusia Uchaguzi was TLS kama Mwabukusi asiporudishwa kwenye orodha ya Wagombea
 
Hao mafisadi wameamua kujipachika ukiziwi
 
Back
Top Bottom